Je serikali imeshindwa kuwafanya wamiliki wa nyumba/majengo ya kupangisha na mafundi ujenzi kukata leseni za biashara ili walipe kodi?

jenga ya kwako ulipishwe kodi.watu wamekopa mishahara wanakula majani wakajenga wewe mlevi unataka watu wasijenge kuogopa kodi? hovyo kabisa.
 
jenga ya kwako ulipishwe kodi.watu wamekopa mishahara wanakula majani wakajenga wewe mlevi unataka watu wasijenge kuogopa kodi? hovyo kabisa.
We no lofa umekopa ujenge ya kuishi ww na makanyagio wako au ya biashara? Huo ni ufala pesa ya kodi nalipa mm mpangaji wewe unatopoka nini hapa mzee.
 
Sheria inasema 10% ya kodi ya nyumba wewe mpangaji inatakiwa uisalimishe TRA, inaitwa withholding tax.
10% ipeleke tra lakini unakumbuke kwangu ulete kodi uliyotimia, tofauti na hapo utaama bila kupenda. Maendeleo hayana chama.
 
Dawa hapa inatakiwa nyumba zote zitambuliwe ili mmiliki alipie kodi kwa serikali afu yeye ndio atabaki kubanana na wapangaji wake Kama tunavyolipa kodi ya ardhi au ikatiwe leseni ya biashara Kama guests house ilimradi tu ni nyumba ya biashara ikadiliwe kodi.
 
Serikali sio kwamba haioni ila nadhani hawajawa na mpango thabiti wa kudhibiti mfumuko wa kodi za nyumba kipindi watakapoamua kuanza kusanya hizo kodi maana lazima wenye nyumba wapandishe kodi tu ambapo kwa wenye nyumba wasio waaminifu watapandisha maradufu maana watakuwa kama wamepata sababu sasa!
 
Uchawi unaanzaga namna hii.[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…