Je, Serikali Ina Haki ya Kudhibiti Kile Unachoandika Kwenye Simu Yako?

Je, Serikali Ina Haki ya Kudhibiti Kile Unachoandika Kwenye Simu Yako?

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
136
Reaction score
292
Je, Serikali Ina Haki ya Kudhibiti Kile Unachoandika Kwenye Simu Yako?

Fikiria uko kwenye simu yako. Unamwandikia rafiki yako ujumbe wa kawaida:
• Unapoandika “oppa” (boyfriend) — simu inabadilisha kuwa “comrade”
• Unapoandika “South Korea” — inageuzwa kuwa “puppet state”

Hii si stori za kubuni. Hii ni hali halisi katika nchi ya Korea Kaskazini.
Simu zao zina mfumo maalum wa kubadilisha maneno yako kwa muda halisi ili yaendane na propaganda ya serikali.

Swali Linalofikirisha.......

Je, hii ni njia halali ya kulinda utamaduni na usalama wa kitaifa?
Au ni hatua hatari ya kufuta uhuru wa mtu hata kabla hajafikiri?
Kuna Makundi mawili kinzanii
Wanaounga Mkono Wanasema:
• “Ni njia ya kulinda utambulisho wa taifa.”
• “Kuzuia maneno ya kigeni ni njia ya kudhibiti athari za kibeberu.”
• “Propaganda ya nje inaweza kuivuruga nchi — lazima kuwe na ukuta wa kinga.”

Wanaopinga Wanasema:
• “Hii si kinga bali ni kifungo cha kimawazo.”
• “Simu inapaswa kuwa chombo cha binafsi, si cha serikali.”
• “Kudhibiti maneno ya mtu ni sawa na kumvua utu wake.”
❓Tujiulize Kwa Kina:
• Kama simu yako leo ingeanza kuchagua maneno kwa niaba yako, ungefanyaje?
• Uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi au ni zawadi ya serikali?
• Iwapo teknolojia ina uwezo wa kubadilisha fikra zetu, je, sisi bado ni huru?
MAONI YAKO NDIO MSIMAMO WAKO
🔸 Je, unaona udhibiti huu ni sahihi kwa ajili ya amani ya nchi?
🔸 Au unahisi ni unyanyasaji wa kiteknolojia unaofuta uhuru wa mtu mmoja mmoja?
Tupie jibu lako kwenye comment — tusikie sauti yako.
Huu si mjadala wa Korea Kaskazini pekee... ni mjadala wa kizazi kizima.
 
Back
Top Bottom