Je, Serikali kuja na kodi ya kichwa baada ya kuhitimisha zoezi la Sensa?

Je, Serikali kuja na kodi ya kichwa baada ya kuhitimisha zoezi la Sensa?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kama mtakuwa muna kumbukumbu nzuri waziri wa fedha alipendekeza kodi ya watu wazima yaani kodi ya kichwa.

Binafsi napenda kulipa kodi na kama serikali itaona uhalali wa kuleta Kodi mpya zingine ziletwe haraka.

Sasa hii kodi inapaswa iwe kwa madaraja. Ashukuriwe Mungu sensa imekuwa mgongo wa serikali kupata watu kwa madaraja.

Hivyo baada ya sensa tutarajie kodi ya kichwa kuanza rasmi.

Wananchi wanaambiwa jambo moja tu kuwa serikali inataka ijue idadi kamili ya watu ili wapate kuwapelekea huduma sawasawa na uhitaji wao ila hawaambiwi kuwa Serikali inataka ifanye tathmini ya kiwango cha kodi kwa kila mtu.
 
Ni vema kodi ya kichwa,kodi ya baiskeli,kodi ya kuuza mboga za majani na vijikodi "vituko" virudishwe.Itakuwa raha mustarehe na burdani maanani.Uhuru umezidi.😂😂😂😂
 
Wasituyumbishe hapa wanacholenga ni kuombea misaada Kwa wafadhili wanaowaita majina wanayoyajua! Kama walivyokuwa na kukubali COVID hatimaye kupewa Hela Lukuki na wakajengea matundu choo!
Huu ni ULAJI wa aina yake na wananchi wakiendelea kuishi maisha yao kama wakimbizi!!.
 
Hivi tuna Aina gani ya Wananchi wasiojua kwamba Sensa ni utaratibu wa kidunia siyo matakwa ya mtu mmoja au kundi la watu.

Wengi Wetu tunatafuta sababu ya kuunganisha shida zetu na mambo yasiyohusika kama tatizo ni TOZO tutafute ufumbuzi wa hiyo TOZO hasa double taxation NK.

Hata kama Serikali itaongozwa na hao unaowaamini lazima waweke TOZO ingawa wanaweza kuweka maneno tofauti lakini mwisho wa siku lazima tutalipa Kodi.

Muhimu Kodi isiwe ya kibabe,UJANJA usiumize Raia.

Sensabika mwanangu haina MADHARA kwako.
 
Naungana kn
Napendekeza walete kodi zote mpaka za matako, serikali hii hisiyoheshimu raia wake na raia waka3ndelea kuichekea nadhan sasa iamue hata kuwaua kabisa, utakuwa jambo jema
Napendekeza walete kodi zote mpaka za matako, serikali hii hisiyoheshimu raia wake na raia waka3ndelea kuichekea nadhan sasa iamue hata kuwaua kabisa, utakuwa jambo jema tu
Naunga mkono hoja watuuwe tu
 
"Sheria ya kodi ya kila Mtanzania mwenye miaka 18 na mwenye NIDA anapaswa kuwa na TIN na kutumia TIN kwenye kila muamala wa malipo au manunuzi, Itaanza kutumika tar 1 January 2023. Watanzania tujiandae mambo bado mabichiiiii.Rejea finance bill 2022"

Credit toka Twitter kwa msubhati.

Kwa namna ingine hii ni kodi ya kila kichwa hata uwe mteja unapiga debe mwananyamala stendi.
 
Mambo hayo na kila mwisho wa mwaka una file Tax returns
Screenshot_20220825-150527.jpg
 
Usiwadanganye watu. Tathimini ya kipato hupatikana katika HBS tu. Ila katika sensa unaweza kujua idadi ili ujue utakusanya kiasi gani kwa kiwango utakachokadria
 
ila hawaambiwi kuwa Serikali inataka ifanye tathmini ya kiwango cha kodi kwa kila mtu.
Nilimsikia waziri aakilisema hili alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha TV. Akasema "kila mtu atakadiriwa kulingana na kipato chake".

Ukiyaangalia maswali ya kwenye sensa yanapita mle mle . Sasa ninyi endeleeni kufunguka kuhusu vipato vyenu huko kwenye sensa. Tusije kulaumiana baadaye.
 
Kama mtakuwa muna kumbukumbu nzuri waziri wa fedha alipendekeza kodi ya watu wazima yaani kodi ya kichwa.

Binafsi napenda kulipa kodi na kama serikali itaona uhalali wa kuleta Kodi mpya zingine ziletwe haraka.

Sasa hii kodi inapaswa iwe kwa madaraja. Ashukuriwe Mungu sensa imekuwa mgongo wa serikali kupata watu kwa madaraja.

Hivyo baada ya sensa tutarajie kodi ya kichwa kuanza rasmi.

Wananchi wanaambiwa jambo moja tu kuwa serikali inataka ijue idadi kamili ya watu ili wapate kuwapelekea huduma sawasawa na uhitaji wao ila hawaambiwi kuwa Serikali inataka ifanye tathmini ya kiwango cha kodi kwa kila mtu.
NA YA BAISKELI itapendeza zaidi ili Makusanyo yawe mengi
 
Nilimsikia waziri aakilisema hili alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha TV. Akasema "kila mtu atakadiriwa kulingana na kipato chake".

Ukiyaangalia maswali ya kwenye sensa yanapita mle mle . Sasa ninyi endeleeni kufunguka kuhusu vipato vyenu huko kwenye sensa. Tusije kulaumiana baadaye.
Hilo ndilo litakalofuata
 
Back
Top Bottom