Jamani wanajanvi, sioni kama ni mantiki kumruhusu mtumishi akajiendeleze kwa kuchukua shahada ya pili ya ualimu kisha akirejea kazini serikali inashindwa kumlipa mshahara wa masters. Hii inawavunja moyo walimu wenye nia ya kujiendeleza kitaaluma. Hii ni kwa walimu wa s/msingi na s/sekondari. Vyuo vikuu hawahusiki, pia diploma na grade A teachers sijui ndio maana sijazungumzia. Nawasilisha.