Je serikali kutokumlipa mshahara mwalimu mwenye masters ya ualimu ni sawa?

Je serikali kutokumlipa mshahara mwalimu mwenye masters ya ualimu ni sawa?

Ingekuwa rahisi watu wasingekuwa wanadisco vyuo vya ualimu. Ualimu nimeusoma ni mgumu tena sana tu. Unajua Curriculum development and evaluation? Philosophy of educatio je? Educational Psychology? Acha kabisa msuli ni muhimu labda mimi nilikuwa na uelewa mchache ndio maana naona mambo yalikuwa magumu chuoni.
 
Jamani wanajanvi, sioni kama ni mantiki kumruhusu mtumishi akajiendeleze kwa kuchukua shahada ya pili ya ualimu kisha akirejea kazini serikali inashindwa kumlipa mshahara wa masters. Hii inawavunja moyo walimu wenye nia ya kujiendeleza kitaaluma. Hii ni kwa walimu wa s/msingi na s/sekondari. Vyuo vikuu hawahusiki, pia diploma na grade A teachers sijui ndio maana sijazungumzia. Nawasilisha.
S
Sio Mwalimu tu hata Watumishi wengine wenye Masters wanapewa increment mbili tu. Sijui kwanini Watu wanadhani Walimu pekee ndio wanaokosa haki zote za msingi kuliko watumishi wengine
 
Mimi mtu mwenye DEGREE YA EDUCATION namuona kama mwanafunzi wa form6 wa mzumbe au ilboru tena anaweza akamzidi mwalimu mwenye DEGREE

kweli na ndo mana mwl mwenye degree anaweza akafundisha kuanzia naxar mpaka advance level!
 
Ingekuwa rahisi watu wasingekuwa wanadisco vyuo vya ualimu. Ualimu nimeusoma ni mgumu tena sana tu. Unajua Curriculum development and evaluation? Philosophy of educatio je? Educational Psychology? Acha kabisa msuli ni muhimu labda mimi nilikuwa na uelewa mchache ndio maana naona mambo yalikuwa magumu chuoni.

you are right
 
Kwa maana hiyo Tanzania walimu wenye ngazi ya master hawahitajiki? Mwisho iwe elimu ya shahada tu? vipi kuhusu Deploma na Advance deploma? Je wataalamu waliobobea katika research za kielimu watapatikana vipi?
 
Mkuu unachanganya mambo, ujue kwenye kila kazi mtu anayoajiriwa kuna majukumu yake, sio kila kazi unafanya hizo reasearch hata kama una Phd, kingine lazima ujue siyo kila kazi unaporudi kutoka masomoni unapandishwa daraja, kazi zingine mpka usubiri pale zitakapotangazwa hizo promotions ndio uombe, kuna faida za kusoma hata kama sio kwa leo, ujue kwenye ngazi mshahara kwa kila elimu kuna kugota kwenye kupanda madaraja kulingina na elimu yule aliyesoma zaidi yeye anapanda zaidi
 
Haya maombi yakimfikia Mh. Rais Dr Samia Suluhu Hassan atayafanyia kazi,
tuna Rais msikivu Sana, sku moja watu wenye Shahada mtakuwa na rank yenu ya salary, hii itafanya walimu wasitafute kuhamia sehem nyngne baada ya kuhtm masters zao
 
Nadhani kuliko kulalamika walimu mmngeandika muswada kuiomba serikali ilitazame hilo kwa jicho la karibu sana. Kama ni kweli Mhitimu wa Masta upande wa Elimu ni useless basi haina maana kabisa ya kwenda kumahiri hicho kitu ilhali hakina manufaa yoyote.
 
Back
Top Bottom