SJamani wanajanvi, sioni kama ni mantiki kumruhusu mtumishi akajiendeleze kwa kuchukua shahada ya pili ya ualimu kisha akirejea kazini serikali inashindwa kumlipa mshahara wa masters. Hii inawavunja moyo walimu wenye nia ya kujiendeleza kitaaluma. Hii ni kwa walimu wa s/msingi na s/sekondari. Vyuo vikuu hawahusiki, pia diploma na grade A teachers sijui ndio maana sijazungumzia. Nawasilisha.
Mimi mtu mwenye DEGREE YA EDUCATION namuona kama mwanafunzi wa form6 wa mzumbe au ilboru tena anaweza akamzidi mwalimu mwenye DEGREE
Ingekuwa rahisi watu wasingekuwa wanadisco vyuo vya ualimu. Ualimu nimeusoma ni mgumu tena sana tu. Unajua Curriculum development and evaluation? Philosophy of educatio je? Educational Psychology? Acha kabisa msuli ni muhimu labda mimi nilikuwa na uelewa mchache ndio maana naona mambo yalikuwa magumu chuoni.
Mkuu unachanganya mambo, ujue kwenye kila kazi mtu anayoajiriwa kuna majukumu yake, sio kila kazi unafanya hizo reasearch hata kama una Phd, kingine lazima ujue siyo kila kazi unaporudi kutoka masomoni unapandishwa daraja, kazi zingine mpka usubiri pale zitakapotangazwa hizo promotions ndio uombe, kuna faida za kusoma hata kama sio kwa leo, ujue kwenye ngazi mshahara kwa kila elimu kuna kugota kwenye kupanda madaraja kulingina na elimu yule aliyesoma zaidi yeye anapanda zaidiKwa maana hiyo Tanzania walimu wenye ngazi ya master hawahitajiki? Mwisho iwe elimu ya shahada tu? vipi kuhusu Deploma na Advance deploma? Je wataalamu waliobobea katika research za kielimu watapatikana vipi?