Lengo la Magufuli kuanzisha maduka mapya ya dawa nje ya Hospitali za umma ilikuwa kuwakomoa wenye maduka binafsi nje ya hospitali hizo , ukimsikia alipokuwa anatia nia hiyo utanielewa, maana aliropoka hadharani...
Naamini kila hospitali hapa nchini ina structure tofauti, au miundombinu kimajengo yako tofauti sana. Ukiongelea muhimbili naweza kukubali kwamba kila wodi labda iwe na pharmacy yake, kwasababu haya majengo ni makubwa sana, Sewa haji, Mwaisela, Kibasila, Out patient clinic, Wodi ya watoto huku, wodi za wazazi kule,psychiatry huku, na MOI na kadhalika ni eneo kubwa na kila jengo linahitaji kujitegemea kama tunaweza.
Ingawa zamani sana, nakumbuka Muhimbili ilikuwa na Pharmacy hapo jingo la Out-patient ili serve purposes vizuri tu, MOI najua wanayo yao, huku JK heart institute wanayo yao. Binafsi naona kama Muhimbili inawezekana, lakini hizi hospitali zingine zinaweza kuwa na Pharmacy mbili moja kwa wagonjwa wa nje na nyingine kwa wagonjwa waliolazwa tu.
Mfumo ulitakiwa uwe hivi, mgonjwa akiingia amuone daktari, apate vipimo, arudi kwa daktari kisha aandikiwe dawa, aende pharmacy apewe hapo hapo hospitali, na kama analazwa basi dawa apewe kwa utaratibu wa kitabibu na madaktari husika kwa usaidizi wa ma-nurse.
Sio mgonjwa kalazwa mnaambiwa mkanunue dawa nje, sasa wamemlaza ili iweje?
Na wagonjwa wa nje kutembea na prescription barabarani wengi huuziwa dawa zisizo kwa kutokujua na hawa wenye maduka baridi huko barabarani.
Hili ni tatizo kubwa na sugu. Lakini akiuziwa pharmacy ndani ya hospitali sio rahisi kuuziwa dawa fake, na kama dawa aliyoandikiwa na daktari haipo, mpharmacia anaweza mwambia mgonjwa nenda kamwambie daktari hiyo dawa aliyokuandikia haipo au haikufai, mwambie akubadilishie iliyopo hapa kwetu ni aina Fulani. Na kwa kufuata taratibu mgonjwa anasaidika na kuapa matibabu sahihi na kupona.
Hii kuzunguka kila kona ya mji unatafuta dawa bei rahisi, unauziwa dawa zisizo kwa bei unayoona inakufaa na unatumia kumbe unajiumiza badala ya kujisaidia.
Kila wodi kuwa na pharmacy kwa hospitali ndogo za wilaya haiwezekani kimfumo na kimuundo, pia sioni kwanini iwe hivyo, ziwepo mbili tu wagonjwa wa nje na moja wagonjwa wa ndani, na kama hospitali siyo kubwa sana wanaweza kushare duka moja hospitali nzima, cha msingi dawa ziwepo.
Nurses wa in-patient hufuata dawa za wagonjwa waliolazwa pharmacy na kuzigawa kulingana na utaratibu na muda aliopangiwa mgonjwa aliyeko chini ya uangalizi.
Hawa wa nje tununue hapo hapo pharmacy na kama hakuna dawa mfamacia atoe taarifa kwenye medical meeting asubuhi au kwa chief medical officer au DMO muda wowote ili naye atoe taarifa kwa madaktari na matatibu waliopo.
Hakuna ubaya wa kuwa na maduka Hospitali mkuu, hapo ndio hasa mahala pake, Bima ni issue nyingine, taaluma ya tiba ni issue nyingine na siasa ni issue nyingine kabisa.