Uchaguzi 2020 Je, Serikali kuwa na Maduka ya kuuza Dawa za Binadamu ndiyo kuimarisha Sekta ya Afya?

Magufuli aliziiba pesa za wastaafu atashindwaje kuzikwiba na hizo za bima
 
Ni njia nzuri ya kuua biashara za watu. Huko serikalini kuna watu akili zao haziko sawa wanatengeza sera kufanya siasa, badala ya kuinua Afya na uchumi .Awamu ya 5 inachosha sana wanaendesha inchi km familia ama kampuni
 

Congrats mkuu.

Ningekuwa naweza ku opt LIKE hata elfu 1 ningefanya hivyo mkuu.

Umechangia ki weledi kabisa mkuu.
 
Wewe ndio una mawazo mufilisi kabisa.Hivi huoni kwamba ukifanya dawa ziwe more accessible na zikauzwa kwa bei nafuu kuliko kwenye maduka binafsi umeboresha hudumu za afya!Na ni nani asiyejua kwamba kwenye hospitali zetu za serikali sasa dawa zinapatikana zaidi kuliko kwenye awamu zote zilizopita?Usipotoshe mambo mkuu kwa malengo yako ya kisiasa,be realistic.After all maendeleo ni process,serikali haitafanikisha kila kitu mara moja,lakini adhma yake ni kuwezesha dawa zipatikane kwenye hospitali zote kila wakati. Tunajua tatizo la wizi wa dawa lipo,lakini hili nalo naamini serikali italimaza,ni swala LA muda tu.Rome was not built in a day.
 
"ilitakiwa dawa nyingi ziwekwe kwenye maduka ya kila wodi ili kuimarisha huduma". Mkuu hapa kidogo umeniacha. Ninachofahamu wodi hazina duka la dawa. Hospitali inaweza kuwa na labda dispensing mbili kwa mfano. Watu wa wodini kwa mfumo wa zamani ndiyo wanaenda kuchukua dawa pharmacy kubwa na kuzileta wodini kwa ajili ya wagonjwa. Walipoleta mfumo mpya wa malipo na duka la dawa ndipo unatakiwa uende dukani au mgonjwa mwenyewe akachukue dawa azilete wodini. Na mfamasia yupo mmoja ambaye anakaa pale pharmacy na siyo kila wodi kwamba kuna mfamasia,hapana. Nilikuwa najaribu kuweka sawa kidogo,tuendelee kuelimishana.
 
unafahamu kwamba kila wodi ina chumba cha watoa dawa ?
 
Samahani unamaanisha nini unaposema "kila wodi ina chumba cha mtoa dawa"? Mimi nipo wilayani kwenye hizo shughuli nifafanulie ndugu. Asante tunaelimishana tu
unafahamu kwamba kila wodi ina chumba cha watoa dawa ?
 
Serikali watoe ruzuku kupitia bima ya afya ambao watafanya tathmini ya mahitaji ya madawa na vifaa tiba ambavyo vinahitajika na hospitali na vituo vya umma na binafsi na hivyo kuwezesha upatikanaji rahisi na nafuu wa dawa na vifaa, hii itasaidia pia wale wasio kwenye mfumo rasmi wa bima ya afya, mfano kaya maskini kuweza kuchangia kiasi kidogo, tuseme sh. 10,000/= kwa mwaka na kuweza kupata huduma za afya zinazoridhisha.
 
Labda isiwe serikali ya viwonder
 
Naunga mkono.

Inawezekana mleta UZI hajui na hana uhakika na anachokisema mkuu.
 
Hawana nia njema na sisi hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…