Je, Shahawa au Mbegu za mwanaume huwa zinakaa kwenye mwili wa mwanamke kwa siku au Masaa mangapi?

Je, Shahawa au Mbegu za mwanaume huwa zinakaa kwenye mwili wa mwanamke kwa siku au Masaa mangapi?

Salamu wanajamvi!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, napenda nifahamu mwanamke anapolala na kujamiiana na mwanaume zile shahawa, mbegu na majimaji vinapoingia kwenye uke wake huwa zinakaa muda gani??

Inajulikana kuwa uke unao uwezo wa kujisafisha na kutoa zile shahawa baada ya muda au siku fulani. Na mwanamke huwa anajisafisha baada ya lile tendo. Lkn kujisafisha kwake mwanamke hakumalizi ule uchafu, uchafu husafishwa na kuwa Safi kwa kusafishwa na uke wenyewe. Je, uchafu mpaka uishe na uke au uchi wa mwanamke uwe Safi kabisa inachukua masaa mangapi au siku ngapi?
Yaani malighafi za kuujaza ulimwengu unaita uchafu!? Huo unaouita uchafu una watu zaidi ya milioni 100 humo! Yaani mabao 70 tu ya mwanaume mwenye afya njema ni zaidi ya population yote hii unayoiona duniani kuanzia mtaani kwako, kwenye TV hadi magazetini.

Mtake radhi Mungu na sote aliotuumba kwa mfano wake (wanaume), pamoja na watoto wote.
 
Utungisho ni kuunganika kwa kiiniseli cha mbegu za uzazi za kiume na kiiniseli cha ova. Ili utungisho utokee, ni sharti mbegu za kiume ziingie ukeni katika kipindi kisichozidi siku 3 kabla ya ovulesheni au katika kipindi kisichozidi siku moja baada ya ovulesheni. Kipindi cha ovulesheni ni kifupi kwa sababu mbegu za kiume na ova huishi kwa muda mfupi, na zote hufa zisipokutana na kuungana katika kipindi hiki. Kufuatia ovulesheni, ova huchukuliwa na fimbria ya mshipa wa falopio iliyo katika upande huo wa mwili ambapo ovari iliachilia ova. Ova hubaki kwenye mshipa wa falopio ikiwa ingali hai na inayotenda kazi vyema kwa muda wa saa 12 - 24. Mbegu za kiume zinaweza kuishi kwa muda mrefu zaidi kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke, kwa takriban saa 72, ingawa nyingi hufa mapema.

Mbegu za kiume ziingiapo ukeni huogelea kupitia katika seviksi huku zikiingia kwenye uterasi, kisha kuingia kwenye mishipa ya falopio. (Tazama tena Mchoro 3.3.) Utungisho wa ova hufanyika katika mshipa wa falopio. Kukazana kwa misuli ya kuta za uterasi na mishipa ya falopio husaidia kusongesha mbegu za kiume. Mbegu hizi zinaweza kuogelea milimita kadhaa kwa sekunde, hivyo zinaweza kufika katika mishipa ya falopio kwa muda wa takriban dakika 15. Hata hivyo mamilioni ya mbegu hizi hufa zikiwa zingali zinasonga.
 

Attachments

  • Screenshot_20240724_005906_Chrome.jpg
    Screenshot_20240724_005906_Chrome.jpg
    423.5 KB · Views: 13
Back
Top Bottom