Suala la faida na hasara za kijamii linatoka wapi wakati hili ni suala la kiimani?! Anyway, kuna mahali niliandika kama ifuatavyo:-
Hivi kwanini wasio Waislamu ndo wanakuwa more concerned na habari za mwezi kuliko Waislamu wenyewe?
Anyway, iko hivi...
Kuna wale wanaosimamia kile ambacho kilitamkwa na Mtume bila kujali mabadiliko ya teknolojia na kuna wale wanaofanya maamuzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia duniani!!!
Kauli ya Mtume inasema kwamba "Fungeni na fungueni kwa kuuona mwezi, na kama hujaonekana, basi zitimie siku 30".
Yaani, kama mlianza kufunga tarehe 1, ikifika tarehe 29, chunguzeni kujiridhisha kama mwezi umeonekana. Kama mkiona, basi kesho msifunge na kama hamjauona, kesho endeleeni kufunga kama siku ya mwisho!!
Kwenye hadithi hii wametaja maximum distance kuonesha, ikiwa Eneo X mwezi umeonekana na Eneo Y hujaonekana lakini distance between X and Y ipo ndani ya umbali uliotajwa, basi Y nao watafanya kama X kwa hoja kwamba, inawezekana hawajauona kutokana na sababu mbalimbali, hususani za Kijiografia.
Lakini kubwa zaidi, hata kwenye ulimwengu wa leo, wanaangalia kikanda zaidi!
Sasa wale Conservatives... wanasimamia kwenye hiyo hadithi! Kwamba, ikifika Mwezi 29, na ukaonekana, basi watu wataanza kufunga au kufungua! Kama hujaonekana, watasubiri siku 30!
Kundi hili hawataki zile habari za kwamba Saudi Arabia mwezi umeonekana kwa sababu hadithi haisemi mwezi ukionekana Saudi Arabia basi fuateni huo wa Saudia!!
Kundi la Pili, wao wanaangalia mabadiliko ya kisayansi na teknolojia ambayo zama za Mtume hayakuwapo!!!
Hawa, wanachoamini ni kwamba, mwezi ukionekana Saudi Arabia basi LAZIMA na Tanzania itakuwa umeonekana tu hata kama mmeshindwa kuuona!!! Na kwavile siku hizi teknolojia ya upashaji habari ipo, basi wakisikia Saudi Arabia umeonekana, basi wao wanaenda nao sambamba!!
Kule Saudi Arabia wana namna tatu za kujiridhisha kuonekana kwa mwezi ambazo ni: by naked eyes, binoculars au kwa kutumia Wanajimu wakati sisi tunategemea kuuona kwa macho TU!
Pamoja na njia hizo 3, Saudia wanaiamini zaidi njia ya Wanajimu kuliko matumizi ya binoculars!!!
Kwahiyo it's not the BIG ISSUE kama msio Waislamu mnavyotaka kuifanya!!
Waislamu wenyewe, individually or collectively wanajua wafuate theory ipi. Na sehemu mbalimbali duniani huwa wanatumia theories hizo mbili!
Wanaopenda sana kutumia mwezi wa Saudi Arabia ni Ansal Sunni ambao wapo sect ya Imam Hanbal wakati East Africa, especially Kenya na Uganda, wapo sect ya Imam Shaffi!
Na kaeni mkifahamu kwamba hata Rwanda na Uganda, NOT necessarily kwamba wanakuwa wameuona kwenye nchi zao; unaweza kukuta wao wanafuata ile theory ya kwamba, kama mwezi umeonekana Mashariki ya Kati basi hata Rwanda/Uganda ni sawa tu kwenda nao sambamba!!
Hata hivyo, especially for astronomical point of view, ni nadra sana kuona mwezi unaonekana baada ya siku 30 kwa miezi miwili consecutively... yaani, kama mlianza kufunga baada ya mwezi kuonekana siku ya 30 basi kuna uwezekano MKUBWA SANA, mwezi unaofuata utaonekana baada ya siku 29!!