Je, Sheria Inaruhusu Wakili Wa Mshitakiwa Kuwa Shahidi Wa Mshitaki?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Turejee kesi ya serikali dhidi ya Kamanda Tundu Lissu ambapo mawakili wa serikali walitaka wakili Kibatala aliyekuwa upande wa Lissu awe shahidi namba 1 wa mshitaki.

Kwa kuwa Wakili Kibatala tayari alikuwa na maslahi na Kamanda Tundu Lissu, mawakili wa serikali walipata wapi imani kwamba Kibatala atakuwa turufu kwao?

Na je kisheria mawakili wa serikali walikuwa na trick nzuri au walishindwa cha kufanya?

Tujadili
 
BansenBurner; Bila shaka hata kwako hili ni jambo hujawahi kulisikia ama sivyo?

karibuni @WANASHERIA
 
Sio hiari mtu kuwa shahidi upande wa serikali kwenye kesi za jinai. crown ina mamlaka kisheria kumlazimisha ( compel ) mtu yoyote ambaye ana knowledge na jambo ambalo anaweza kuiwashia taa mahakama ili iweze kuhukumu kwa haki. Hivyo kuchaguliwa au kuitwa kama shahidi ni lazima la kisheria na ukikataa unaweza kuchukuliwa hatua ni watu ambao wana kinga kisheria hawawezi kulazimishwa kuwa mashahidi. Hivyo kama mawakili wa serikali wameona kwamba anaweza kuthibitisha mashtaka yao atalazimiswa tu apende asipende na akikengeuka ( turn hostile ) watamshtaki.
 
Kizuri serikali yenyewe imeonyesha kuwa beki yake inakatika sana... hahahaaa hii forward ya Lissu na Kibatala haijapata kutokea duniani.. Lissu amethibitisha kuwa yy ni mwalimu wa sheria hapa Tanzania... ccm oyeeeeeeeeeeee
 
Vifungu gani vina_Cement hoja yako?
 
Ukikagua vyeti vya mawakili na wanasheria wa serikali wamefaulu vizuri sana, ila ukija kwenye usimamiaji wa kesi vichwani ni ziro. Walikua wana kariri madesa pale kwenye mdigrii. Ovyo sana
 
Hivi unaweza kumlazimisha mume awe shahidi dhidi ya mkewe au mke dhidi ya mume katika kesi ya jinai?
Tuanzie hapo!
 

Unamlazimisha awe shahidi, akisema hajui hilo unalotaka alishuhudie utamfanyaje? Sheria hii inaweka mpaka upi kati ya mashahidi wa kutishiwa ama wa kutengenezwa? Kibatala amegoma, sheria inakaaje? Atalazimishwa kusema uwongo mahakamani kwa mujibu wake kwamba kinachodaiwa yeye hakijui, hakukisikia na wala hakuwepo kwenye hilo tukio?

Analishwa kiapo cha kusema kweli, anasimama kama shahidi wa serikali halafu yeye ana dispute utetezi wenu, mahakama itamhukumu kwa kugoma kusema ilichomlazimisha aseme au serikali baada ya shauri itamshughulikia nyuma ya pazia, ili kumshikisha adabu?

Analazimishwa kuandika maelezo kinyume na utashi pamoja na ukweli anaoujua yeye, aki turn hostile mahakamani nini adhabu yake?

Hivi katika sheria zetu, kuna sehemu Mahakama imepewa uwezo wa kumhukumu mtu "kumfukuza ahame Tanzania na kumfutia uraia" hata kama ni Mtanzania wa asili? Anachaguliwa nchi y akwenda kuishi na familia yake? Gharama za kumwondoa Tanzania na ukoo wake analipa nani ili asirudi tena?

Hii sheria kama haipo, ninapendekeza itungwe. Nitaeleza baadaye ni kwa nini nasema hivi. Kwa sasa nisaidie ufafanuzi hapo juu.
 
Walichokosea ni kumtoa messi uwanjani wakamwingiza peleee haki ya nani hawakuaminu lissu aliposimama kujitetea najua walifahamu hii game tushapigwa tatu bilaaaa hahahaha sorry nipo nje ya mada kidogo
 
kwa hiyo Kibatalala alipomuuliza state attorney "unanilazimisha niwe shahidi..." ina maana haijui hii sheria ya kulazimishana ushahidi? Kibatalala that is, hajui?
 
Hivi unaweza kumlazimisha mume awe shahidi dhidi ya mkewe au mke dhidi ya mume katika kesi ya jinai?
Tuanzie hapo!
Huwezi ukalazimishwa kutoa ushahidi kulingana na kanuni kuu inayotamkwa katika kifungu cha 130(1) cha sheria inayohusiana na ushahidi Tanzania. Ila kifungu kidogo cha pili yani 130(2) kinatoa mbadala wa kanuni kuu kuwa mmoja ya mwanandoa anaweza kutoa ushahidi dhidi ya mwenzake mfano makosa ya ubakaji kama ilivyokuwa kesi ya Babu seya. Pia kasome sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 CHAPTER XV itakupa mwanga katika makosa ambayo unaweza kulazimishwa kutoa ushahidi.
 
Hivi unaweza kumlazimisha mume awe shahidi dhidi ya mkewe au mke dhidi ya mume katika kesi ya jinai?
Tuanzie hapo!
kuna baadhi ya case mwanamke au mme hawez toa ushahidi dhid ya mwezake maana hawa watu wawil tunaasume ni kitu kimoja....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…