Sio hiari mtu kuwa shahidi upande wa serikali kwenye kesi za jinai. crown ina mamlaka kisheria kumlazimisha ( compel ) mtu yoyote ambaye ana knowledge na jambo ambalo anaweza kuiwashia taa mahakama ili iweze kuhukumu kwa haki. Hivyo kuchaguliwa au kuitwa kama shahidi ni lazima la kisheria na ukikataa unaweza kuchukuliwa hatua ni watu ambao wana kinga kisheria hawawezi kulazimishwa kuwa mashahidi. Hivyo kama mawakili wa serikali wameona kwamba anaweza kuthibitisha mashtaka yao atalazimiswa tu apende asipende na akikengeuka ( turn hostile ) watamshtaki.
Unamlazimisha awe shahidi, akisema hajui hilo unalotaka alishuhudie utamfanyaje? Sheria hii inaweka mpaka upi kati ya mashahidi wa kutishiwa ama wa kutengenezwa? Kibatala amegoma, sheria inakaaje? Atalazimishwa kusema uwongo mahakamani kwa mujibu wake kwamba kinachodaiwa yeye hakijui, hakukisikia na wala hakuwepo kwenye hilo tukio?
Analishwa kiapo cha kusema kweli, anasimama kama shahidi wa serikali halafu yeye ana dispute utetezi wenu, mahakama itamhukumu kwa kugoma kusema ilichomlazimisha aseme au serikali baada ya shauri itamshughulikia nyuma ya pazia, ili kumshikisha adabu?
Analazimishwa kuandika maelezo kinyume na utashi pamoja na ukweli anaoujua yeye, aki turn hostile mahakamani nini adhabu yake?
Hivi katika sheria zetu, kuna sehemu Mahakama imepewa uwezo wa kumhukumu mtu "kumfukuza ahame Tanzania na kumfutia uraia" hata kama ni Mtanzania wa asili? Anachaguliwa nchi y akwenda kuishi na familia yake? Gharama za kumwondoa Tanzania na ukoo wake analipa nani ili asirudi tena?
Hii sheria kama haipo, ninapendekeza itungwe. Nitaeleza baadaye ni kwa nini nasema hivi. Kwa sasa nisaidie ufafanuzi hapo juu.