SoC01 Je, Sheria isemayo kata mti panda mti inatekelezwa?

SoC01 Je, Sheria isemayo kata mti panda mti inatekelezwa?

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Je, Kwa mtazamo wako unalionaje hilo?

Katika mazingira yetu wengi tumezaliwa na kuikuta miti ambayo mwanzo tulijua tu ni kwa ajili ya kivuli na kutupatia kuni na mbao tu, Lakini mara baada ya kukaa darasani kwa vipanda kadhaa ndipo tukatambua maajabu na umuhimu wake katika anga hewa kwamba husaidia katika uzalishwaji wa mvua na pia inasaidia kuondoa hewa chafu zote zilizopo katika mazingira yetu na kuliacha anga hewa likiwa safi kabisa.

Lakini bado shida ipo kwenye utekelezwaji wa sheria za maliasili tulizojiwekea ambapo katika maeneo mengi unaweza ukakuta miti imekatwa lakini hakuna mche utakaoonekana kupandwa eneo hilo ikiwa kama ishara yenye kuthibitisha utekelezwaji wa sheria hiyo na hatimaye imekua ni kaulimbiu isiyo na utekelezwaji na Matokeo yake watu wamekuwa wakikata miti Na kuharibu uoto wa asili uliopo katika eneo fulani kwa lengo la kuchana mbao kujipatia kipato na hata kujipatia kuni kwa ajili ya biashara na matumizi ya majumbani.

Jambo linalopelekea kuharibu kwa kiasi kikubwa maisha ya viumbe na mimea kiujumla. Na endapo hali hii inavyoendelea itasabisha jangwa ukame na njaa kwa viumbe wote na hata kupoteza maisha hivyo tungeliomba sekta husika iweze kulichunguza hili na iweke sheria kali ambazo kama mtu akipatikana na hatia hii ashindwe kujinusuru, Hii itakua imeweza kwa kiasi kikubwa kunusuru maisha ya viumbe na kuthibiti mabadiliko ya tabia ya nchi inayotokana na uvunaji holela wa misitu unaotokana na shughuli za kibinadamu

Asante kwa kunipa muda wako
 
Upvote 0
Back
Top Bottom