Je, shetani/ibilisi anatoka koo zipi miongoni mwa koo za majini? Wazazi waliomzaa ni akina nani?

Kwa hiyo?
Ukijua wazazi wa ibilisi itakusaidia nini? Au usipojua wazazi wake itakusaidia nini?

Kwa kifupi kuna koo 70 za majinni. Koo 7 zinazomuhusudu Mungu na Koo 7 hazimuhusudu Mungu zimepitiliza kwenye ushetani mpaka Majinni wenzao wanawaogopa. Kumbuka nabii Suleyman a.s alipomuomba Mungu amuoneshe Majinni wote katika maumbile yao ya asili. Malaika Jibril a.s akashuka kutoka Mbinguni na kumtaarifu Suleyman katika sijda aliyokuwa akimuomba Mungu akisali. Kwamba Mungu amemkubalia dua yake, Malaika Jibril a.s akatoa wito wa sauti kali Kuwaita majini wote waje mbele ya nabii Suleyman. Majinni wote walalifika huku Malaika wengine wakiwachunga mithili ya mchungaji anavyowachunga mifugo yake.......

Kuhusu majini ni kweli wao ni viumbe wa mwanzo kuishi kwenye huu ulimwengu kabla ya binadamu. Ukielewa hivyo inatosha, tosheka na hayo. Na ukitaka kujua kwa nini jeshi la malaika walimuomba Mungu wamchukue ibilisi unajua sababu? Unajua kwa nini alikuwa anaitwa Abaa sijda? Na kukataa kumsujudia Adam ni mwingi wa kujiona mkubwa. Rejelea aya katika Suratul Baqarah inayoelezea ibilisi alipokataa kusujudu inasema "ILLA IBILIISA ABAA WASTAKBAR, WAKANA MINAL KAAFIIRIN. Na kama sijakosea rejelea katika suratul Twaha Mungu alipomuuliza " Kipi kilichokuzuia kutii amri yangu pindi nilipo kuamrisha? Ibilisi alijibu KHALTANII MIN'NARIIN WAKHALTAHU MIN TWIIN" hapo ndipo lilipo jibu LA swali lako la ibilisi kukataa kumsujudia nabii Adam.

Alimwambia Mungu kati ya hilo dongo(mchanga) ambaye ni binadam na Mimi uliyeniumba na moto ni ipi malighafi yenye thamani? Alikisia na alikosea kwa sababu ya Kiburi chake akalaaniwa.
 
Tuanzie hapa, wewe kumjua binadamu wa kwanza ni Adamu imekusaidia nini?
 
Wewe mafundisho haya umeyapata wapi mbona yanapoteza uhalisia kabisa
 
Hivi Mzee baba sasa mapepo yanayowavamia watu wao wqpo kundi gani
 
Kumjua Ibilisi kaumbwa kwa moto imekusaidia nini?
Una mapungufu ya taaluma ya kuelewa maana.

Asili ya matatizo ya Adam na uzao wake ni ibilisi, bhasi hata kumjua adui wako ni wa namna gani ni najisi? Ukumbuke hatujatofautiana na wazazi wa ibilisi bali tumetofautiana na yeye ibilisi, ndiyo maana Qur'an haijaona umuhimu wa kuzungumzia wazazi wake. Bali Qur'an inachukua matukio muhimu.

Ndiyo maana nikakuambia kujua wazazi wa ibilisi au kutowajua ni elimu isiyokuwa na manufaa na ujinga usiyodhuru.

Usiku mwema.
 
KUNA WATU WANAANDIKA HOJA!!
KUNA MWINGINE ANAANDIKA STORY!!.
sasa kama by merely assumptions tu mtu unakomaa kubishia vitu ambavyo hata huna hoja ya msingi Wala ushahidi au vyanzo vyovyote vya habari !!
Tuendelee tu kule celebrities kutupigia story za kina Zari!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…