IBILISI/SHETANI NDIO KIZAZI KILICHO KATIKA MAFICHO YA UPEO WA MACHO NAE IBILISI NA MAJINI WALIUMBWA KABLA YA ADAM NA ALITOKANA NA KUUMBWA KWA NDIMI ZA MOTO "Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto."(QURAN 15:27).....KIHISTORIA IBILISI ALIKUWA MCHAMUNGU KIASI CHA KUITWA BABA WA SIJDA KUTOKANA NA KULE KUMSUJUDIA MWENYEZI MUNGU KIASI CHA KILA SEHEMU YA ARDHI ILIENEA SIJDA ZAKE....ALIASI KWA KULE KUTAKABALI KWAKE NAKUJIONA BORA ZAIDI YA ADAMU NA KUKATAA KUMPA SIJDA YA HESHIMA ADAM PINDI ALIPOUMBWA ``11. Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu
isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.12. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.13. Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa
walio duni.14. Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.15. Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula.16. Akasema: Kwa kuwa
umenihukumia upotofu, basi
nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.17. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.18. Akasema:Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote."(QURAN 7:11-18)
.....IBILISI ALIKUWA KTK KIZAZI CHA MAJINI "Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa
miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na
dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu."(QURAN 18:50) ILA BAADA YA KUASI KWAKE ALITEREMSHWA DUNIANI...IBILISI ANA KABILA ZAKE IKIWA NI PAMOJA NA MAJINI/PEPO/ NA MASHETANI(KUNA NA MASHETANI WATU) NALO NDILO LINAUNDA JESHI LAKE ``Na
majeshi ya Ibilisi yote.``(QURAN 26:95)
HAKUNA MAFUNGAMANO/USHIRIKA BAINA YA MAJINI NA BINADAMU HATA KAMA UNA KUNUFAISHANA"Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu!
Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua."(QURAN 6:128)..ILA MWENYEZI MUNGU AKITAKA YEYE KWA IDHINI YAKE ANAWAAMRISHA MAJINI YAMTUMIKIE MJA WAKE APENDAVYO KAMA ALIVYOYAAMRISHA MAJINI YAMTUMIKIE MFALME NABII SULEIMAN "Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyayushia chemchem ya shaba. Na katika majini walikuwako walio kuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anaye jitenga na amri yetu katika wao, tunamwonjesha adhabu ya Moto unao waka."(QURAN 34:12)
SOMA ZAIDI KWENYE POST HII
JINI,SHAYTWAAN NA UCHAWI