Je, shilingi milioni kumi inatosha kujenga nyumba nzuri kijijini?

sa hapo mbona ukianza na boma fresh hela ikikata unaezeka vyumba viwili unahamia na kupambana kumalizia mambo mengine


Ni idea nzuri. Kwa mujibu wa maoni yako na wadau wengine hapa, napata picha kidogo. Nafikiri ni vizuri niende na flow tu mpaka pale ntakapofikia. Hata nisipomaliza lakini hii bajeti yangu itanifikisha mbali.
 
Itakufikisha mahali ila haitotosha tatizo ni kuwa pwani ujenzi unatumia tofali za block ambazo ni expensive
Mbona tunaambiwa watu wa Pwani ni wavivu sana. Huwa wanaweza vip ku afford hizo tofali za blocks ?
 
Kwa nyumba za Dar za kuweka dirisha fremu ya mbao + wire mesh + Mesquito itatosha, lakini ukifanya kisasa kuangaika na Aluminium na finishing ya kisasa hutafika popote
 
Sikubali na wewe,

kwasababu mtoa mada hajataja ukubwa wa nyumba yake, idadi ya vyumba, ukubwa wa chumba kimoja kimoja
Kwa mantiki hii umekubaliana nami kuwa 10m haitoshi
 
Sikubali na wewe,

kwasababu mtoa mada hajataja ukubwa wa nyumba yake, idadi ya vyumba, ukubwa wa chumba kimoja kimoja


Mimi nimemetoa bajeti yangu, shilingi milioni kumi na kuuliza je inawezekana kupata nyumba yenye nafasi huko kijijini? Au ni nyumba ya aina gani naweza kujenga huko kijijini. Sikutaja aina au ukubwa wa nyumba kwasababu naomba ideas kutoka kwa wadau hapa. Asante.
 
Mbona tunaambiwa watu wa Pwani ni wavivu sana. Huwa wanaweza vip ku afford hizo tofali za blocks ?
No waliojenga pwani wengi sio wazaliwa wa pwani bali ni wageni *wakuja* asilimia kubwa ya watu wa pwani bado wanaishi ndani ya mbavu za mbwa japo sio wote but as time goes on wanabadilika
 
Uzoefu wangu:
1.Mtu aliyejenga anamkatisha tamaa anayetaka kujenga. Utasikia nyumba bila million 100 hujengi.
2. Biashara? Bila milioni 200 hufanyi biashara.

Yaani, ilimradi akukatishe tamaa tu. Sasa sijui ni unafiki, wivu au husda, sielewi.
Na ukishafanikiwa sasa, wanaanza maneno; kaiba, anaringa, na mengine mengi.
Ndugu usirudi nyuma; watu wanajenga nyumba na wanahamia kabla ya kukamilka.
Anahamia chumba kimoja ilimradi kina choo na kimeezekwa.

Ukitaka kujenga, usifikirie ukubwa wa nyumba, bali angalia ulichonacho na uanze na hicho.
Mimi huwa ninasema; ukitaka kujenga, anza kujenga tu, maana usipoanza hautajenga: yaani kama una hela ya msingi au rumu moja wewe jilipuwe: achana na watu na maneno yao yasiyo na tija.
Watz wapo wanafiki kupita maelezo!
 
Kama unataka kujenga, ukisikiliza baadhi ya watu humu ndani hakika huwez kijenga kamwe, milioni kumi si haba itakufikisha mbali sana japo inaweza usiifanye nyumba kuwa ya kisasa.

Ambao hawajajenga humu ndani ndiyo wa kwanza kukatisha watu tamaa, MTU anatoa kauli za Kipuuzi eti Million kumi inajenga shimo la choo!!!! Kama una kiwanja hebu plan nyumba ndogo ya wastan utafika mbali na hata mama yetu utashangaa amesha hamia.
 
Hii ni point kubwa sana ndugu umesema vizuri yaan ukiwa na eneo dogo basi
 
Bati 100 ni nyingi mno chumba kimoja cha 10 kwa 13 kinahitaji bati tufanye 16 mara vyumba 4 ni bati 60 na kitu. Roughly fanya bati 70 kwa hiyo 1.7 na usafiri misumari pia kilo 30 ni mingi mno kilo 20 inatosha mbao inategemea na muinuko wa paa kwa mimi milion 10 inatosha Kabisaa
 
Asprin toa sababu kwa nini haitoshi
Haitoshi kwa sababu haitoshi. Hiyo ni hela ndogo sana kujenga nyumba "ya kisasa yenye nafasi". Kuna tofauti kubwa sana kati ya nyumba na banda.
 
Ili awe anarudia rudia dukani si ndio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…