Je, Simba SC tunalo la kujifunza kutoka kwa Yanga SC?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa unajua Simba wako mbali kuliko Yanga, sasa simba wajifunze nn kutoka kwa team aliyo iacha mbaliii??

Hivi unajua unachoongea lakiniii??
 
Huyo anayeiga kwako mbona kakuzidi kila kitu kuanzia makombe, H2H yan hufui dafu kwake kwa lolote na bado aige kwakoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Watu Humu Mnajibu Kama Sio Mashabiki na Wapenzi Wa Mpira, Tuachane na Historia zote za Nyuma sijui tulifanya nini ikawa nini, Tunaongelea sahizi wakati timu inaelekea Kwenye Mashindano Ya SuperCup, Haiwezekani Kama Kocha Alishiriki katika Kusajili wachezaji hadi sasa Awe hana First 11 yenye uhakika na Ushindi.

Ukiangalia Simba Ya Mgunda na Sahizi ni sawa? Ukiangalia Simba Ya Gomez? Sven? Ile Simba Ya Pira Biriani?

Na Hapa Tujifunze kwa Yanga kwanini Wao wamesajiri wachezaji kama Sisi ila Wao wachezaji wameweza kuingia Kwenye Mfumo na Kuwa Gumzo? Wakati sisi Tulienda Hadi Uturuki na Timu bado inajitafuta?

Kocha wetu viongozi waliacha Katika Kambi Ya Wiki 4 Uturuki Kocha Kakaa na Timu Wiki 1,Shida nini Kwenda Kusoma Ukocha?
 
Huyu ni simba tangu zamani na humu anajulikana labda wewe hujui .

Amesema ukweli sababu ana uchungu na team yake tutolee ushabiki wa kipumbavu hapa pokeeni ushauri hapo.
Ndo maana yanga inayopigiwa mfano mtoa mada juzi ilichukua ngao ya hisani kwa mtibwa.Ni juzi tu simba ameshinda bao nne dhidi ya mtibwa.
 
Reactions: BRN
Kwa hiyo simba haishindi, uanamichezo wako upo wapi sasa?Toka simba aliposajili mara zote ameshinda.Au mpira ni nini?
 
Reactions: BRN
Simba ilionekana bora kwakua Yanga ilikua inatembeza bakuli na bado Yanga ilitoa ushindani wa kutosha.
Yanga ilikua ikianza na Ditram Nchimbi na substitution yupo Yipe.

Sasa timu zinalingana ki uchumi na maji na mafuta yanajitenga.
Mafuta yakabeba ndoo kwa timu ya mfano.
 
Reactions: BRN
Kwa mtazamo wangu naona kuna sehemu mbili ambazo mtani wangu unakosea

Kwanza kupoteza falsafa ya timu. Timu lazima iwe na falsafa yake mfano kumiliki mpira, kupaki basi n.k na pale mnapofanya usajiri either wa mchezaji au kocha basi mnaangalia anaeingia kwenye falsafa yenu, baada ya kuondoka uchebe falsafa ya timu imekua haieleweki kila kocha anaekuja anakuja na falsafa yake hii inasababisha kuanza upya kila anapokuja kocha mpya falsafa ya simba ni kumiliki mpira kwa pasi fupi akisogelea lango la adui wakati hii sio falsafa ya Robertino. Uki-establish falsafa ya timu hata anapokuja kocha mpya ataendelea pale alipoishia mtangulizi wake. Angalia falsafa ya Nabi za Gamondi wote wanamiliki mpira tofauti tu Gamondi anacheza mpira wa direct zaidi.

Pili kiwewe cha kuwauza Chama na Miquisone. Kabla Chama hajaenda Morroco na Miquisone hajaenda Misri niseme wazi scouting ya simba ilikua vizuri sana ila baada ya hao wawili kuondoka ni kama timu ilipata kiwewe inavyoonekana hawa wawili waliuzwa huku timu ikiwa haijajua wa kusajili kuziba mapengo yao matokeo yake ikanunua wachezaji wengi kwa kukulupuka na kubahatisha. Kuna cha kujifunza hapa unapouza key player usipaniki. Angalia utulivu wa yanga baada ya kumuuza Mayele mchezaji ambae alikua kipenzi vya mashabiki. Hawakukulupuka na kusajiri wachezaji ovyo ovyo kwa sababu walishapiga hesabu ya nani ataziba iyo nafasi.

Tengenezeni falsafa imara ya timu iwe ndio muongozo wenu katika kufanya recruitmemt ya wachezaji na kocha, pili boresheni timu ya scouting. Binafsi naona hayo ndio maeneo mawili ambayo yanga imewapiga bao.

NB; Ni mtazamo wangu tu watani zangu, turekebishane kistaarabu
 
KUNA MDAU ALISEMA KUA TIMU ITAKAYOKUA INACHEZA SIMBA NI ILE ILE YA MSIMU ULIOPITA WA 2022/23 [emoji2957]
 
Umewachokoza makolo, povu linawatokaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Nnachokiona ,
Simba kiusajili Ni nzuri,
Ila inaharibiwa na mbinu za kocha,
 
Kwanza simba sio mbovu ila shida wanalinganisha na Yanga lazima ionekane mbovu tu,

Robertihno alipewa simba kwenye kipindi cha mpito hivyo simba bado ipo kwenye transition kuweni na subira
 
Wakati Simba wanatangaza nafasi ya kocha, si ungepeleka CV yako ili uchujwee?

Kawaingize wewe kwenye mfumo, ukiiongelea Simba bila kuhusisha Yanga ingekuajee??

Utopoloo wee
 
Kwa mtazamo wangu naona kuna sehemu mbili ambazo mtani wangu unakosea

Kwanza kupoteza falsafa ya timu. Timu lazima iwe na falsafa yake mfano kumiliki mpira, kupaki basi n.k na pale

NB; Ni mtazamo wangu tu watani zangu, turekebishane kistaarabu
Pengo LA mayele linazibwa na Musonda?? Ndo kwa mantiki yako? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe ndio unajua kuwa kocha hana first eleven? mlikaa kikao gani?
 
Angalia Namna ambavyo Pacome, Yao, Max, Skudu, Konkon nk walivyo wahi kuingia Kwenye kuliko akina Luis, Onana, Kramo, Ngoma nk.
Kwani zimechezwa mechi ngapi tangu reference yako ya Ngao ya Hisani?
 
Pengo LA mayele linazibwa na Musonda?? Ndo kwa mantiki yako? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nahitaji reply za watu wa michezo na itapendeza zaidi wakiwa wanaume wenzangu
 
Simba ni Simba na Yanga ni Yanga, hata jezi zao zipo tofauti. Ni ujinga kuwaza ulivyo waza.

Ikiwa una mahaba na Yanga songa mbele na Yanga yako, tuachie Simba yetu.

Kama washabiki wa Simba ndo mna Tabia hizi, mtangoja sana kufanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…