Tuseme tu ukweli mimi ni simba damu na nina kadi ila siridhishwi mfumo wa mwalimu,kikosi ina wachezaji wazuri ila kila mechi ni kama tunabahatisha, tuseme ukweli kocha wetu ndo tatizo,anaweza akawa na falsafa yake lakini inashindwa kufanya kazi ipasavyo.
Una Chama,Ngoma, Baleke , Miquison ,Phiri lakini anashindwa kuunganisha timu,wachezaji wana papara. Enzi za Uchebe , Kishingo ,Gomes na Mgunda unaona soka likitandazwa safi,kocha kapokea timu msimu unaisha,wameweka kambi na mechi kibao za kirafiki nakini hamna soka linaloeleweka.
Hata kikosi (first 11) haieleweki kama ameshapata maana huoni hata combination ya wachezaji,mtu kama Saido ni kama anaingilia nafasi za wengine na kuharibu, Simba hadi sasa inatumia mpira wa ngumu na uwezo wa wachezaji lakini siyo mipira ya kupanga mashambulizi ya maana.
Wachezaji ni wazuri ila kocha anafeli san