Je, simu yako inapata sana joto?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Simu yako inapata Sana Joto !!!



Ulikua unatumia simu fresh tu ghafla simu imebadilika na kuanza tabia za ajabu inapata joto sio mchezo 😏, ukitumia kidogo ilo joto lake unaweza sema umechemsha chai kwenye heater πŸ˜€.




Kuna sababu nyingi ambazo upelekea simu Zetu kupata sana joto wakati tunazitumia kama vile
βœ“ kutumia simu kupitiliza yani wewe masaa mengi unatumia simu upelekea kupata moto
βœ“ Mwanga Mkubwa wa simu yako upelekea simu kupata sana joto
βœ“ kuchaji chaji simu Kila mara au unakuta simu inashinda kwenye chaji upelekea kupata sana joto



βœ“ chaji unayotumia sio original mbovu au betri bovu upelekea simu kupata sana joto
βœ“ kutumia simu kwenye jua upelekea simu kuua kwa kupata sana Joto, kuua betri pamoja na mfumo mzima wa circuit ya simu



βœ”οΈ Kutokufanya update kwenye simu yako Kwan app au system inakua outdated na kupelekea simu kushika sana moto.
βœ”οΈ Virus au malware , kupitia virusi vinavyoingia kwenye simu usababisha mfumo wa simu kutumika kwa nguvu na kupelekea kupata sana joto.

Unafanyaje kuwa Salama
βš™οΈ Punguza Mwanga kwenye simu yako
βš™οΈ Usipende kuweka makava magumu kwenye simu
βš™οΈ Usitumie simu kwenye jua Kali jihadhari
βš™οΈ Tumia chaji imara au original
βš™οΈ Badilisha betri
βš™οΈ Hakikisha unapenda kufanya update ya app na mfumo mzima wa simu yako.
 
Noted,,πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…