Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini?

Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini?

------mama mkulima wa China aondokana na umaskini kwa kutengeneza fagio la mabua ya mtama


Na Hassan Zhou
1617932707264.png


Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China hivi karibuni ilitangaza waraka uitwao “Kupunguza Umaskini: Uzoefu na Mchango wa China”. Waraka huo umeeleza jinsi Chama cha Kikomunisti cha China CPC kilivyoongozana na watu wa China kupambana na umaskini katika miaka 100 iliyopita, haswa baada ya mkutano mkuu wa 18 wa CPC, kutokana na juhudi kubwa zilizodumu miaka minane, mwishoni mwa mwaka jana, China ilikuwa imetimiza lengo kuu la kutokomeza umaskini uliokithiri kama ilivyopanga, na kwamba katika kiwango cha sasa ambacho ni juu ya kile cha Benki ya Dunia, watu karibu milioni 100 waishio vijijini wameondokana na umaskini. Je, siri ya China ni nini? Wacha tuangalie jinsi familia kadhaa za kichina zilivyofanikiwa kuondokana na umaskini, ili upate jibu la siri.
Waswahili husema, “anayeweza kugeuza yalala kuwa utajiri”. Kwa kuuza fagio linalotengenezwa kwa mabua ya mtama, mwanamke mkulima Li Yaomei sio tu alimsomesha binti yake chuo kikuu, bali pia amelipa pesa nyingi alizokopa kutoka kwa ndugu na marafiki zake.
1111.jpg

bibi Li Yaomei akitengeneza fagio la mabua ya mtama

Li Yaomei ni mkulima kutoka kijiji maskini cha Longyuan, kaskazini magharibi mwa China. Aliishi maisha magumu na hali yake ya afya haikuwa nzuri, lakini shida haibishi hodi, ajali ya barabarani aliyoipata Li ilimlazimisha kukopa Yuan laki tatu, sawa na dola za kimarekani elfu 40. Hata hivyo Li Yaomei mwenye bidii alienda shambani wiki mbili tu baada ya kutoka hospitali. Na ndani ya miaka mitatu, mama huyo alitengeneza mafagio zaidi ya elfu 25 kwa kutumia mabua ya mtama yaliyotupwa na watu, na kupata fedha za kulipa deni lote.

Mafanikio ya Li Yaomei yalileta mwamko mpya, kijiji cha Longyuan kilijenga kiwanda cha kuwasaidia maskini, na Li, akiwa msimamizi wake, anawaongoza wakulima wengine sita maskini kushiriki kwenye kazi ya kutengeneza fagio la mabua ya mtama. Kila mwaka, kiwanda hicho kinaweza kupata oda za mafagio zaidi ya elfu 10, hivyo Li Yaomei na wenzake wamekodi mashamba na kupanda mtama. Ili kupata oda zaidi, wao pia wanauza mafagio mubashara kupitia mtandao wa internet. Mchumia juani hula kivulini, kadri siku zinavyoenda, maisha ya wakulima hao yanaboreka, na wana matumaini zaidi na siku za baadaye.

Mama huyo amenikumbusha kuwa “penye nia pana njia” na maisha ya neema yanapatikana iwapo tunafanya kazi kwa bidii. Kitu kingine ninachotaka kusisitiza ni soko, kwani bidhaa nzuri haina maana kama haina soko.
22222.jpg

mwanamke mchina akipiga ngoma na kijana wa Afrika
3333.jpg

bidhaa za kiafrika zikionyeshwa katika maonyesho China

Kila mchina aliyeenda kutalii nchi za Afrika alinunua vitu vya sanaa sokoni. Lakini kwa kutegemea mauzo ya msimu mfupi tu wa utalii, ni vigumu kubadili maisha ya watu. Kama sehemu nyingi za vijijini hapa China, nchi za Afrika pia zina vyama vya ushirika au Wajumbe wa Nyumba Kumi. Taasisi hizo zinapaswa kutumiwa vizuri ili kukusanya rasilimali na kuwatafutia watu soko, bila kujali ni katika mtandao wa internet au maonyesho halisi.

Vitu vinavyosahaulika na watu kama mabua ya mtama pia vinaweza kusaidia kutimiza ndoto. Iwapo njia sahihi zinatumiwa, watu sio tu wanaweza kuondokana na umaskini, bali pia ni fursa nzuri ya kuonesha vitu vya sanaa vinavyobeba tamaduni za kipekee za kiafrika kwa dunia nzima. Leo kwangu kesho kwako, hakuna jasho linalopotea bure.



Ikiwa una swali ama maoni kuhusu makala hii, unaweza kunitumia barua pepe katika anuani hapa chini.

64909787@qq.com

Pia unaweza kunifuatilia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook: @yoyoasema
 
Back
Top Bottom