Je, sisi kama taifa tunakosea wapi kuelekea nchi ya kiviwanda na uwekezaji?

Je, sisi kama taifa tunakosea wapi kuelekea nchi ya kiviwanda na uwekezaji?

Sijapata kuelewa ni kipi hasa una maanisha, unapaswa kuiwekea sentensi yako katika ustadi mzuri zaidi wa kueleweka na jamii nzima. Karibu tena kwa ufafanuzi wako uliobora.
Neno "tunaelekea" umekwisha litumia hivyo nami nimelitumia kulingana na muda, uliopita, huu au ujao.
 
You have a cartel posing as a government
,And much worse,a half- intelligent voting bloc..you'll never get anywhere
 
Serikali kupitia wizara ya nishati inapaswa kujiza titi katika umeme safi kwa mazingira kama nyongeza ya megawatt kwa ajili ya matumizi ya uwakika kwa viwanda.
 
Megawatt tunazo zalisha haziwezi kukidhi mapinduzi ya kiuchumi ya kiwanda, ni ngumu kuvutia wawekezaji wa kiviwanda kwa kiwango kidogo cha umeme tunacho zalisha kwa mwaka[ megawatt ].
 
Ningependa kuwa karibisha wadau wote wa Jamiiforum watao penda kushiriki katika mjadala huu wenye swali liulizalo.

Je sisi kama taifa tuna kosea wapi katika wizara ya nishati kuelekea katika nchi ya kiviwanda na uwekezaji ?

Katika mjadala huu ningependa kutoa mfano utakao tupa mwangaza kidogo katika hilo swali tuta kalo lijadili.

Mfano una husisha ulinganifu wa taifa la kiviwanda na uwekezaji duniani, taifa la China na taifa letu la Tanzania katika swala la nishati. Mfano :-

Kwa mwaka wa 2021 taifa la China lime tengeneza zaidi ya megga watt billion nane na million mia tano [ 8, 500, 000, 000 + ] huku taifa letu la Tanzania likiwa limetengeneza zaidi ya megga watt elfu moja na mia sita [ 1, 600 + ].

Je sisi kama taifa tuna kosea wapi katika wizara yetu ya nishati kuelekea nchi ya kiviwanda na uwekezaji ukilinganisha na namna wenzetu wanavyo fanya katika wizara zao za nishati katika ustawi bora wa kiviwanda na uwekezaji .

Karibuni nyote.
Watanzania weusi na Waarabu wa bongo wanapenda retail kuliko manufacturing. Wahindi kidogo wanapenda processing, manufacturing na workshops.
Waarabu na Wabongo wanakimbilia kwenye kununua mbasi na malori.
Hawataki kuweka mtaji katika utengenezaji wa vitu vidogo vidogo tunavyoagiza.
Tubadilike. Tupeleke nguvu kwenye manufacturing. Tuagize mitambo lkn sio finished products.
 
Tuna paswa kujifunga mkanda na kuweka bajeti kubwa katika wizara ya nishati itakayo saidia ukuaji ulio bora wa wizara hii kwa ajili ya viwanda.

Tunapaswa kufanya tafiti na kuongeza njia nyingi zaidi za kupata umeme wa uhakika, kuliko kutegemea chanzo cha maji pekee kama umeme wa kuendesha uchumi wa taifa.

Tunapaswa kuongeza njia za kupata umeme wa uhakika kama:-i, umeme wa kinyuklia
ii, umeme wa jua
ii, umeme wa upepo
iii, umeme wa gesi
iv, umeme wa makaa ya mawe
 
Watanzania weusi na Waarabu wa bongo wanapenda retail kuliko manufacturing. Wahindi kidogo wanapenda processing, manufacturing na workshops.
Waarabu na Wabongo wanakimbilia kwenye kununua mbasi na malori.
Hawataki kuweka mtaji katika utengenezaji wa vitu vidogo vidogo tunavyoagiza.
Tubadilike. Tupeleke nguvu kwenye manufacturing. Tuagize mitambo lkn sio finished products.
Kweli kwa kiwango kikubwa tuna hitaji zaidi light industries/ viwanda vya kati ili kuua bidhaa utitiri za kichina zinazo tiririka nchini na katika bara letu la Afrika, tuta kuwa na nafasi kubwa zaidi sisi ya kutengeneza fedha tofauti na China kama tukitilia mkazo katika hili.
 
Tuna hitaji uwekezaji katika mashamba ya umeme jua yakutosha katika taifa hili, wizara ya nishati inapaswa kuzingatia hili swala kwa makini zaidi.
05014_30MWQinghai-1200x675.jpg
china_aid_renewable_energy_asia-1.jpg
GettyImages-1232517061.jpg


Tuna hitaji pia kuzingatia uvunaji wa umeme kwa njia ya upepo kupitia bahari na mikoa yenye kasi kubwa ya upepo.
3500.jpg
IMG_bl05_solar__panel_2_1_A48L0VRC.jpg
5db7e8a6a310cf3e97a367bd.jpeg
 
Zaidi ya megawatt 600,000 China ana zalisha kwa mwaka kupitia umeme jua.
Na
Zaidi ya megawatt 400,000 za umeme upepo China ana zalisha kwa mwaka.

Tuna paswa kujiza titi kwa bajeti iliyo shiba katika haya maswala kama mfano ulio bora kwetu kwa wizara yetu ya nishati.
 
Back
Top Bottom