Riba ni gharama ya kukopa pesa.
Ikipanda, kukopa pesa kunakuwa na gharama zaidi.
Kwa mfano, sasa hivi inepanda kut9ka 5% mpaka 5.5%.
Maana yake, Benki ya Biashara kukopa shilingi milioni moja Benki Kuu , ilikuwa unalipia shilingi 50,000, lakini sasa watalipia shilingi 55,000.
Na benki za biashara zikishakopa kutoka benki kuu, nazo zinaongeza cha juu chake, kwa kuangalia watu hawalipi mikopo, kujiwekea faida benki zisipate hasara, nk. Mkopo ukifika kwako, unaweza kukopa 1 million ukalipa 1.25 million kwa sababu 0.25 million inaweza kwenda kwenye riba.
Ila pia, riba kuongezeka inatakiwa kuwa na faida kwa wawekezaji. Benki zinatakiwa kupandisha riba kwa watu wanaoweka fixed deposits na savings accounts zenye interest rates, CDs etc. Kwa hivyo kuna fursa hapo pia, ila sijajua itapanda kwa kiasi gani na kama hicho kiasi kitavutia.