Je, soko la hela za kizamani kweli lipo au ni utapeli tu?

Mudugu

Senior Member
Joined
Mar 17, 2018
Posts
141
Reaction score
135
Wana jf wenzangu naomba mnisaidie kwa hili maana nimekaa nikijiuliza sana bila kupata jibu hivi kweli soko la hela za kizamani lipo au ni utapeli tu?

Maana hii habari nimeisikia kitambo sana kuwa hela za kale ambazo zimo kwenye list yakutafutwa ukiipata na ukaipeleka sokoni tayali utakuwa umetajilika na huku kwetu wapo wanaojituma kuzisaka hizo hela lakini bado sijaona hata mmoja amefanikiwa
Je nikweli? Au magumashi tu.

Maana tangiepo niisikie hii habari bado sija shuhudia ambae ametajirika kupitia hizo hela.

Kuna rafiki yangu ananishawishi nijiingize katika utafutaji wa hizo hela.

Lakini akilini hainiingii hata kidogo.

Je, niko sahihi au nakwepa utajiri?
 
Mkuu fanya kazi utafanikiwa hizo zingine ni propaganda tu.

Eti weka buku ushinde milion fumbavu .
 
Mkuu fanya kazi utafanikiwa hizo zingine ni propaganda tu.

Eti weka buku ushinde milion fumbavu .
Hahahaha
Ndio maana mm sitaki kuamini amini kitu ambacho sina uhakika nacho
 
Huo ni uhuni tu.

Ila mimi swali langu ni kwa wale wanaonunua pesa za zamani katika ungo,unakuta wamemwaga nyingiii,wanazipeleka wapi na kwa matumizi gani??
 
tumia kichwa chako kufikiri kwa mfano ukianza kizitafuta kesho asubuhi unahisi unaweza kuzipata lini
Hapo umeongea point mkuu
Maana kuna watu wameanza kuzitafuta wakiwa bado vijana mpaka sasa wamezeeka lakini hakuna lolote familia zao zinashida mtupu
 
Hivi Shilingi kumi na Shilingi 20 bado zinatumika?
 
MKUU NASIKIA ULE NI MZUNGUKO TU WA PESA KAMA MIZUNGUKO MINGINE ILIVYO.
yan ukiipata wewe na wewe unamuuzia mwingine.Mwingine nae anamuuzia mwingine,na huyo mwingine anapelekwa kwa muuzaji mwingine.
 
Usijisumbue hakuna utajiri wa namna hiyo.Biashara yenyewe iko kama ya kishirikina vile,halafu hata mteja wa mwisho hijulikani anapoipeleka bidhaa.Fikiria tu hata yule anayeshawishi hana uwezo wa kununua bidhaa endapo itapatikana.Watu wa namna hii ndio wameshawishi uchunaji wa ngozi za binadamu,ukataji wa viungo vya walemavu wa ngozi nk.Chukua tahadhari mkuu.
 
Biashara hiyo ipo
Lakini soko lake limetawaliwa na Mazingira yenye utata mwingi.
Utapeli, Ushirikina nao pia upo
Watu wengi wamelizwa Kupitia biashara hii.
Ushauri wangu fanya kazi
Watu wengi wametapeliwa kwa sababu yakupenda Mteremko.
Nimefanya Utafiti wa biashara hii kwa miaka 3
Nimegundua mengi yenye kushangaza

Pacha wa biashara hii mwingine ni Maji mekundu yanayopatikana kwenye Miamba
Kwa kua hapa natumia jina lngu siwezi kufunguka zaidi.
 
Mkuu tumia anonymous ili utupe zaid matokeo ya research yako!
 
MKUU NASIKIA ULE NI MZUNGUKO TU WA PESA KAMA MIZUNGUKO MINGINE ILIVYO.
yan ukiipata wewe na wewe unamuuzia mwingine.Mwingine nae anamuuzia mwingine,na huyo mwingine anapelekwa kwa muuzaji mwingine.
Hahahahaha
Kumbe nipe nikupe
 
Asante mkuu
 
Hapo umeongea point mkuu
Maana kuna watu wameanza kuzitafuta wakiwa bado vijana mpaka sasa wamezeeka lakini hakuna lolote familia zao zinashida mtupu
Ule ni utapeli ambao umejikita kwenye uadimu wa hizo hela then aliekupa mchongo uzitafute anaenda kumpanga mtu kuwa anazo then we ukienda kununua kwa promise ya kwenda kuziuza kwa hela nyingi then huyo aliyekupa taarifa kuwa hela za kigeni deal anapotea au anajifanya hajui pa kuzipeleka kwa kisingizio chochote.Utabaki na mihela yako kama mwehu ambayo umeyapata kwa gharama kubwa
 
Mh watu wajanja kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…