Lyetu
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 1,268
- 3,429
Mama wa watoto kadhaa anahukumiwa zaidi ya miaka 20 kwa kukutwa na nyamapori kilomoja, ila kuna kundi la watu linafanya uwindaji haramu kwa kuua mamia ya wanyamapori kwa kisingizio cha tamaduni.
Ufugaji wa ng'ombe wa kienyeji umekuwa kama uharifu nchini kwa asilimia kubwa ya wafugaji, mifugo yao inataifishwa na kupigwa mnada, ila kuna kundi limeachiwa pori lifuge mifugo kwa uhuru na wakitaka kuamishwa wanajengewa na nyumba kwa kisingizio cha tamaduni.
Mimi na wewe tukitembea na siraha kama sime au visu vikiwa hadharani bila kumdhuru yeyote, kuna uwezekano wa kukamatwa na kuchukuliwa hatua, ila kuna kundi linaruhusiwa kutembea na siraha kwa kisingizio cha tamaduni.
Nikwamba haya makundi mawili tamaduni zao ziko juu ya sheria?
Mbona tamaduni za wengine zinapingwa vikali na mamlaka ila za haya makundi mawili zinapewa kipaumbele?
Watanzania tumekubali baadhi ya wanachi wafungwe na wengine wafaidi matunda ya nchi kwa kisingizio cha tamaduni?
Sina uhakika sana ila wapokot walipewa umaalumu kama wanaopewa wale watembea na sime, leo wanamiliki siraha za moto na wamefikia hatua ya kutunishiana misuri na Jeshi.