Je, Tanzania inaenda kutangazwa rasmi Taifa la Kidikteta?

Je, Tanzania inaenda kutangazwa rasmi Taifa la Kidikteta?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Mataifa kadhaa Duniani yamepitia nyakati ambazo Tanzania inapitia kwa sasa, ambapo mifumo yote ya haki za wananchi huangamizwa na watawala.

Kwenye utawala wa kidikteta, hakuna mifumo ya haki ambayo huwa inafanya kazi. Utawala wa kidikteta hupora mifumo yote ya utawala na haki, na kuiweka chini yake.

1. Bunge haliwezi kuwa huru, na hufanya kazi kwa maelekezo ya Serikali

2. Mahakama haiwi huru, na hufanya kazi kwa maelekezo ya Serikali

3. Tume ya uchaguzi biwa haiwi huru, na hufanya kazi kwa maagizo ya watawala.

4. Vyombo vya ulinzi havifanyi kazi ya kulinda usalama wa raia au nchi, bali watawala, na zaidi hufanya kazi ya kuwatisha na kudhulumu haki za wananchi.

5. Vyombo vya habari huwa haviruhusiwi kuandika au kutangaza chochote cha kuwakera watawala

Je, katika haya, katika nchi yetu, ni lipi ambalo hatujalifikia ili tujisifu kuwa nasi tumefanikiwa kuwa Taifa la kidikteta?


NB: Kilele cha utawala katili huwa ni udikteta. Mkishafika kwenye udikteta huwa hakuna utawala mbaya zaidi ya hapo. Kinachofuatia huwa ni ama kubakia kwenye udikteta au kuondoka kabisa kwenye udikteta na kuingia kwenye demokrasia, kama tulivyoshuhudia kwa baadhi ya mataifa mengine:

MALAWI
Malawi iliishi chini ya udikteta wa Kamuzu Banda kwa miaka mingi, leo ina demokrasia thabiti.

CHILE
Chile ilidumu chini ha udikteta wa Augustino Pinochet, leo ni nchi ya kidemokrasia.

NIGERIA
Wanaijeria waliishi chini ya udikteta wa San Abacha kwa mateso makubwa, leo Nigeria ni nchi yenye mfumo bora kabisa wa kidemokrasia kwenye uchaguzi barani Afrika.
 
JPM alisingiziwa mabaya mengi sana
Nae pia alikudikteta hakuna kumsafisha
download.jpeg
 
Back
Top Bottom