SoC04 Je, Tanzania inahakikisha vipi maendeleo yanaenda sambamba na uhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa baadaye?

SoC04 Je, Tanzania inahakikisha vipi maendeleo yanaenda sambamba na uhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa baadaye?

Tanzania Tuitakayo competition threads

donxydag

New Member
Joined
Jun 4, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Je, Tanzania inahakikisha vipi maendeleo yanaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadaye?

Kuhusu swala la Tanzania na maendeleo na uhifadhi mazingira ili liwe halisi inabidi;
(a)kwanza serikali ihamasishe wananchi kutumia gesi kama nishati bora kwa matumizi ya nyumbani nampongeza Raisi kwakuanza na hatua hii, ili elimu hii iwe halisi inabidi serikali iamue kubadili mfumo ambao utatoa msaada wa elimu ya kumsaidia mtanzania kufurahia nishati asilia(gesi) aliyonayo. Na siyo mfumo wakufanya nishati asilia(gesi) kuwa kama biashara badala ya kujikita katika kupambana na namna ya kumsaidia mtanzania aweze kufurahia alichonacho ndiyo kwanza inaweka wawekezaji wengi wakusambaza gesi za kampuni tofauti tofauti na bei kubwa zisizo na kiwango au kiasi maalumu na hao wawekezaji hawawezi kujua hali ya mtanzania wa hali ya chini katika kumudu upatikanaji wa bidhaa za mtanzania mwenyewe hasa gesi na ingewezekana makaa ya mawe yasiuzwe tuu nje bali yasafirishwe kwa lengo la kuchakatwa zaidi kwenye viwanda vyakuzalisha nishati na yakachakatwe katika kiwango cha chini kabisa ndipo nishati yake irejeshwe nchini ili kutumika kama nishati ya kupikia na mengineyo.

(b)Inapaswa kutoka elimu ya vitendo kuhusu umuhimu na faida zinazotokana na kuyafanya mazingira rafiki kwa Tanzania yenye maendeleo kwa kila mtanzania; Hii inawezekana ikiwa tuu rasilimali zinazopatikana nchini zinamuwezeshe kila mtanzania kumudu kiwango cha maisha kwakuwepo na upatikanaji wakutosha wenye bei sawasawa na maisha halisi ya mtanzania wa hali ya chini kabisa, na hii inawezekana ikiwa tunavyanzo vingi vya gesi asilia basi serikali inaweza ikawa na kampuni moja tuu ya uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa nchi nzimaa, aidha taifa gesi kwaajili ya nishati kwa kila mtanzania na vituo vya taifa gesi vipatikane kila mahali kama umeme unavyopatikana; badala yakuwa na ushindani wa makampuni mengi ambayo yanazidi kuleta ushindani wa bei kama biashara badala yakumsaidia mtanzania wa hali ya chini yanamfanya zaidi ashindwe kumudu bei kubwa zilizopo ambazo zinabadilikabadilika.

(c)Jambo la mwisho ni kuhusu oili chafu au dizeli chafu ambayo hupatikana viwandani kwenye vyombo vya moto hii nayo ni nishati nzuri kuliko ukataji ovyo wa miti inaweza ikatumika kupikia kwa jiko lake maalumu na ingependeza kama majiko yake yahamsishwe kutengenezwa na kuuzwa kwa bei nafuu kwa kila mtanzania.
Screenshot_20240624-110209.png
 
Upvote 3
Back
Top Bottom