Je, Tanzania inahitaji BBI kama Kenya?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Na Malisa GJ,

Leo Kenya imezindua ripoti ya BBI, ambayo ni kifupi cha maneno Building Bridge Initiatives, yani jitihada za kujenga daraja la maridhiano ya kitaifa.

Ripoti hiyo imezinduliwa katika ukumbi wa BOMAS jijini Nairobi na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 5000, huku mamilioni wengine wakifuatilia kupitia runinga. Rais Rais Uhuru Kenyatta ndiye aliyeongoza shughuli hiyo, akisindikizwa na viongozi wa ndani na nje ya nchi.

Tanzania imewakilishwa na Waziri Palamaganda Kabudi ambaye ametoa hotuba nzuri na ya kusisimua. Ameongea kwa weledi mkubwa akisistiza mshikamano na maridhiano kitaifa. Amelaani vyama tawala kukumbatia madaraka na kupuuza wenye mawazo mbadala.

Ameshauri kuwepo kwa serikali zinazokaribisha mawazo mbadala, na kushirikisha vyama vya upinzani katika kuunda serikali. Hutaamini kama ni yule mzee mwenye "tashwishwi" anayeongea kwa "kujibagaza" akiwa hapa chini.

Ripoti ya BBI ni kilele cha mchakato ulioanza mwezi Machi mwaka jana (2018). Ripoti imesheheni mambo mengi sana, lakini baadhi ya mapendekezo yaliyopo kwa kifupi ni kama ifuatavyo;

#KISIASA;
1. BBI inapendekeza demokrasia jumuishi (Consociationalism). Yani ukishindwa kwenye uchaguzi hupotezi kila kitu. Kwa mfano CCM iliyopata kura mil.8 haikupaswa kuunda serikali yenyewe na kupuuza vyama vya upinzani vilivyopata zaidi ya kura mil.6. Consociationalism inazuia mmoja kushinda na kubeba madaraka yote, na aliyeshindwa kupoteza kila kitu.

2. Wagombea wa nafasi ya urais watakaoweza kufikisha walau 5% ya kura watapata ubunge moja kwa moja.

3. Mgombea atakayeshindwa urais (aliyeshika nafasi ya pili) atakuwa ndiye Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

4. Kuwepo kwa Tume huru ya uchaguzi ambayo Mwenyekiti wake atakuwa na madaraka ya kitendaji (Executive Powers).

5. Kipengele cha sheria kinacholazimisha Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kuwa Mwanasheria/Jaji kifutwe.

6. Tume ya uchaguzi iwe na wajumbe kutoka vyama vya siasa (vyenye wabunge), asasi za kiraia (NGOs) na sekta ya habari. Wanaamini 'composition' hiyo itakua mwarobaini wa Tume huru ya uchaguzi, na itakuwa ya kudumu.

7. Rais awe mkuu wa nchi na mkuu wa serikali, na achaguliwe kwa absolute majority ya kura zote (50% + 1). Kama hakuna mgombea atakayepata 50% + 1 basi wagombea wawili wa juu watapigiwa kura tena.

8. Kuwe na Waziri Mkuu ambaye atateuliwa na Rais kutoka chama chenye wabunge wengi. Atakuwa mtendaji mkuu wa serikali na kiongozi wa serikali bungeni.

#MAADILI_YA_UTUMISHI;
1. Watumishi wa umma wanaomiliki biashara zao binafsi wamezuiwa kufanya biashara na serikali au taasisi zake.

2. Ikitokea kashfa ya ufisadi, 5% ya fedha zilizokombolewa apewe aliyeibua ufisadi huo. Yani kwa mfano Kafulila alivyoibua ufisadi wa 400Bil za Escrow, angepewa 20Bil.

3. Kiongozi wa umma akiwa na mali zinazozidi thamani ya KSH 50M (kama Bil 1 za kitanzania) aeleze alivyozipata.

#KIUCHUMI;
1. Kiwango cha juu cha deni la taifa (debt ceiling) kiwe 45% ya GDP. Kwa sasa kiwango cha deni la Kenya ni 90% ya GDP yao, kwahiyo wameamua kuifunga mkanda serikali 'isikopekope hovyo'.

2. Mashirika ya umma yawe na mfuko maalumu wa kutoa mafunzo kwa vijana kwenye ubunifu wa biashara na ujasiriamali.

3. Kuondoa "madalali" kwenye sekta ya kilimo ili kuboresha ufanisi wa sekta hiyo, na kumuwezesha mkulima kuwasiliana na mteja moja kwa moja.

4. Kuondoa kodi kwa vijana wanaoanza biashara, mpaka pale biashara zao zitakapoanza kuimarika.

5. Kuongeza mapato yanayokwenda kwenye serikali za mikoa (kaunti) kutoka 15% ya sasa mpaka 35%.

6. Kuhakikisha magavana wanatenga 20% ya fedha za kaunti kwenda kwenye mifuko ya maendeleo ya kata.

Je na Tanzania nasi tunahitaji BBI?

Kwa hisani ya Malisa GJ


Pia soma
 
Aisee nzuri!
Ila Tz haiwezekani japo ingetufaa!
 
Building Bridges Initiative (BBI) yaani Mpango wa Kujenga Madaraja au kuwaunganisha Wakenya ni mpango mzuri ila umejaa namna ya kuwaunganisha wasaka madaraka au wanasiasa wa juu na kugawana vyeo - si kuwaunganisha wananchi wote wa Kenya ngazi ya chini!

Ulianzia juu na handshake ya Raila na Uhuru, natamani ungeshuka chini na kuhamasisha handshakes nyingi miongoni mwa wananchi wa makabila tofauti: handshake ya mkikuyu na mjaluo, mkamba na mkalenjin, mluhya na mpokot, mteso na mturkana, nk.
 
Kenya wanaishi watu, Tanzania wanakaa nyumbu, kila jambo wao ni kufuata na kusifia tu, bado tuna safari ndefu sana miaka zaidi ya 100,na bila kutoana ngeu huko hatufiki ng'o.
Watawala wanaona kama wanaongoza mazombie hawana hofu yoyote.
 
Wacha waendelee na makabrasha yao muda Ni mchache na mambo Ni mengi.

Ifikie wakati waafrika tuanze kuzitizama nchi zetu kama urithi adhimu na tuache kuzifanya mashamba ya kuacha legacy.

Jitihada binafsi nilizofanya zinaonyesha asilimia kubwa ya wanasiasa huhitaji madaraka si kwa ajili ya kuleta athari chanya katika nchi zao bali kusimika personal legacy ( nimewahi kuwa kiongozi kadha wa kadha lakini wanayoyalalamikia wananchi hawana kumbukumbu ni yapi wamefanya ya kujivunia kwa nchi na raia wake)

Namuunga Mkono Dr. Mhe Rais John Joseph Pombe Magufuli, si kwakua yuko sahihi kwenye kila Jambo bali kujitofautisha na viongozi wengine Barani Afrika kwa kuonyesha kwamba muda wa vikao vya maamuzi, semina, mchakato unaendelea, tumetangaza tenda sijui makorokoro gani kagundua kwamba ndio kifungo kikuu cha maendeleo pamoja na Uzembe na Uvivu wa watumishi wa umma na hulka za watanzania za kulia lia kila uchao.
 
Building Bridges Initiative (BBI) yaani Mpango wa Kujenga Madaraja au kuwaunganisha Wakenya ni mpango mzuri sana, ila umejaa namna ya kuwaunganisha wasaka madaraka au wanasiasa wa juu na kugawana vyeo - si kuwaunganisha wananchi wote wa Kenya ngazi ya chini!

Ulianzia juu na handshake ya Raila na Uhuru, si mbaya kwa kuanzia. Ila natamani sana ungeshuka chini na kuhamasisha handshakes nyingi miongoni mwa wananchi wa makabila tofauti: handshake ya mkikuyu na mjaluo, mkamba na mkalenjin, mluhya na mpokot, mteso na mturkana, nk.
 
Gwappo Mwakatobe, mkuu nilitaka kuanzisha topic kama hii,
lakini nashukuru umeianzisha na kwa ufupi inaeleweka.

kuna watu humu tayari wameanza kuisifu bila hata kuijua imebeba maudhui gani,na leo na miezi kadhaa itakuwa nado huko huko juu kwa wasaka nafasi.
tatizo ni pale itakapitakiwa kupigiwa kura au kutokupigiwa bali ipitishwe na bunge kama muswada,
washamgiliaji wa leo ndio watajua huko mashinani wanasemaje ?
 
Kwetu ilishafanyika. Magufuli aliteua wapinzani na kuwapa nafasi.
Lakini tumeuana hao hao wapinzani wakiwasema wenzao waliopata teuzi na kusema wana njaa au wamenunuliwa.
Ha ha ha nchi ngumu hii
 
Reactions: Oii
Nimesoma hii comment nikarudi kuangalia ID nikajikuta najutia muda wangu niliotumia kusoma huu utumbo Cherenganya,
 
Mpango umekaa kimkakati kuwezesha namna bora ya kugawana vyeo miongoni mwa wanasiasa na sio kuwasaidia walala hoi kujikwamua na umasikini
 
Kenya wanaishi watu, Tanzania wanakaa nyumbu, kila jambo wao ni kufuata na kusifia tu, bado tuna safari ndefu sana miaka zaidi ya 100,na bila kutoana ngeu huko hatufiki ng'o.
Watawala wanaona kama wanaongoza mazombie hawana hofu yoyote.
Ukiambiwa uandamane unajifungia ndan na kitecno chako

Afu unasema tutoane ngeu

Shwain
 
Kwa Tanzania sijui kama kuna mwenye uwezo wa kuishawishi CCM ,kama CCM ilikubali Mfumo wa Vyama vingi lakini leo inahangaika kutaka kuviua itakubaki BBI?
 
Gwappo Mwakatobe,
Unatamani "ungeshuka chini" kivipi. Si huo sasa unakwenda kujadiliwa na wananchi, na wapo huru kutoa maoni na mapendekezo yao, au hukujua hilo?

Tatizo kubwa walilonalo Kenya ni ukabila. Wamejitahidi weee kutengeneza Katiba nzuri na kudhani itasaidia, lakini wapi. Hata hii BBI ni juhudi nzuri, lakini ukabila umewakwama kweli kweli. Kuuondoa usiharibu mambo yao ni kazi ngumu sana.

Kama wanataka, wajaribu kuweka viongozi wa ngazi za juu wanaotoka kwenye makabila madogo madogo kwa miaka kadhaa. Hawa wakiweza kuondoa athari zinazotokana na makabila makubwa kila mara kuweka viongozi wao, inaweza kusaidia kufifisha tatizo lao hili.
Kazi sasa ni namna ya kuwezesha hayo makabila madogo yatoe viongozi watakaounganisha taifa lao.
 
Haya yapo Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…