Je, Tanzania inahitaji BBI kama Kenya?

Ni kweli unachosema, lakini ni kweli pia kwamba huo ni mchakato mrefu. kuna machungu ya kihistoria ambayo hayawezi kabisa kufutwa mara moja tu. zinahitajika jitihada za wakenya wote kuunga mkono jitihada hizo.

Handshake kuanzia juu ina uzuri wa AUTHORITY, ikifika chini ina uzuri wa SUSTAINABILITY na PRACTICABILITY. ikianzia chini kama hakuna kibali juu, itaishia hivyo hivyo, na inaweza kuhujumiwa kutoka juu. Ikishika mizizi chini, itadumu hata wale walioianzisha wakiondoka madarakani au kufariki.

Kule Zanzibar serikali ya umoja wa kitaifa ilitokana na HANDSHAKE ya Maalim Seif na Karume. baada ya hapo watu ambao walikuwa wamejengewa misingi ya kutozikana, sasa walianza kusahau tofauti zao. unakumbuka nani amehujumu? siyo wananchi. ni wale watu wa juu
 
Oginga Odinga alishafariki siku nyingi! Aliyepo anaitwa Raila Amolo Odinga
Ahsante kwa sahihisho hilo; naelewa hivyo, ni swala la kukosea tu.

Lakini turudi kwenye "Handshake iliyozaa BBI", ni kipi wewe unachoona hakifai.
Haiwezekani kuwa sababu tu ya kwamba ilianzishwa na viongozi wa juu, ndiyo iwe sababu ya kuifanya haifai, hata kama wananchi wanapewa fursa ya kuijadili na kutoa mapendekezo wanayoona wao yanafaa.

Kama ni swala tu la vyeo vilivyopendekezwa, ya kwamba viongozi wanasukumwa na kujitengea nafasi zao katika uongozi wa nchi, je, wananchi wakati wanajadili na kupendekeza wakiyakataa hayo haitawezekana kuleta muundo tofauti wanaoutaka wao?

Niambie wewe kama kuna hicho kizuizi kwa wananchi kufanya hivyo.

Naomba tafadhari umsome mkuu 'Mindi' #41.
 
Wakenya wametuzidi kwenye Kila kitu kasoro Ukabila tu....
Wana nia ya kweli na Maendeleo ya Nchi yao!
 
I concur mkuu huu ni ulaji tu unatengenezwa tukumbuke kulisha kuwa na BBI Zanzibar (maridhiano) yaliyozaa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iliishià wapi.
Yaliyopo ndani ya BBI yanategemea zaidi ridhaa ya Uhuru na Raila kuliko wananchi wakenya ni kwasababu hiyo wanataka report ipitie bungeni tu na kusiwe na referendum (means isiingie kwenye katiba)

Tujiulize tu Ruto akiukwaa urais hii report itatekelezeka!!?? kwa maoni yangu bbi lengo kuu ni kumpeleka Raila ikulu (Ruto akishinda hakuna BBI) will Raila accept defeat and agree to become Official leader of the opposition in the Parliament!!???

Kabudi niwakuwashauri wakenya kuhusu BBI wakati ccm imekataa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kweli!?? tuwe serious basi, kweli kabudi ni wakupongeza handshake wakati Kuna wabunge waliitwa kwenye party cocus kwa kwenda Nairobi kumuona lissu

Devolution ndo kitu pekee watanzania tunahitaji kujifunza from Kenya "madaraka mashinani" which magu n even Nyerere hawataki kukisikia
 
Kenya wanaishi watu, Tanzania wanakaa nyumbu, kila jambo wao ni kufuata na kusifia tu, bado tuna safari ndefu sana miaka zaidi ya 100,na bila kutoana ngeu huko hatufiki ng'o.
Watawala wanaona kama wanaongoza mazombie hawana hofu yoyote.
Kenya Kuna nyumbu nyingi tu
 
Building Bridges Initiative (BBI) yaani Mpango wa Kujenga Madaraja au kuwaunganisha Wakenya ni mpango mzuri sana, ila umejaa namna ya kuwaunganisha wasaka madaraka au wanasiasa wa juu na kugawana vyeo - si kuwaunganisha wananchi wote wa Kenya ngazi ya chini!

Ulianzia juu na handshake ya Raila na Uhuru, si mbaya kwa kuanzia. Ila natamani sana ungeshuka chini na kuhamasisha handshakes nyingi miongoni mwa wananchi wa makabila tofauti: handshake ya mkikuyu na mjaluo, mkamba na mkalenjin, mluhya na mpokot, mteso na mturkana, nk.
 
natamani "ungeshuka chini" kivipi. Si huo sasa unakwenda kujadiliwa na wananchi, na wapo huru kutoa maoni na mapendekezo yao, au hukujua hilo?

Tatizo kubwa walilonalo Kenya ni ukabila. Wamejitahidi weee kutengeneza Katiba nzuri na kudhani itasaidia, lakini wapi. Hata hii BBI ni juhudi nzuri, lakini ukabila umewakwama kweli kweli. Kuuondoa usiharibu mambo yao ni kazi ngumu sana.

Kama wanataka, wajaribu kuweka viongozi wa ngazi za juu wanaotoka kwenye makabila madogo madogo kwa miaka kadhaa. Hawa wakiweza kuondoa athari zinazotokana na makabila makubwa kila mara kuweka viongozi wao, inaweza kusaidia kufifisha tatizo lao hili.
Kazi sasa ni namna ya kuwezesha hayo makabila madogo yatoe viongozi watakaounganisha taifa lao.

SIGNATURE
 
Ahsante sana kwa kuuona ukweli huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…