Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Ni kweli unachosema, lakini ni kweli pia kwamba huo ni mchakato mrefu. kuna machungu ya kihistoria ambayo hayawezi kabisa kufutwa mara moja tu. zinahitajika jitihada za wakenya wote kuunga mkono jitihada hizo.Building Bridges Initiative (BBI) yaani Mpango wa Kujenga Madaraja au kuwaunganisha Wakenya ni mpango mzuri ila umejaa namna ya kuwaunganisha wasaka madaraka au wanasiasa wa juu na kugawana vyeo - si kuwaunganisha wananchi wote wa Kenya ngazi ya chini!
Ulianzia juu na handshake ya Raila na Uhuru, natamani ungeshuka chini na kuhamasisha handshakes nyingi miongoni mwa wananchi wa makabila tofauti: handshake ya mkikuyu na mjaluo, mkamba na mkalenjin, mluhya na mpokot, mteso na mturkana, nk.
Handshake kuanzia juu ina uzuri wa AUTHORITY, ikifika chini ina uzuri wa SUSTAINABILITY na PRACTICABILITY. ikianzia chini kama hakuna kibali juu, itaishia hivyo hivyo, na inaweza kuhujumiwa kutoka juu. Ikishika mizizi chini, itadumu hata wale walioianzisha wakiondoka madarakani au kufariki.
Kule Zanzibar serikali ya umoja wa kitaifa ilitokana na HANDSHAKE ya Maalim Seif na Karume. baada ya hapo watu ambao walikuwa wamejengewa misingi ya kutozikana, sasa walianza kusahau tofauti zao. unakumbuka nani amehujumu? siyo wananchi. ni wale watu wa juu