Je, Tanzania kukumbwa na rungu la FIFA?

Je, Tanzania kukumbwa na rungu la FIFA?

Mtemi02

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2020
Posts
319
Reaction score
221
Shirikisho la soka la Dunia (FIFA) katika kanuni zake hukataza Serikali kuingilia masuala ya soka.

Kwa maelezo ya TFF ni kuwa maelekezo ya kusogeza mbele mechi ya Simba na Yanga yametoka Serikalini kwa maana nyingine serikali imeingilia masuala ya soka directly. Na walichofanya TFF ni kama vile kuichongea serikali huko FIFA.

Endapo hili likitokea na ikiwezekana kabla halijatokea Waziri husika anatakiwa kujiuzulu mara moja ili kuwajibika.

Aidha uongozi wa TFF nao wanatakiwa kuwajibika sababu wao ndiyo wazimamizi wa sheria na kanuni za soka, ilikuwaje wapeleke mechi masaa mawili mbele kinyume na kanuni zao zinazosema masaa 24?

Kadhalika uongozi wa Simba SC unatakiwa kuwaomba radhi mashabiki wao maana kukubali kucheza saa moja bila hata kutoa tamko la kukemea inaonesha aidha hawajui kanuni au wanaunga mkono upuuzi wa TFF

View attachment 1777743
IMG-20210508-WA0025.jpg
 
TFF Imeishimu mamlaka Yanga hakuheshimu mamlaka.Ila imefuata kanuni .wote wapo sawa lkn naona mmoja kwa kuwa ni mdogo azabu inamuhusu.
 
Back
Top Bottom