Je Tanzania kuna legend wa soka?

kidole007

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2012
Posts
3,094
Reaction score
1,876
Ni mchezaji gani TZ ambae tunaweza kumpa hadhi ya u legend yaani gwiji

Unaweza mtaja hata kama amefariki
Ukimtaja unataja na mambo aliyolifanyia soka letu

Nawasilisha
 
Jela Mtagwa, Malota Soma aka Boll juggler.
 
Agustino Peter Magari "Peter Tino" ambaye mwaka 1980 alitupeleka Lagos kwa bao lake la ugenini kwa kuifunga Zambia. Kumbuka ni mara ya kwanza na mwisho mpaka leo Tz hajawahi kufuzu Afcon na Tino bado yuko hai na hakuna Tino mwingine aliyezaliwa kutufikisha hapo.
 
At least wewe umeongea point..!
 
Tanzania Ma-legendar wako kwa ngazi tofauti.
Ngazi ya kwanza ni-
Omary bin Jabir
Maulid Dilunga
Hawa kwa pamoja kwa umahiri wao wa kucheza soka waliweza kuchaguliwa Kwenye timu ya Afrika

Kundi jingine ni la kina
Sunday Manara
Kassim Manara
Hawa ni wachezaji wa mwanzo wa Tanzania kwenda kucheza soka Ulaya.

Kundi jingine hili linamuhusisha;
Kitwana Manara
Huyu alilitawala soka la Afrka Mashariki kwa muda mrefu.

Mwingine ni
Mohammed Chuma
Huyu naye alijijengea umaarufu mkubwa kwa kuchezea timu ya taifa kwa muda mrefu na kuagwa kwa heshima.

Kundi la mwisho hili linawahusisha wachezaji wafuatao;
1- Juma pondamali
2-Daud salum Bruce Lee
3-Hassan zitto/Mohammed kajole
4-Salim Amir/leodgar Tenga/Mukebezi
5-Jellah Mtagwa
6- Mohammed Adolf /Juma mkambi
7- ,Omar Hussein
8- Hussein Ngulungu
9- Peter Tino
10- Mohammed Salim
11- Thuwen Alii /Charles Alberto
Na wengineo niliowasahau hawa ndo waliofanikisha Tanzania kucheza fainali za Afrika 1980 kule Lagos.
 
Tupo mtu mwingine Anaitwa abdalah kibadeni. King. Usisahau kuwa huyo ndie alichaguliwa kuwa mchezaji WA karne mwaka 2000..maana ktk uchezaji kufanya mengi na hata ktk ukocha hakuna kocha aliemfikia rekodi zake.
 
Tupo mtu mwingine Anaitwa abdalah kibadeni. King. Usisahau kuwa huyo ndie alichaguliwa kuwa mchezaji WA karne mwaka 2000..maana ktk uchezaji kufanya mengi na hata ktk ukocha hakuna kocha aliemfikia rekodi zake.
kibadeni alikua anarukaruka tu huwezi mlinganisha na manara computer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…