Je tanzania kuna usawa?

Je tanzania kuna usawa?

Nyanya mbichi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Posts
3,716
Reaction score
2,218
Katiba ya Tanzania - Ibara ya 13.

Ibara ndogo ya (1),
Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa kwa mujibu wa sheria ya Nchi.


(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika; \n(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo.
 
Kwa mujibu wa .....akiwa bado ana
fahamu alimsikia daktari aliyekuwa
akimhudumia akiomba msaada wa
gari la kubeba wagonjwa ili
limchukue na wito
ambao ulijibiwa kwa maelezo
kwamba lilikuwa halina mafuta.
Majibu hayo kwa mujibu wa......
yalisababisha daktari huyo aombe
kuletewa gari la wagonjwa la
((wagonjwa maarufu (VIP) )) ambalo
lililitwa na muda mfupi baadaye
akapakizwa tayari kwa safari ya
kukimbizwa ......

LENGO LANGU NIKUTAKA KUJUA KAMA KWELI USAWA UKO KWA WATU WOTE TANZANIA ,HAKUNA ALIE BORA KULIKO MWINGINE AU JUU YA SHERIA KULIKO MTU MWINGINE?

KWA NINI KUNA VIP?

TAFADHALI NAOMBA MAJIBU
 
Back
Top Bottom