Je, Tanzania ni nchi ya hatari kama Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore ilivyoeleza?

Daah jamaa wametusagia kunguni mpaka inatia hasira.

Ila hii nchi haifahamiki sijui kwanini, huko duniani hatujulikani aisee.

Wenzetu Kenya na UG wanatajwatajwa sana huko.
 
Hatari ni kitu relative. Inawezekana kuna vitu wenyewe Watanzania wamezoea lakini ni hatari.

Singapore wana standard tofauti sana, huko hata kutupa karatasi barabarani tu ni bonge la kesi.

Sasa ukitaka kuuliza kama Tanzania ni hatari au si hatari, inabidi ujue standard gani unatumia.
 
Daah jamaa wametusagia kunguni mpaka inatia hasira.

Ila hii nchi haifahamiki sijui kwanini, huko duniani hatujulikani aisee.

Wenzetu Kenya na UG wanatajwatajwa sana huko.
nimeona hoja kuu wanazotumia ni terrorism, ambayo ni kweli kwa hali yetu ya siasa pamoja na uporaji wa ovyo ovyo ambao upo

na hili suala la Ben Saanane litaongeza kuni kwenye huo moto wa terrorism
 
Wametuonea sana
 
Hapa hapa Tanzania kuna Watu wanaishi Lakini hawajui msumbiji kuna machafuko
 
Wametuonea sana
Ila kwa kiasi fulani wapo sahihi kwakuwa mambo kama petty theft na uporaji yapo sana bongo. Na ukizingatia uchaguzi unakaribia kwahiyo masuala ya ugaidi na utekaji yataongezeka.
 
Nchi yetu inatabia ya kusema Uongozi Kwa mambo yaliyo wazi. Kwa kifupi tu funzu Kwa kubadili ukweli. Sasa wenzetu wakitendewa hu report kwao na kuweka kwenye record. Na labda ukifika idadi kadhaa wanajua hii si bahati mbaya.

Wanausalama wetu kama mnavyowajua ukipigwa tukio wewe ndio unageuka mtaji. Sitasahahu kisa keep Moja tuko bushi Mzee akaletewa barua ya vitisho vya kuuliwa. Kuipeleka polisi yeye ndio aliwekwa ndani kutoka ilibidi busara itumike kama mnavyojia.
 
Marekani wao wanatumia standard ipi? Maana nao wamesema huku kuna hatari
 
Hili silo jambo la kulifurahia hata kidogo. Nadhani serikali na vyombo vyake vya dola wanatakiwa kuchukua hatua stahiki.
 
Vitu vingine mnavipuuza viki-backfire mnatafuta mchawi. Si tumejuzwa humu kwamba kuna mhubiri wa kimataifa anatafutwa duniani huko kwa terrorism yet amekaribishwa nchini kuendesha midahalo?

Duniani huko wako makini and they share intel a lot.
Nashangaa wanashtuka 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…