Je, Tanzania tuna mtaala wa elimu

Je, Tanzania tuna mtaala wa elimu

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,544
Katika elimu neno mtaala (Curriculum) linamaanisha utaratibu, mpangilio, muundo na maudhui ambayo mwanafunzi hupaswa kufuata na kukamilisha kama sehemu ya matakwa ya kupata tuzo fulani ya kielimu na kitaaluma. Neno mtaala vile vile linamaanisha matarajio, malengo na maudhui ambayo mwanafunzi anatarajia kuyakamilisha kabla ya kutunukiwa tuzo ya kitaaluma katika ngazi fulani.

Kuna aina mbalimbali ya mitaala. Kuna mitaala ambayo imeandikwa na ambayo haijaandikwa. Kuna mitaala inayoonekana na isiyoonekana. Kimsingi mtaala ni mambo yote ambayo mwanafunzi hupitia katika kujifunza tangu anapojiunga na mfumo rasmi wa elimu hadi anapohitimu katika ngazi fulani ya elimu ikiwamo malengo ya elimu, maudhui, njia na nyenzo za kujifunzia na njia za tathmini.

Sasa kutokuwa na nyaraka moja iliyoandikwa na ikaitwa "Mtaala" haimaniishi nchi yetu haina mtaala. Ni sawa na kusema Uingereza haina katiba kwa sababu tu Katiba yake haijaandikwa katika waraka mmoja unaoitwa katiba. Matatizo ya elimu Tanzania hayatokani na kutokuwa na Mtaala au kuwa na mitaala dhaifu, bali udhaifu wa utekelezaji wa mitaala, ikiwemo mazingira magumu na dhaifu ya kufundishia na kujifunzia.

(Dr. Kaitila Mkumbo, Raia Mwema....Feb 6-12,02,2013)
 
Back
Top Bottom