Je! Tanzania tunahitaji wasomi wengi au Hustler wengi?

Je! Tanzania tunahitaji wasomi wengi au Hustler wengi?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tatizo la Afrika kwa mawazo yangu sio kutokuwa na wasomi wa kutosha bali tuna matatizo makubwa matatu

1. Kutokuwa ma maarifa
2. Utamaduni wa kupuuza -Sheria, wezi, rushwa....
3. Ubinafsi- Mfano Rushwa

Wasomi wetu wengi ambao ndiyo viongozi wamekuwa wabinafsi kiasi kwamba wanaweka upendeleo kwa kuajiri mfano ndugu au kikabila, kula pesa za rushwa badala ya kuwekeza kwa wananchi na utamaduni wa kutokufuata sheria ambao ndiyo unaleta rushwa.

Hustler: Ni wale watu ambao ni wahangaikaji, wabunifu na wamependa maendeleo. Hawa ni wale watu ambao leo ukiwapeleka sehemu yeyote Dunia wataangalia jinsi ya kujikwamua na kufanikiwa na sio kulalalama au kujigamba. Mfano mzuri wa Hustler ni Lema. Lema ameondoka Tanzania kwa miaka miwili bila kutegemea na kwenda Canada. Kwa muda wa miaka miwili tu ameshatafuta wawekezaji na kuingia ubia nao, amejifunza kufanya biashara tofauti. lakini Tanzania tuna Hustler wengi ambao tunatakiwa kujifunza kwao badala ya kusoma tu halafu tunasubiri kazi.
 
We need more Hustlers.

Jitathmini wewe mwenyewe, halafu angalia ni vitu gani ambavyo unapenda na unaweza kuvifamya kwa moyo mmoja.

Ingia mtandaoni angalia na fuatilia kwa ukaribu watu wanaofanya hicho unachokifanya ujifunze kupitia wao na usitake kukopi. Jifunze tu, halafu sasa...

Ukimaliza hapo, nenda kwenye zile account zako za mtandaoni (Twitter, Facebook, Instagram hata hapa JF pia) anza kuandika na kupost.

Fanya katika hali ya kawaida na usijilazimishe.

Wakati unafanya hivyo njoo nikufundishe mbinu mbalimbali za kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine mtandaoni. Sitahitaji pesa mingi sana ni kati ya 10k hadi 45k kutegemeana na utakayohitaji kujifunza kufanikisha jambo lako.

Halafu nikishakufundisha, endelea kuweka post mtandaoni.

Fanya hivyo kwa miezi Sita usitegemee faida yoyote.

Halafu miezi Sita inayofuata, hakikisha mtu akikutafuta kutaka kujua lolote kwako HAKIKISHA ANAKULIPA.


Baada ya hapo, Fungia vyeti vyako kabatini maana hautavihitaji tena ili kupata pesa.

Kama wewe ni mvivu hata usinitafute kukufundisha hayo yote. Endelea kukumbatia vyeti.

Kama una moyo mgumu (Hustler). Karibu PM tuyajenge.
 
Endelea kuhaso bila elimu au kusomesha wanao kama hamuwi vibarua wa milele.

Ubinafsi ni kawaida tu, hata mitume wa yesu walikuwa ndugu.
 
1. Tunahitaji mifumo rafiki na wezeshi kwa kila rika na viwango tofauti vya elimu na katika kila kada.
2. Tunahitaji sheria kali na zisizo onea watu wa maisha ya chini.
3. Tunahitaji inequalities/haki na hii itazaa uzalendo.
 
America is built by Hustlers not Phds...

The JP Morgans, Rockerfellers, etc..

Elimu kidogo kaz na risk and mindset ya independence.

Africa politicians and Pastors kila mtu ni Drs, doing literally nothing to their community.
 
Tz wasomi wengi hustler wachache by the way tunahitaji wasomi wanaohaso at the same time
 
Inategemea na sera ya nchi

Kama ni service based, itahitaji wasomi wengi

Kama ni industrial based itahitaji technicians wakutosha

Kama kilimo itahitaji wasomi, technicians etc
 
Endelea kuhaso bila elimu au kusomesha wanao kama hamuwi vibarua wa milele.

Ubinafsi ni kawaida tu, hata mitume wa yesu walikuwa ndugu.

Lema na Msukuma wamesoma wapi?
 
Inategemea na sera ya nchi

Kama ni service based, itahitaji wasomi wengi

Kama ni industrial based itahitaji technicians wakutosha

Kama kilimo itahitaji wasomi, technicians etc

Wasomi ni muhimu lakini Hustlers nao ni muhimu. Tatizo leo hatuoni kama Hustlers ni muhimu lakini kwa mawazo yangu ni muhimu kuliko wasomi ambao wapo na hatuhitaji wengi. Unaweza ukawa msomi lakini usiwe na maarifa
 
Hustler ni wale watu ambao ni wahangaikaji, wabunifu na wamependa maendeleo. Hawa ni wale watu ambao leo ukiwapeleka sehemu yeyote Dunia wataangalia jinsi ya kujikwamua na kufanikiwa
Ktk mazingira yenye hayo matatizo 3 uliyobainisha ni ngumu sana mhangaikaji kutoboa.

Unapoanza kuinuka tu atakuja mla rushwa atakuyumbisha mpk utafunga mradi wako.

Ogopa Sana kuishi kwenye nchi yenye mifumo mibovu ya kisheria na maadili
 
Back
Top Bottom