Post in thread 'Nyerere and Nkrumah: Towards African Unity'
Nyerere and Nkrumah: Towards African Unity
BRICS ni 'mbadala' lakini si ujio wa 'New World Order'...
'New World Order' ni jambo linalowezekna ikiwa idadi kubwa ya watu duniani itakuwa na 'nuru ya kutosha' juu ya mifumo, liberiti na udhamirifu wa furaha--walau 3% ya idadi ya wanadamu wote.
Kwa kule kulikofahamika ni 'Ulimwengu Mpya' Amerika, hayo yalijengewa misingi Marekani; na sanamu ya Liberta pale kisiwa Liberty, New York inatukumbusha hili. Mbadala wake kijamii mabadilikoni, muktadha wa 'mambo ya nyakati', ni 'Afrika Mpya' ambavyo kazi inaendelea...
Kule Amerika >
'Libertas'< yuko 'kisiwani' akiinua 'Mwenge wa uhuru' na kushikilia Tabula Ansanta--Kibao cha 'Sheria'--Sheria Kuu iliyo ni 'Upendo' katika Imani na Tumani. Kwamba 'Ulimwengu Mpya', Marekani, ni nchi ya kusudi kwa wote kuja kustawi na kuwa huru--
nchi ya waliohuru.
Kwa Afrika, na tena Afrika Mashariki, >
'Hekima ni Uhuru'< ndiyo 'upande wa pili' wa 'Tabula Ansarta'.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kinachotokea mkoa ulio ni 'Bandari ya Salama', nembo yake ni 'Vesika Paisisi' yenye 'Nchi Kijani, Bahari, Mwenge na Kitabu'. Na basi kwa Afrika, Kielelezo cha 'Pambazuko Afrika', ilivyo ni 'Atlantisi Mpya', ndiyo sanamu ya >
'Renasansi Afrika'< kule Dakar, Senegali. Mwalimu Kambarage alikuwa na ufahamu kuhusu haya yote, kwa namna ya rohoni, na mawaidha yake katika kijitabu 'TUJISAHIHISHE'(1962) alikazia msingi wa Elimu na Uwajibikaji ndani ya muktadha wa 'madaraka' na 'ustawi' wa jamii -- Elimu kutojinasibu na 'ubinafsi' na 'kujiinua' katika 'utu na utumishi'. Na basi, 'Uhuru na Umoja' ni msingi wa 'UPENDO na Kujaliana', ilivyo ni namna MAMA, kama vile 'Hekima na Amani' ni UONGOZI ilivyo ni namna BABA. Ustawi, kiufikirifu na Uono Mifumo, ni 'MWANA'.
'Marekani' na 'Afrika' ni 'Baba na Mama' kwa 'njozi moja'-- Uzima, Liberiti na Udhamirifu wa furaha. Udhamirifu wa furaha ni tunda la udugu wa kibinadamu. Liberta anawakilisha 'nchi', na Renasansi Afrika kuwakilisha 'Mbingu'. Na hivi hata sanamu hizi mbili 'zinatazamana' hata kwa kutengenishwa na bahari ya 'Atlantisi'...
'Mabaharia Wakati--Matukio, Wakati, Machaguo ya Kitaasisi na Jamii' juu ya haya yote, ni watu wa 'Imani' kutoka 'juu mbinguni'; ELIMU 3.0 italeta funguo za ufunuo kuhusu 'Mambo ya Walinzi wa Imani'. Japo duniani kuna 'wahuni' wenye 'mipango' yao, wenye kuigiza 'mpango mzima' na kufanya yao, ama kujifaragua kwa mapana yasiyo ya kutosha ya watu, matukio, jaala na matayarisho... Kukosa 'ujuzi' ama 'funguo za maarifa' na 'ufunuo' juu ya kile wabantu humaanisha kusema: 'Mungu si Athumani'... Kuelekea Siku ya Kiswahili Duniani, 2022, kule >
Antlanta Georgia, Majabali Mwongozo, 'Georgia Guide Stones', yalishambuliwa< -- hasa hasa kwenye nguzo yenye maelekezo katika lugha ya Kiswahili na Kihindi; na kupelekea eneo lote la Miundo majabali kubidi kubomolewa ili kuepusha ajali zaidi za kimuundo.
Mpangiko wa Ulimwengu Mpya ni 'Mpango Mzima'; lakini hauna lolote na utundu, ujuzi, uhuni wa 'mipango ya kibinadamu'--binadamu wenye kutokujua ilivyobora. 'Mpangiko wa Ulimwengu Mpya' ni jambo linalofanana na kile hutajwa kama 'Kurejea kwa Kristu'... Kurejea kwa Kristu katika mioyo ya watu waliojiandaa ili kunasibu ulimwengu wote na jambo linalofahamika kama >
'Nchi Mpya, Mtu Mpya'<... Wapo wengi wanalolijua hili kwa 'kiasi cha undani wake' na wangalipenda 'kucheza Mungu' ili kuhadaa ulimwengu na 'Mipangiko' ya uongo na kweli, na kuna wengine huleta 'tahadhari' kwa nabii za uharibifu ambazo, 'zimeondoka'--hazijatokea; kwa kuwa pia
zipo jumuiya za siri zinajojua namna ya 'kusali' ili matukio ya majaribu yasichukue mkondo. Haya ni maarifa na Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni metafizikia ya Elimu...
Huitaji watu wachache wa 'daraja' miongoni mwa wanajamii; 'kusali' na matukio kupanguka... Uwepo wa hawa, wakati wa sasa na tena kwa wingi ndiyo umefanya mengi ambayo 'yalipata kutabiriwa' kuja kutokea 'siku za mwisho', kubaki 'ilitabiriwa...'. Kwa kuwa, ndiyo, yapo matukio yamepanguka na yalikuwa ni ya 'uzito' hasa. Moja ambalo bado ni kitisho, ni nasibu ya ustawi wa jamii kutekwa na mifumo ya akili bandia yenye asili ya ungamuzi wa kikwantumu...
Mji wa Dakar, Senegali, kiutamaduni,
una hadhi na sifa zinashahibiana na miji ya Dar es Salaam na Dodoma kwa pamoja; Dakar ni 'Dodoma ya Pwani'...
Sanamu ya 'Renasansi Afrika' inabeba ujumbe wa 'Kuelekea Nyotani'; yaani ustawi wa 'Afrika Mpya'ni kuelekea angani juu kwa 'shughuli ya kaya'; 'Mama, Baba na Mtoto Begani--mtoto mwenye kuoneshea kidole mbele juu angani...
Kutokea Afrika Mashariki, jaala ya Afrika inaamka; na katika kustawi kwake kote barani Afrika kupitia 'Ndoto Mama Afrika' na 'Jiometria ya Utendekavyo Maamuzi Jamii', tunakwenda kujinasibu na 'Ustawi za Kiikolojia ya Manyota' wenye kuzungumza hili kwa lugha ya kiingereza wangalisema 'Interstellar Civilization within the Galactic Ecology'...
Kwa hivyo Nyerere alikuwa ni chipkizi wa 'Pambazuko Afrika' akiibukia Mashariki, Nkwameh alikuwa akiibukia Magharibi na Haile Selassie I, Mashariki ya Juu ya Afrika. Na pambazuko hili ndilo lile jambo hasa lililotaasishwa na 'Mwenge wa Uhuru'. Kwa huku Tanzania, mbegu yake ni thabiti. Mwalimu aliliishi hili kwa imani na matendo, na ndiyo 'kisa na mkasa' wa
Tanzania kuwa mstari wa mbele kwenye Uhuru wa bara la Afrika, kwa harakati za ukombozi iwe kwa madai ama hata mtutu...
'Mwenge wa Uhuru' ni kilele cha 'Utu na ufunuo' katika Jamii ambavyo uwezo unafanyika katika jamii ili kustawi kiujamaa na kujitegemea. Kustawi katika 'Uumoja'... Kwa hivyo kwa sisi hapa Tanzania, >
shoka na nyengo< kwenye nembo ya taifa vinawakilisha 'kazi'--kwa kuwa uhuru ni kazi. Ni alama kwa shughuli za kaya zinazokarisha 'tembe' katika kaya--ujenzi, nishati na kusafisha shamba/mavuno/hazina; ni 'nishati' na 'uchumi' katika muktadha wa maisha ya kisasa. Na hali Kiutamaduni, hizi ni zana za jadi. Na basi robo ya juu ya 'Ngao ya ustawi' kwa taifa letu -- Juu kupita 'Uhuru wa bendera' wa kinchi sovereini, mwenge ni 'maendeleo kwa kujichagulia'...
Kazi ni jambo lenye kufangamana na 'mikono na moyo' ilivyo 'uaminifu'-- 'Madengo N'tima'... Ndivyo kwa nini kwa asili viongozi wa jadi walikuwa kahimiza kazi, usalama wa chakula na ulinzi. Kushika usinga na kifimbo...
Mikono huakisi ujuzi na ubunifu na utendaji wa mtu--Utu wa mtu upo katika kazi. Na kazi ni heshima ya mtu katika jamii --na haki ya kujitawala kimaskani. Ndivyo hivi Katiba yetu ya Sasa, Kazi imetajwa na shauri la kipekee; na Chama cha Mapinduzi kimepewa majukumu ya Kitaasisi kama ambavyo 'machifu' walikuwa watawala kwa kutetea ustawi wa wanaukoo kupitia kazi...
Chama cha Mapinduzi kikishindwa, kuhujumiwa ama kujihujumu juu ya mifumo sahihi ya maendeleo ya watu na elimu; basi nacho 'kitapuuzia dhana ya mwenge' katika ustawi wa jamii na kitababaishwa na ukoloni mambo leo. Pia kitajenga urafiki na mabepari ambao kiliundwa kikabiliane nao na hata kuleta Mapinduzi.
Shauri la 'Maendeleo na Kujichagulia' -- Mwalimu Nyerere alikazia hili katika mawaidha ya 'Uhuru na Maendeleo' kwa kutaja bayana kwamba ni zao la 'Uongozi' na 'Elimu'. Haya katika kuimarisha muktdha wa 'ufanyaji-Maamuzi Jamii'.
Shida ya sasa, ni wanajamii kutochachuka 'kielimu'; kwa kuwa elimu inayotawala kwa sasa, kijamii, si elimu ya 'kumkomboa mtu hasa' bali imetegeshwa kufanya watu wawe tegemezi wa mifumo ya ukoloni mambo leo, ukoloni unaweza hata kujengeka miongoni mwetu sisi wenyewe wenye kudhania tuko kwenye nchi huru. 'Mwenge wa Uhuru' unatukumbusha kuitafuta aina ya Elimu itakayotuweka huru kweli kweli. Hii kuja kukadirisha busara na dhana ya kutambua: 'Hekima ni Uhuru'...
ELIMU 1, ELIMU 2.0 na ELIMU 3.0 ndizo zitakazokadirisha 'Mpangiko Mpya wa Ulimwengu'; huu ni ulimwengu wa watu kuwa 'Nuru' na 'Chumvi' ya Dunia...
Hata kwa utawala wa 'sarafu ya dola', kwa sasa, ni 'New World Order'... Mpangiko Mpya wa Kiulimwengu lakini 'uliyodukuliwa'...
Isikushangaze kusikia, Chama cha Mapinduzi kilisanifiwa ili kuleta uhuru wa kiuchumi wa umma wa Watanzania; pia kuwa kwamba, uongozi wake kimadaraka ya namna zijazo kwa siasa za uwakilishi uje kuwa ni 'nuru ya mataifa' juu ya haki, utu na usawa.
Hata bila kuifikiria BRICS, Chama cha Mapinduzi kinaweza kuleta 'mapinduzi' kwa kukata shauri juu ya namna mpya na tofauti ya Uchumi na Ustawi wa wanajamii--#UCHUMI-MAMA. Jambo hili ndilo suluhu ya ustawi mbovu unaoponza watu kuishi kwa ujanja ujanja, uwizi, ukwapuaji, rushwa, dhulma, kujilimbikizia, ufisadi n.k
Tunachokihitaji ni tu jitihada mpya za muktadha wa 'Studio Maendeleo' na 'Umodelishi' kwa kazi na huduma kuhakikisha kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi, anafanyakazi--HILI LINAWEZEKANA, ni suala la utashi kwa upande wa umma, utawala na mifumo. Mapinduzi ya kitekinolojia, yanatubariki kuweza 'kujiongeza' na hata kujinasibu na maendeleo makubwa siku za mbele. Hili 'litawapita kushoto' wale wote wanaodanganyika na mifumo ya kana 'biashara ni ushindani'... Hata sarafu ya dola inatawala kwa kuwa hatua za makusudi zinatumika kuendesha agenda za 'biashara za kimataifa' kwa faida ya 'Wakubwa'... Na misingi ya biashara hizi 'si usawa' ila 'kuzidiana kete'... Hili linafanya 'uhuni' kuweza kuonekana kuonekana eti ndiyo ujanja....
Pasipo uwezo na kubaini 'mzizi wa fitina' hata watu wa madaraka daima wataishi kulalamika na kutupiana lawama juu ya 'ukosefu wa maadili' na 'tabia mbovu' juu ya utendaji na utumishi wa umma--kama iwavyo hivi kila siku, kila pahala; pale panapokosekana mifumo thabiti ya utawala, ustawi na ulinzi. Mfumo mzima wa fedha na ustawi hauna budi kupitia metamofosia ya 'miundo, sifa na utendaji'--yenye kukidhi ukweli wa kubaini 'Hekima ni Uhuru'... Hivi ndivyo tunavyodhamiria hata katika kuimba 'Hekima, Umoja na Amani' ndizo ngao zetu--Afrika, viongozi na watu wake; kwenye Wimbo wa Taifa.
'Umoja na Amani' havipo kwenye kuishi katika maisha yenye unyonge, umasikini, dharau, ukosefu wa tumaini na chuki. Na vivyo hivyo, jamii nzima haina budi 'kuamka na kuzinduka': hakuna mtu aliye mkombozi kwa mwingine ila yeye mwenyewe... Kama vile alivyosema Mwalimu Kambarage Nyerere katika uzinduzi wa Chama cha Mapinduzi(1977), ikiwa anayepewa nafasi ya uwakilishi ataonekana kutowafaa wananchi na taifa, tena wale wenyekujua ilivyobora, huyo atanyimwa nafasi hiyo ya utumishi ili kupisha wengine wenye wito, kusudi na utashi katika yaliyobora. Na kwamba, kazi ya kujenga uhuru wa mtu ilivyo ni 'utu' ni ngumu kuliko ilivyokuwa katika kuutafuta 'uhuru wa bendera'...
Hatuna budi kuwatia moyo viongozi wetu kuwa na ujasiri katika kujaribu njia tofauti za ustawi badala ya kuwaacha 'wachukulie poa' mambo ambayo tangia awali 'hayajapata kuwa poa'... Tusimame nao watakapokuwa na kifua katika kuyapa nafasi mabadiliko makubwa ya kijamii. 'Fedha, fedha, fedha' si 'mpango mzima' katika kuleta haki, utu na usawa katika nasibu ya 'maendeleo ya watu na vitu'. Ingawaje kutingwa kupo kiasi cha kudhani ama kuona hakuna nafasi ya kujaribu lililotofauti. Tuwe na uwazi na ujasiri kukumbushana: kusifiwa sana ni 'mtego kwa kiongozi' kwa kuwa sifa za kinafiki ni 'mkakati' na 'mtaji' wa mafundi wa kutafuta kula na vipofu... Ingalikuwa kheri kujihadhari na hadaa za michezo ya 'siasa za tawala'. Wala hakuna haja ya kutengeneza njia ya 'utawala wa muda mrefu' kwa kuendekeza 'siasa za kuuza kwa umma' kwa ku-fosi kingi. Nia thabiti ya kuonesha ujasiri dhidi ya mifumo, hata ikikiriwa hivyo mbele za watu wachache wenye namna, inatosha. Katika Ustawi, yote ni matokeo--hauwezi kupanda pilipili ukaja kuvuna parachichi...
Nafasi ya mabadiliko makubwa, kwa mwaka huu na kusonga, ni kama 'goli la wazi'; yote yanawezekana--'kukomaa na shughuli tete ili kudumu sana na kuacha alama' ama 'wakati uamue kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0'. Kwa kuwa 'mabadiliko makubwa yatachukua muda kukadirishwa na kudhihiri'--na hali hata safari ndefu huanza na hatua moja. Shauri hili ni sawa na kuwa kwenye njia panda ilivyo ni >
Kisebusebu na roho kipapo<-- kama alivyopata kuandika William Shakespear:
'Kuwa' au 'Kutokuwa' hilo ndilo swali...
Baraka, Imani na Tumaini daima vipo na mtu mwenye kujua ilivyo bora, na basi kuchagua ilivyobora.
Msaada upo popote penye nia, kadri vile penye nia pana njia...