Je, Tatizo ni Shetani ? Au ni maamuzi yako ?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Unaweza kuomba, kufunga na kusema “Nakataa umaskini!” lakini kama hujabadilisha maamuzi, nidhamu, matumizi na namna unavyotafuta kipato, maisha yako yanaweza kubaki yaleyale.

Wengine kila mwaka wanaomba mafanikio, lakini wanaendelea na madeni yale yale, matumizi yale yale, ujuzi ule ule na maamuzi yale yale. Halafu wakikwama wanasema, “Shetani anapigana na fedha zangu.”

Wakati mwingine si shetani ni sisi wenyewe tunajirudisha nyuma.

Jifunze ujuzi mpya. Tafuta fursa. Punguza matumizi yasiyo ya lazima. Acha kukopa ili kuwafurahisha watu. Jenga nidhamu ya fedha na anza kutumia kile kidogo ulicho nacho kwa hekima.

Omba, lakini chukua hatua. Imani iende sambamba na juhudi.

Kwa sababu huwezi kuomba maisha mapya huku ukiendelea kuishi kwa maamuzi yale yale.

Usiombe tu maisha yako yabadilike—anza kubadilika wewe.
 
kuna muda mahamuzi yako uwa yanakosa nguvu mbele ya roho zinazokuhusu kwakua nazo uwa zinaitaji usawa kwaiyo kiujumla mafanikio yanaitaji kwenda sawa na roho zinazokuhusu
 
Swala ni maamuzi na subira Kuna wanaofanya kazi kwa bidii nao hawafanikiw as long as wanaendelea kusonga mbele mambo yanabadilika taratibu kuomba sana Kuna saidia kwasababu Kuna nguvu za giza na Ulimwengu wa kiroho unamambo mengi sana swala la msingi ni kuendelea KUPAMBANA na kufanya kazi kiasi kwamba usiache kazi ukakimbilia kwenye ibada kwenda kuomba Mungu aboreshe Maisha yako wakati umeacha kwenda kazini, na wapenda Islamic anafunga duka ek45 anakwenda kuswali akirud anafungua na kuendelea na biashara
 
Tatizo linaanza na wewe mwenyewe halafu Shetani anakusaidia kumalizia plan yako
 
Unaweza kuomba, kufunga na kusema “Nakataa umaskini!” lakini kama hujabadilisha maamuzi, nidhamu, matumizi na namna unavyotafuta kipato, maisha yako yanaweza kubaki yaleyale.

Wengine kila mwaka wanaomba mafanikio, lakini wanaendelea na madeni yale yale, matumizi yale yale, ujuzi ule ule na maamuzi yale yale. Halafu wakikwama wanasema, “Shetani anapigana na fedha zangu.”

Wakati mwingine si shetani ni sisi wenyewe tunajirudisha nyuma.
Ingefaa na Tukumbuke daima kwamba bila Shetani; kusingelikuwako na maendeleo yoyote hapa duniani.

Back
Top Bottom