Je, TBS wana kitengo cha ukaguzi wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya kuchunguza simu na betri zinazoingizwa nchini?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Shambulio ambalo kawaida linaitwa la kigaidi lililofanywa na Israel nchini Lebanon lazima lituzindue na kutufanya tuanze ukaguzi wa kina wa vifaa vya kielektroniki vinavyoingia nchini. Je, kitengo hicho kipo TBS?

Kuanzia sasa, ni muhimu kwamba simu na betri zinazoingizwa nchini zifanyiwe majaribio ya kutosha katika maeneo ya mpaka. Kwanza, waanze na betri.

Pia, makampuni ya simu yanapaswa kuweka mikakati maalum ili watu waweze kutuma ujumbe mmoja kwa idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja. Katika tukio la Lebanon, walipokea ujumbe mmoja kutoka chanzo kimoja na karibu wote walifungua ujumbe huo kwa pamoja, ambayo ilikuwa kama switch ya bomu ndani ya simu zao.
 
Mkuu hapa una hoja!! Tuache masihara INATISHA
Mtu katika familia anakusudia kuidhuru familia yake.Anatuma ujumbe mmoja halafu ndugu wakifungua wanaumia au kufa kwa pamoja.
 

Usalama wa wa-Tanzania unalindwa na Mungu pekee.
 
tiibiiesii hao hamna kitu wako kwa ajili ya kula wao na familia zao, unakumbuka kipindi cha magari kukaguliwa huko nyumbani kwa kushirikiana na NIT? kimsingi hamna kipindi mafamba na maskrepa yaliingia kama kile mpaka wakaamua ukaguzi urudi kwenye nchi husika , kuna vitaasisi vinapiga hela lakini havina msaada kwa mwananchi wa kawaida.
 
Mimi nawajua sana hawa ndio maana nimeona niwape tahadhari.
Lebanon kuanzia leo hakuna ruhusa walkie talkie wala pager kuingia nazo uwanja wa ndege.
Nchi zote duniani zingetoa tangazo la marufuku kwa muda kwa bidhaa hizo zote zilizotokea Taiwan.Hungary na Japan
 

Hosea 4: 6

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
 
Nani akushambulie 😄
Tbs,sjui tfda wenyewe hawakaguwi kuanzia vifaa vya kieletronik mpk vyakula,vinywaji

Ova
 
Wana vifaa vya kila aina shida ni matumizi sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…