Je, teknolojia katika ufugaji wa samaki inaweza kuleta athari?

Good,
Kama miaka mitano nyuma nilifuga tilapia chotara na wale Mozambicus na cat fish. Ni kweli mbegu za asili zinatoweka kwa kasi ya ajabu, mimi nimeamua kutunza mbegu hizi za asili, mozambicus, tilapia na cat fish. Kwa sasa nakusanya cat fish jamii mbalimbali na kuwatunza vizuri.
Mkuu sio mbay ukanicheki kunipa mwongozo ABC nkuja pm saivi.
 
Hizo za zege ndio nimewatoq catfish humo kwangu hawaongezek nimewawek waishi kama watakavyoishi wakiw ktk natural ponds...

Tilapia akiwa ktk ponds za zege uzaliaji wake si mkubwa maana kwa jinsi nilivyowasoma tabia yao wana mtindo wa kutengenez viota kama Kuku.. sasa ktk hii natural pond langu wanaviota vya kutosha sana...
Naomba kujua kuna wale tilapia ambao hawazaliani. unachukua mbegu unaweka bwawani kwako wakifikia uzito unaotakiwa unawavua, unasafisha bwawa unaweka vifaranga vipya. sasa kwa aina hii kwenye bwawa la zege na bwawa la kawaida kuna utofauti wa ukuaji? Given huduma za chakula, aeration na kubadili maji iko constant
 
Hakuna kitu mtaalam atakuja kupinga hata kama kitakuwa na athari kwa baadaye, kumbuka aliyezindua ufungaji huo ni nani alafu huyo mtaalam ambaye hajitaki ataongelea wapi?.

Labda aww humu JF kwa avatar fake ndipo apandishw uzi, vinginevyo subirini hadi yatukute ndipo wataalam fake waongee kwa wkt huo.
Duh!!.Kwa hiyo tusiwaamini wataalamu?.Watu waliosomeshwa kwa kodi zetu?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Duh!!.Kwa hiyo tusiwaamini wataalamu?.Watu waliosomeshwa kwa kodi zetu?.
Wataalam wenyewe wameamua kuingiliwa na wanasiasa unataka umuamini vipi?.

Sato, Sangara nk, wote hao wapo ziwa Victoria na wanazaliana kulingana na wkt na majira yao, wkt fulani Magufuri (late) alizuia kuvua samaki kwa kipindi fulani ili wazaliane na hata baadaye akasema uvuaji wa samaki usiwe uvuvi wa samaki size fulani.

Yote hiyo ilikuwa na makusudi ya kutunza uzao kwa wingi fulani, ila unajua baadaye kilichoendelea.

Sasa leo wataalam badala ya kushauri as hapo nyuma wanakubali kuketwa kwa samaki uzao mpya ambao najua hawajafanyiwa utafiti rafiki, tena wanalelewa ziwani kwenye maeneo maalum.

Kumbuka hilo eneo halitadumu kufugia samaki nakupa 2 to 3yrs hakutakuwa na hizo shoroba za uzalishaji wa samaki hapo Mwanza.

Tunza hii.
 
Naomba kujua kuna wale tilapia ambao hawazaliani. unachukua mbegu unaweka bwawani kwako wakifikia uzito unaotakiwa unawavua, unasafisha bwawa unaweka vifaranga vipya. sasa kwa aina hii kwenye bwawa la zege na bwawa la kawaida kuna utofauti wa ukuaji? Given huduma za chakula, aeration na kubadili maji iko constant
Hapo huwa wanaweka jinsia moja na mara nyingi ni MADUME pekee...

Kwa upande wa Tilapia Dume huwa ni mkubwa kuliko jike. So.. dume atakupa faida zaidi, na ndio maana huwa wanawafugq madume tupu. So ukiweka madume 1000 basi uhakika wa kuvuna samaki 950+ ni mkubwa.

Ila, ukiweka jinsia tofauti 1000 utavuna samaki zaidi ya 2000 ila wana variation ya uzito, jinsia, pia na quality. Kingine itakucost chakula kingi bila kusahau utatumia muda mrefu zaidi kuwasubiri wakue ktk zile grams ulizoweka target.

Mbinu ni kufuga jinsia moja tu.. ndio utapata matokeo hayo.
 
Ukuaji wa uchumi wa nchi ni pamoja na matumizi ya teknolojia mbalimbali ili kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla.

Katika Sekta ya uvuvi, kilimo cha samaki kimekuwa kikihimizwa kila leo kwa lengo la kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya soko.

Kwa Tanzania nimekuwa nikiona mabwawa yakichimbwa kwa ajili ya ufugaji samaki.

Lakini kumbe si mabwawa tu, pia fish cages zinaweza kutandikwa ziwani na uzalishaji wa samaki ukaendelea.

Kilichonifanya niandike hapa:-

i) Mbegu ngeni inayoletwa (Spp. ngeni)

Ufugaji huu unahusisha mbegu ngeni kutoka nchi za wenzetu (Tilapia spp) na inasemekana mbegu ngeni ni tamu ukilinganisha na hii ya kwetu ya asili.

Je, uwepo wa mbegu hii ngeni haiwezi kuitawala Spp. tuliyonayo, na mwisho wa siku tukapoteza kabisa ile ya kwetu?

ii) Aina ya chakula
Chakula kinachotumika kuwalisha hawa samaki inasemekana kina kemikali ambazo baadaye huwaathiri samaki majike na kugeuka kuwa madume.

Je, endapo hiyo kemikali itaathiri samaki wa asili na kukumbwa na mabadiliko hayo,kuzaliana kwa samaki wa asili kutaendelea kuwa sawa?

iii) Uvuvi haramu
Serikali yetu imekuwa ikipiga vita juu ya uvuvi haramu, je, huu uwekezaji hatuwezi kuuterm katika uvuvi haramu?

Wataalamu wa masuala ya uvuvi na kilimo cha samaki, naombeni elimu kuhusu hili.

[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]
Na wasiwasi na elimu yako hio point nmb 2 umetuingiza chaka mzee hicho chakula cha kuwalisha kinatokana na mioango yako ipoje labda unahitaji kuzalisha samaki wa jinsia moja hivo utawalisha ili kuwabadili sex kwaio bicho chkl ni maalumu kwa ajili ya kuchange sex.
Kuhusu mbegu offcourse ni chache lkn unaweza kuzipata kwa wazalishaji wengine pia sio lazima uagize toka nje ya nchi.
Tumia wild seed
Kusema kwmb tilapia wa asili si watamu mbn sio kweli
Kuhusu chakula unaweza ukatengeneza chako pia sio lazima ununue
 
Hujaelewa swali langu.

Mkuu, mimi sio mtaalamu wa aquaculture ndio maana nimeleta hapa kupata uelewa, lakini hata hivyo swali langu ni, je, hicho chakula chenye mlengo wa kubadili jinsi ya samaki hakiwezi kuwaathiri samaki wa asili? Jike [emoji3591]dume, na kupunguza mazalia asilia ya samaki?

Kumbuka naongelea matokeo hasi ya ufugaji wa samaki kwenye vyanzo asilia.
 
Ukuaji wa uchumi wa nchi ni pamoja na matumizi ya teknolojia mbalimbali ili kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla.

Katika Sekta ya uvuvi, kilimo cha samaki kimekuwa kikihimizwa kila leo kwa lengo la kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya soko.

Kwa Tanzania nimekuwa nikiona mabwawa yakichimbwa kwa ajili ya ufugaji samaki.

Lakini kumbe si mabwawa tu, pia fish cages zinaweza kutandikwa ziwani na uzalishaji wa samaki ukaendelea.

Kilichonifanya niandike hapa:-

i) Mbegu ngeni inayoletwa (Spp. ngeni)

Ufugaji huu unahusisha mbegu ngeni kutoka nchi za wenzetu (Tilapia spp) na inasemekana mbegu ngeni ni tamu ukilinganisha na hii ya kwetu ya asili.

Je, uwepo wa mbegu hii ngeni haiwezi kuitawala Spp. tuliyonayo, na mwisho wa siku tukapoteza kabisa ile ya kwetu?

ii) Aina ya chakula
Chakula kinachotumika kuwalisha hawa samaki inasemekana kina kemikali ambazo baadaye huwaathiri samaki majike na kugeuka kuwa madume.

Je, endapo hiyo kemikali itaathiri samaki wa asili na kukumbwa na mabadiliko hayo,kuzaliana kwa samaki wa asili kutaendelea kuwa sawa?

iii) Uvuvi haramu
Serikali yetu imekuwa ikipiga vita juu ya uvuvi haramu, je, huu uwekezaji hatuwezi kuuterm katika uvuvi haramu?

Wataalamu wa masuala ya uvuvi na kilimo cha samaki, naombeni elimu kuhusu hili.

[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]
Nikiwa kama mtaalamu na mdau wa ufugaji samaki Naomba kuchagia kwa kujibu maswali yako kama ifuatavyo

i) upandikizwaji ya samaki wasiokuwa wa asili - ni sahihi kabisa hii inawaza kusababisha biological pollution kama samaki watachanganyikana na samaki wa asili kuna uwezekana mkubwa wa kuzalisha species mpya kabisa na kama samaki hao ni carnivorous kuna hatari ya samaki hao kuwala samaki wa asili.

ii) Matumizi wa hormone - kwenye uzalishaji wa kuna husisha matumizi ya hormone 17-alpha methyltestorone kwa ajili ya kufanya sex reversal kuzalisha samaki wenye sifa za kiume ili kupunguza kuzaliana na kufanya samaki wakue haraka

Matumizi ya hii hormone hayana madhara yoyote kwa mtumiaja na hata kwa samaki wa asili sababu uwekwa kwa kiwango kidogo sana na Huish nguvu mapema kabla ya kumfikia mlaji wa mwisho

Kwa samaki wa asili amna madhara kwa sababu matumizi ya hormone ufanyika hatchery kwa ungalizi maalumu hadi pale vifaranga vinapomaliza dose ndio upelekwa kwenye bwawa au cage

Kwa sasa hatutumii tena hormone kuzalisha samaki wenye sifa za kiume, tunatumia njia inayofaamika kama YY. Kwenye hii njia tunatumia samaki madume (super male) ambao wakizaliana na majike vifaranga vyote vitakavyozaliwa vinakuwa madume tu

Naomba kuwasilisha
 
iii) Huu ufugaji samaki uwezi kuuterm kama ufugaji haramu kwa sababu unahusisha kuzalisha na kuwalea samaki katika mazingira yanayodhibitiwa kama vile mabwawa, matangi, au mabwawa ya samaki, badala ya kuwakamata kutoka vyanzo asilia kwa kutumia njia haramu kama vile chemicals, nyavu ndogo au mbinu zinazo haribu mazingira.

Ufugaji wa samaki ni rafiki kwa mazingira kwa sababu inapunguza fishing pressure kwa kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya watu na kuwa kama njia mdala ya kuzalisha samaki kwa uhakika zaidi
 
Karibu Mkuu mimi ni mtaalamu

Ingefaa zaidi kama ungenunua mbegu kutoka chanzo cha kuaminika ili uwe na uelewa wa aina gani (species) gani unafuga na sifa zao zikoje

Swala la kutofautiana rangi kwa uelewa wangu ni kwa sababu majike na madume wanatofautiana rangi dume anakuwa na rangi yenye mvuto iliyochanyikana na blue au nyekundu ila jike anakuwa na rangi moja

Hao wenye madoa mara nyingi wanatoka kwenye vyanzo vya hasiri mara nyingi ni kwenye chanzo cha maji unachotumia mfano mto

Ni sahihi, muhimu sana kuwapa samaki chakula kulingana na umri/size ya mdomo wao

Njia rahisi zaidi ni kuwatenga samaki kulingana na size zao, haishauliwi kuchanganya smaaki wakubwa na wadogo kwenye bwawa moja

Itakupa ugumu sana kwenye management na kucontrol production

Unaweza nicheck PM tukashare experience physical au kwa kutumia videos

Uzi kama huu hutoona wachangiaji wengi kwa sababu Mitanzania mingi akili zao wanazijua wenyewe.. mambo ya kipumbavu na umbea umbea utawaona mpaka wanaitana.

Nirudi ktk mada.

Binafsi nafuga Tilapia.. kwa njia ya kienyeji yaani bwawa la ukubwa wa 15x30.. kuna changamoto niliipata ktk ufugaji huu, hivyo natamani sana kuongeza maarifa, pia swala la mbegu ni jambo la muhimu sana, mie nilijikuta nina mbegu zaidi ya 4/5 za tilapia.

Kuanzia wale plain, wenye rangi nyekundu, wenye madoadoa, black etc.. pia ukuaji ukawa una variation.. jambo jingine ni chakula.. nilikuwa naandaa mwenyewe ila kuna namna ya kutengenez chakula kulingana na umri na size yao so haya yote yanahitaj elimu na exposure ya wafugaj wengine wanafanyaje..

Mkuu wewe unafuga or?
 
Mie kwa sasa nawafuga pamoja na Tilapia.. na nashangaa kuna utulivu wa hali ya juu.. ingawa wanasema Catfish anakula Tilapia.
Uwa unafanya sampling kujilizisha kama idadi uliyoweka na iliyopo sasa hv ni sawa?

Ni kweli Kambare anakula samaki wenzake ambao ni wadogo kuliko wao, ili uwafuge pamoja ni muhimu Tilapia awe mkubwa mara tatu zaidi ya Tilapia ndio wanaweza kukaa bila shida

Nahisi wewe unaona awakulani kwa sababu Tilapia wanazaliana sana, kinachotokea Kambale anakula vifaranga na inaonekana idadi ya kambale ni kubwa zaidi kuliko Tilapia
 
Naomba kujua kuna wale tilapia ambao hawazaliani. unachukua mbegu unaweka bwawani kwako wakifikia uzito unaotakiwa unawavua, unasafisha bwawa unaweka vifaranga vipya. sasa kwa aina hii kwenye bwawa la zege na bwawa la kawaida kuna utofauti wa ukuaji? Given huduma za chakula, aeration na kubadili maji iko constant
Hapana amna utofauti kujenga au kutokujengea inatokana na ardhi kama ardhi yako inauwezo mzuri wa kutunza maji amna haja ya kujengea, kujenga concrete pond ni kunafanyika kwenye maeneo ambapo ardhi yake haina uwezo wa kutunza maji lakini matokeo ni hayo kama kila kitu kiko constant
 
Nikiwa kama mtaalamu na mdau wa ufugaji samaki Naomba kuchagia kwa kujibu maswali yako kama ifuatavyo

i) upandikizwaji ya samaki wasiokuwa wa asili - ni sahihi kabisa hii inawaza kusababisha biological pollution kama samaki watachanganyikana na samaki wa asili kuna uwezekana mkubwa wa kuzalisha species mpya kabisa na kama samaki hao ni carnivorous kuna hatari ya samaki hao kuwala samaki wa asili.

ii) Matumizi wa hormone - kwenye uzalishaji wa kuna husisha matumizi ya hormone 17-alpha methyltestorone kwa ajili ya kufanya sex reversal kuzalisha samaki wenye sifa za kiume ili kupunguza kuzaliana na kufanya samaki wakue haraka

Matumizi ya hii hormone hayana madhara yoyote kwa mtumiaja na hata kwa samaki wa asili sababu uwekwa kwa kiwango kidogo sana na Huish nguvu mapema kabla ya kumfikia mlaji wa mwisho

Kwa samaki wa asili amna madhara kwa sababu matumizi ya hormone ufanyika hatchery kwa ungalizi maalumu hadi pale vifaranga vinapomaliza dose ndio upelekwa kwenye bwawa au cage

Kwa sasa hatutumii tena hormone kuzalisha samaki wenye sifa za kiume, tunatumia njia inayofaamika kama YY. Kwenye hii njia tunatumia samaki madume (super male) ambao wakizaliana na majike vifaranga vyote vitakavyozaliwa vinakuwa madume tu

Naomba kuwasilisha
Asante kwa elimu na ufafanuzi mzuri mkuu🤝🤝.

Nilichelewa kuona comment yako.
 
Samaki wanaofugwa kwenye cage system hawawezi kuwa wanavuliwa kiharamu maana wale wanafugwa hawavuliwi kutoka katika mazingira yao ya asili. hivyo huwa wanavunwa kama wanavyovuna mazao mengine waliyopanda na hapo ni baada ya kufikisha umri sahihi na uzito sahihi kwa ajili ya kuvunwa.
Huoni kwamba magonjwa yana weza kuathiri samaki ambao hawako kwenye hizo cage kutokana na chakula wanaolishwa samaki wakwenye cage?
 
Uzi kama huu hutoona wachangiaji wengi kwa sababu Mitanzania mingi akili zao wanazijua wenyewe.. mambo ya kipumbavu na umbea umbea utawaona mpaka wanaitana.

Nirudi ktk mada.

Binafsi nafuga Tilapia.. kwa njia ya kienyeji yaani bwawa la ukubwa wa 15x30.. kuna changamoto niliipata ktk ufugaji huu, hivyo natamani sana kuongeza maarifa, pia swala la mbegu ni jambo la muhimu sana, mie nilijikuta nina mbegu zaidi ya 4/5 za tilapia.

Kuanzia wale plain, wenye rangi nyekundu, wenye madoadoa, black etc.. pia ukuaji ukawa una variation.. jambo jingine ni chakula.. nilikuwa naandaa mwenyewe ila kuna namna ya kutengenez chakula kulingana na umri na size yao so haya yote yanahitaj elimu na exposure ya wafugaj wengine wanafanyaje..

Mkuu wewe unafuga or?
Mambo unafuga wapi nije kuona.
 
Ukuaji wa uchumi wa nchi ni pamoja na matumizi ya teknolojia mbalimbali ili kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla.

Katika Sekta ya uvuvi, kilimo cha samaki kimekuwa kikihimizwa kila leo kwa lengo la kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya soko.

Kwa Tanzania nimekuwa nikiona mabwawa yakichimbwa kwa ajili ya ufugaji samaki.

Lakini kumbe si mabwawa tu, pia fish cages zinaweza kutandikwa ziwani na uzalishaji wa samaki ukaendelea.

Kilichonifanya niandike hapa:-

i) Mbegu ngeni inayoletwa (Spp. ngeni)

Ufugaji huu unahusisha mbegu ngeni kutoka nchi za wenzetu (Tilapia spp) na inasemekana mbegu ngeni ni tamu ukilinganisha na hii ya kwetu ya asili.

Je, uwepo wa mbegu hii ngeni haiwezi kuitawala Spp. tuliyonayo, na mwisho wa siku tukapoteza kabisa ile ya kwetu?

ii) Aina ya chakula
Chakula kinachotumika kuwalisha hawa samaki inasemekana kina kemikali ambazo baadaye huwaathiri samaki majike na kugeuka kuwa madume.

Je, endapo hiyo kemikali itaathiri samaki wa asili na kukumbwa na mabadiliko hayo,kuzaliana kwa samaki wa asili kutaendelea kuwa sawa?

iii) Uvuvi haramu
Serikali yetu imekuwa ikipiga vita juu ya uvuvi haramu, je, huu uwekezaji hatuwezi kuuterm katika uvuvi haramu?

Wataalamu wa masuala ya uvuvi na kilimo cha samaki, naombeni elimu kuhusu hili.

[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]
Mi nachangia kidogo hapo kwenye point ya Pili.Ulishaji WA chakula Chenye hormone unafanyika wiki ya pili baada ya vifaranga kuanguliwa,nadhani tuna assume mpaka muda wa kuvuna samaki miezi kadhaa mbele effect hazitakwepo.
Ila njia hii imeshakua ya kizamani Kwa vile haina uhakika,haibadilishi jinsia asilimia 100% kuna baadhi ya samaki watabaki majike hivyo sio effective.
Njia inayotumika sasa hivi ni kuzalisha vifaranga Kwa kutumia yy male,Kwa hivyo vifaranga wanazalishwa wanakua 100% male.
 
Back
Top Bottom