Je, teknolojia katika ufugaji wa samaki inaweza kuleta athari?

Mkuu sio mbay ukanicheki kunipa mwongozo ABC nkuja pm saivi.
 
Naomba kujua kuna wale tilapia ambao hawazaliani. unachukua mbegu unaweka bwawani kwako wakifikia uzito unaotakiwa unawavua, unasafisha bwawa unaweka vifaranga vipya. sasa kwa aina hii kwenye bwawa la zege na bwawa la kawaida kuna utofauti wa ukuaji? Given huduma za chakula, aeration na kubadili maji iko constant
 
Duh!!.Kwa hiyo tusiwaamini wataalamu?.Watu waliosomeshwa kwa kodi zetu?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Duh!!.Kwa hiyo tusiwaamini wataalamu?.Watu waliosomeshwa kwa kodi zetu?.
Wataalam wenyewe wameamua kuingiliwa na wanasiasa unataka umuamini vipi?.

Sato, Sangara nk, wote hao wapo ziwa Victoria na wanazaliana kulingana na wkt na majira yao, wkt fulani Magufuri (late) alizuia kuvua samaki kwa kipindi fulani ili wazaliane na hata baadaye akasema uvuaji wa samaki usiwe uvuvi wa samaki size fulani.

Yote hiyo ilikuwa na makusudi ya kutunza uzao kwa wingi fulani, ila unajua baadaye kilichoendelea.

Sasa leo wataalam badala ya kushauri as hapo nyuma wanakubali kuketwa kwa samaki uzao mpya ambao najua hawajafanyiwa utafiti rafiki, tena wanalelewa ziwani kwenye maeneo maalum.

Kumbuka hilo eneo halitadumu kufugia samaki nakupa 2 to 3yrs hakutakuwa na hizo shoroba za uzalishaji wa samaki hapo Mwanza.

Tunza hii.
 
Hapo huwa wanaweka jinsia moja na mara nyingi ni MADUME pekee...

Kwa upande wa Tilapia Dume huwa ni mkubwa kuliko jike. So.. dume atakupa faida zaidi, na ndio maana huwa wanawafugq madume tupu. So ukiweka madume 1000 basi uhakika wa kuvuna samaki 950+ ni mkubwa.

Ila, ukiweka jinsia tofauti 1000 utavuna samaki zaidi ya 2000 ila wana variation ya uzito, jinsia, pia na quality. Kingine itakucost chakula kingi bila kusahau utatumia muda mrefu zaidi kuwasubiri wakue ktk zile grams ulizoweka target.

Mbinu ni kufuga jinsia moja tu.. ndio utapata matokeo hayo.
 
hongera sana mkuu. moja kitu nachowaza sana kukifanya siku za usoni. Je unafugia wapi mkuu?
Shukran, nafugia Tabata, Maeneo ya Kinyerezi. Nina eneo kama la nusu acre hivi. Ila kwa bwawa nimetenga kipande kiasi.
 
Na wasiwasi na elimu yako hio point nmb 2 umetuingiza chaka mzee hicho chakula cha kuwalisha kinatokana na mioango yako ipoje labda unahitaji kuzalisha samaki wa jinsia moja hivo utawalisha ili kuwabadili sex kwaio bicho chkl ni maalumu kwa ajili ya kuchange sex.
Kuhusu mbegu offcourse ni chache lkn unaweza kuzipata kwa wazalishaji wengine pia sio lazima uagize toka nje ya nchi.
Tumia wild seed
Kusema kwmb tilapia wa asili si watamu mbn sio kweli
Kuhusu chakula unaweza ukatengeneza chako pia sio lazima ununue
 


Hujaelewa swali langu.

Mkuu, mimi sio mtaalamu wa aquaculture ndio maana nimeleta hapa kupata uelewa, lakini hata hivyo swali langu ni, je, hicho chakula chenye mlengo wa kubadili jinsi ya samaki hakiwezi kuwaathiri samaki wa asili? Jike [emoji3591]dume, na kupunguza mazalia asilia ya samaki?

Kumbuka naongelea matokeo hasi ya ufugaji wa samaki kwenye vyanzo asilia.
 
Nikiwa kama mtaalamu na mdau wa ufugaji samaki Naomba kuchagia kwa kujibu maswali yako kama ifuatavyo

i) upandikizwaji ya samaki wasiokuwa wa asili - ni sahihi kabisa hii inawaza kusababisha biological pollution kama samaki watachanganyikana na samaki wa asili kuna uwezekana mkubwa wa kuzalisha species mpya kabisa na kama samaki hao ni carnivorous kuna hatari ya samaki hao kuwala samaki wa asili.

ii) Matumizi wa hormone - kwenye uzalishaji wa kuna husisha matumizi ya hormone 17-alpha methyltestorone kwa ajili ya kufanya sex reversal kuzalisha samaki wenye sifa za kiume ili kupunguza kuzaliana na kufanya samaki wakue haraka

Matumizi ya hii hormone hayana madhara yoyote kwa mtumiaja na hata kwa samaki wa asili sababu uwekwa kwa kiwango kidogo sana na Huish nguvu mapema kabla ya kumfikia mlaji wa mwisho

Kwa samaki wa asili amna madhara kwa sababu matumizi ya hormone ufanyika hatchery kwa ungalizi maalumu hadi pale vifaranga vinapomaliza dose ndio upelekwa kwenye bwawa au cage

Kwa sasa hatutumii tena hormone kuzalisha samaki wenye sifa za kiume, tunatumia njia inayofaamika kama YY. Kwenye hii njia tunatumia samaki madume (super male) ambao wakizaliana na majike vifaranga vyote vitakavyozaliwa vinakuwa madume tu

Naomba kuwasilisha
 
iii) Huu ufugaji samaki uwezi kuuterm kama ufugaji haramu kwa sababu unahusisha kuzalisha na kuwalea samaki katika mazingira yanayodhibitiwa kama vile mabwawa, matangi, au mabwawa ya samaki, badala ya kuwakamata kutoka vyanzo asilia kwa kutumia njia haramu kama vile chemicals, nyavu ndogo au mbinu zinazo haribu mazingira.

Ufugaji wa samaki ni rafiki kwa mazingira kwa sababu inapunguza fishing pressure kwa kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya watu na kuwa kama njia mdala ya kuzalisha samaki kwa uhakika zaidi
 
Karibu Mkuu mimi ni mtaalamu

Ingefaa zaidi kama ungenunua mbegu kutoka chanzo cha kuaminika ili uwe na uelewa wa aina gani (species) gani unafuga na sifa zao zikoje

Swala la kutofautiana rangi kwa uelewa wangu ni kwa sababu majike na madume wanatofautiana rangi dume anakuwa na rangi yenye mvuto iliyochanyikana na blue au nyekundu ila jike anakuwa na rangi moja

Hao wenye madoa mara nyingi wanatoka kwenye vyanzo vya hasiri mara nyingi ni kwenye chanzo cha maji unachotumia mfano mto

Ni sahihi, muhimu sana kuwapa samaki chakula kulingana na umri/size ya mdomo wao

Njia rahisi zaidi ni kuwatenga samaki kulingana na size zao, haishauliwi kuchanganya smaaki wakubwa na wadogo kwenye bwawa moja

Itakupa ugumu sana kwenye management na kucontrol production

Unaweza nicheck PM tukashare experience physical au kwa kutumia videos

 
Mie kwa sasa nawafuga pamoja na Tilapia.. na nashangaa kuna utulivu wa hali ya juu.. ingawa wanasema Catfish anakula Tilapia.
Uwa unafanya sampling kujilizisha kama idadi uliyoweka na iliyopo sasa hv ni sawa?

Ni kweli Kambare anakula samaki wenzake ambao ni wadogo kuliko wao, ili uwafuge pamoja ni muhimu Tilapia awe mkubwa mara tatu zaidi ya Tilapia ndio wanaweza kukaa bila shida

Nahisi wewe unaona awakulani kwa sababu Tilapia wanazaliana sana, kinachotokea Kambale anakula vifaranga na inaonekana idadi ya kambale ni kubwa zaidi kuliko Tilapia
 
Hapana amna utofauti kujenga au kutokujengea inatokana na ardhi kama ardhi yako inauwezo mzuri wa kutunza maji amna haja ya kujengea, kujenga concrete pond ni kunafanyika kwenye maeneo ambapo ardhi yake haina uwezo wa kutunza maji lakini matokeo ni hayo kama kila kitu kiko constant
 
Asante kwa elimu na ufafanuzi mzuri mkuu🤝🤝.

Nilichelewa kuona comment yako.
 
Huoni kwamba magonjwa yana weza kuathiri samaki ambao hawako kwenye hizo cage kutokana na chakula wanaolishwa samaki wakwenye cage?
 
Mambo unafuga wapi nije kuona.
 
Mi nachangia kidogo hapo kwenye point ya Pili.Ulishaji WA chakula Chenye hormone unafanyika wiki ya pili baada ya vifaranga kuanguliwa,nadhani tuna assume mpaka muda wa kuvuna samaki miezi kadhaa mbele effect hazitakwepo.
Ila njia hii imeshakua ya kizamani Kwa vile haina uhakika,haibadilishi jinsia asilimia 100% kuna baadhi ya samaki watabaki majike hivyo sio effective.
Njia inayotumika sasa hivi ni kuzalisha vifaranga Kwa kutumia yy male,Kwa hivyo vifaranga wanazalishwa wanakua 100% male.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…