Je, tetesi kwamba matokeo ya uchaguzi uliomalizika Simba Sc yanachangia kuathiri uwezo wa timu uwanjani, zina uzito kiasi gani?

Je, tetesi kwamba matokeo ya uchaguzi uliomalizika Simba Sc yanachangia kuathiri uwezo wa timu uwanjani, zina uzito kiasi gani?

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam..!!

Katika pita pita zangu mitaani nimekutana na maneno toka kwa wadau wa Simba Sc, hasa mashabiki na wanachama wake, wanaodai kwamba, uchaguzi wa Simba Sc kufanyika wakati ule [katikati ya msimu] yamechangia kuathiri uwezo wa timu uwanjani.

Binafsi napata mashaka na uzito wa madai hayo kwasababu moja kubwa, kwamba, timu ya Simba Sc kwasasa iko chini ya mwekezaji Mo, huyu ndie yupo "responsible" kwa mahitaji yote muhimu ya timu, kuanzia chakula, malazi, usafiri, usajili, mishahara ya wachezaji, na mengineyo.

Kwangu ningeyaona madai hayo [tetesi hizo] zina uzito endapo kama bado timu ya Simba Sc ingekuwa na mfumo uliopita kabla ya ujio wa mwekezaji, ambapo watu binafsi walikuwa wakisajili wachezaji wao, kuwalipa mishahara, na kulazimisha kocha mkuu awapange wachezaji wao, hata kama hawana uwezo uwanjani lengo likiwa kuwatafutia masoko nje kupitia Simba Sc.

Kwa akili ya kawaida, ungetambua kwamba, hawa wachezaji walikuwa na uwezo wa kuwasikiliza mabosi wao waliowasajili na kuwalipa mishahara, pale ambapo mambo binafsi ya mabosi hao hayakwenda vizuri ndani ya klabu, ikiwemo kushindwa uchaguzi, hivyo kuwaambia wachezaji wao wacheze chini ya kiwango ili kuwakomoa wapinzani wao walioshinda uchaguzi.

Lakini leo Mo anatoa kila kitu, hao watu waliopo nje ya timu [kama kweli wapo] wenye uwezo wa kuwashawishi wachezaji kucheza chini ya kiwango na kuathiri matokeo ya timu uwanjani ni wakina nani? na iweje wawe na nguvu kubwa kiasi hicho ya ushawishi kwa wachezaji [ kama wapo]?

Yangu ni hayo tu ...
 
Naona madai haya yanazidi kupata nguvu, baada ya kuona taarifa ya Hassan Dalali kumtaka mwenyekiti Mangungu ayaweke pamoja makundi yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi uliokwisha hivi karibuni.

Mpira wetu una mambo mengi sana ya ajabu ajabu, huu haufai kufananishwa na mpira wa nchi zilizoendelea kama Ulaya na Marekani, mara nyingi mpira wa kibongo una mambo yake kibongo bongo.
 
Kwani transformation ya Simba imekamilika au bado? je Simba sasa inaendeshwa katika mfumo mpya au wa zamani (before transformation) tuanzie hapo
Simba inaendeshwa kwa mfumo mpya, ndio maana sasa tunaona mwekezaji ndie ana play role kubwa kwenye masuala ya timu, zile hisa nyingine 51% wanazosema ni za wapenzi na wanachama mpaka leo zipo tu, lakini haijulikani nani wengine wanamiliki hisa asilimia ngapi.
 
Mpira ni pesa sawa, lakini kuna mambo mengine licha ya uwekezaji yanahitaji bahati pia, kama kuchukua vikombe.
uwezi kuipata iyo bahati hata kama ipo kama una wachezaji wasio na viwango.
kwa mfano Simba kuifunga Al ahly kwa Mkapa ile ilikua ni bahati,lakini pia Simba kipindi icho wachezaji wa Simba walikua kwenye kiwango bora,so far bahati ikaangukia kwenye ubora.
Simba ya sasa kwa Al ahaly aifungwa tu bali itakatwakatwa vipande vidogo kama mishkaki.
 
Basi wachezaji ni wapumbavu, wachezaji ndo wanacheza na sio wenyeviti
 
Uwekezaji uwe mdogo au mkubwa, hauna uhusiano wa moja kwa moja na ushibdi wa timu..

Juzi kwenye EPL, Chelsea licha ya kusajili kwa pesa nyingi, lakini bado ikafungwa na Southampton iliyoko nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi, kuelewana wachezaji uwanjani [ chemistry ] ndio kila kitu.

Hebu sasa turudi mezani, je, performance ya Simba Sc uwanjani, imeathiriwa na makundi ya uchaguzi?
 
Simba inaendeshwa kwa mfumo mpya, ndio maana sasa tunaona mwekezaji ndie ana play role kubwa kwenye masuala ya timu, zile hisa nyingine 51% wanazosema ni za wapenzi na wanachama mpaka leo zipo tu, lakini haijulikani nani wengine wanamiliki hisa asilimia ngapi.
Kama ni hivyo basi huu mfumo mpya haujawa tiba au una sehemu inavuja
 
Basi wachezaji ni wapumbavu, wachezaji ndo wanacheza na sio wenyeviti
Naona kuna haja ya wachezaji wetu wa PL kuwa na elimu angalau kuishia kidato cha sita..
 
Yaani mkuu hadi leo unawaza kuchukuwa vikombe ni bahati?

Nio wonder!
Unadhani Guardiola mpaka leo nini kinamsumbua kushinda UCL licha ya kupita Bayern Munich yenye watu wa maana, na sasa yuko Man City yenye majembe ya kutosha?

Last season, Liverpool anafungwa mechi ya fainali ya UCL na Real Madrid licha ya kuupiga mwingi, unadhani kule kupoteza nafasi walizopata kulisababishwa na kitu gani?

Haya mambo hayataki kukurupuka dogo, tulia ujifunze kwa wakubwa zako.
 
Uchawi una nafasi katika mpira duniani. Sio Tz au Africa pekee.

Porto wameajiri mganga huko na yuko kwenye payroll ya timu.
Ni baada ya Benfica misimu iliyopita kuajiri mganga halafu wakachukua ubingwa.

Porto wakasema usitutanie. Ulaya hiyo.
 
Wajuzi wa mambo waufanyie uchunguzi, lakini na tabia zetu za kiswahili hasa majungu na fitna nazo ni tatizo ..
............ "lakini na tabia zetu za kiswahili hasa majungu na fitna nazo ni tatizo" ..

👆Huu ndiyo mtihani wa mpira wa bongo.
 
Uchawi una nafasi katika mpira duniani. Sio Tz au Africa pekee.

Porto wameajiri mganga huko na yuko kwenye payroll ya timu.
Ni baada ya Benfica misimu iliyopita kuajiri mganga halafu wakachukua ubingwa.

Porto wakasema usitutanie. Ulaya hiyo.
Hii kali[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom