Salaam..!!
Katika pita pita zangu mitaani nimekutana na maneno toka kwa wadau wa Simba Sc, hasa mashabiki na wanachama wake, wanaodai kwamba, uchaguzi wa Simba Sc kufanyika wakati ule [katikati ya msimu] yamechangia kuathiri uwezo wa timu uwanjani.
Binafsi napata mashaka na uzito wa madai hayo kwasababu moja kubwa, kwamba, timu ya Simba Sc kwasasa iko chini ya mwekezaji Mo, huyu ndie yupo "responsible" kwa mahitaji yote muhimu ya timu, kuanzia chakula, malazi, usafiri, usajili, mishahara ya wachezaji, na mengineyo.
Kwangu ningeyaona madai hayo [tetesi hizo] zina uzito endapo kama bado timu ya Simba Sc ingekuwa na mfumo uliopita kabla ya ujio wa mwekezaji, ambapo watu binafsi walikuwa wakisajili wachezaji wao, kuwalipa mishahara, na kulazimisha kocha mkuu awapange wachezaji wao, hata kama hawana uwezo uwanjani lengo likiwa kuwatafutia masoko nje kupitia Simba Sc.
Kwa akili ya kawaida, ungetambua kwamba, hawa wachezaji walikuwa na uwezo wa kuwasikiliza mabosi wao waliowasajili na kuwalipa mishahara, pale ambapo mambo binafsi ya mabosi hao hayakwenda vizuri ndani ya klabu, ikiwemo kushindwa uchaguzi, hivyo kuwaambia wachezaji wao wacheze chini ya kiwango ili kuwakomoa wapinzani wao walioshinda uchaguzi.
Lakini leo Mo anatoa kila kitu, hao watu waliopo nje ya timu [kama kweli wapo] wenye uwezo wa kuwashawishi wachezaji kucheza chini ya kiwango na kuathiri matokeo ya timu uwanjani ni wakina nani? na iweje wawe na nguvu kubwa kiasi hicho ya ushawishi kwa wachezaji [ kama wapo]?
Yangu ni hayo tu ...