Je, TFF ina Wataalam wa kupanga ratiba ya Ligi? Ligi inaenda ukingoni timu moja ina michezo 28 na nyingine 24

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Mpaka leo Ligi ipo ukingoni halafu timu moja ina michezo 28 na nyingine 24, hivi kweli bado tuna Wataalam wakupanga ratiba ya Ligi?

Hebu fikria,...Kuna team hazijakutana tangu ligi ianze.

Najiulza mbona siku hizi wasomi ni wengi kwanini hali inakuwa hivyo? Je, wanakwepaje upangaji wa matokeo na rushwa?

Hebu tazama Ligi nyingine ambazo zipo ukingoni hazijaachana. Kama mambo yapo hivi kweli Vyuo Vikuu tunaenda kufanya nini?
 
Misri Al ahly kacheza mechi 14 wengine 17, South-Mamelod mechi 22 wengine 24, nae Horoya mechi 9 wengine 15, Simba 24, Namungo 22 na wengine 28, 27. Kwa hiyo ukiangalia hapo timu zinazoshiriki kimataifa ndio zinakuwa na mechi pungufu.

Kwa hiyo kama ni upangaji wa matokeo sababu ya upungufu wa mechi basi laumu vyama vyote vya Afrika.
 
Mnajitetea Sana, Swali Ni Kwa Nini Kuna Team Mpaka Ssa Hazijakutana Hata Kwenye Mzunguko Wa Kwanza? Huu Ndio Upangaji Mzuri Wa Ratiba ya League?
 
Mnajitetea Sana, Swali Ni Kwa Nini Kuna Team Mpaka Ssa Hazijakutana Hata Kwenye Mzunguko Wa Kwanza? Huu Ndio Upangaji Mzuri Wa Ratiba ya League?
Tunawalaumu tu Tff ila ni ngumu kupangia klabu ratiba yenye mtiririko mzuri kwa viwanja hivi na ambavyo havimilikiwi na klabu. Mara visimamishwe vikarabatiwe mara mkutano wa kisiasa ufanyike sasa hapo utapataje ratiba nzuri?
 
Tunawalaumu tu Tff ila ni ngumu kupangia klabu ratiba yenye mtiririko mzuri kwa viwanja hivi na ambavyo havimilikiwi na klabu. Mara visimamishwe vikarabatiwe mara mkutano wa kisiasa ufanyike sasa hapo utapataje ratiba nzuri?
Viporo kila ligi vipo lakini kwa tanzania ni vya kushangaza....viporo kuwa vinne sawa kabisa lakini sio mpka viwe 8 au viporo mpka ligi inakaribia kuisha timu moja haichezi mechi na timu nyingine mechi mbili.
 
Bila shaka TFF wapo watalamu walio soma UDSM
 
Kwa kifupi timu za zinazoshiriki champions league ni vigumu kuenda na ratiba ya ligi ya ndani tofauti na ulaya, logisticaly tuko tofauti sana, kama una mechi kinshasa unahitaji utoke siku tano au nne kabla, hakuna jinsi ya kufika kinshasa bila kupitia ethiopia. Sasa unataka simba wiki hiyo hiyo ikacheze na namungo mtwara then wakacgeze na vita kinshasa? Kuna trip ya kwenda misri ilibidi wapitie dubai. Ukiwa upande wa uto unaweza sema kila kitu unaonewa, bahati mbaya kipindi mko kileleni hamkuliona hili.
 
Viporo kila ligi vipo lakini kwa tanzania ni vya kushangaza....viporo kuwa vinne sawa kabisa lakini sio mpka viwe 8 au viporo mpka ligi inakaribia kuisha timu moja haichezi mechi na timu nyingine mechi mbili.
Timu gani ina vipolo nane mzee?
 
Alafu eti msimu huu Namungo na Simba hazijakutana?
 
Ligi zote duniani zinakuwa na viporo kuanzia 2 mpka 4 sio tatizo kwa timu zinashiriki michuano mingi..mf Man city ina Emirate FA, Carabao Cup, EPL, CL timu kama hii haiwezi kukosa viporo...na timu yoyote inayochukua CL kuna wakati ligi inaendelea unakuta wanatakiwa kushiriki klabu bingwa ya dunia wakati huo ligi ya ndani hazisimami
 
Wanayanga mshageukia wapangaji wa ligi?? mbona wakati mnaongoza ligi hii kitu haikuwepo??
 
Kila timu ikijitahidi kushinda mechi zake huwez sikia malalamiko yahivi
 
Mnajitetea Sana, Swali Ni Kwa Nini Kuna Team Mpaka Ssa Hazijakutana Hata Kwenye Mzunguko Wa Kwanza? Huu Ndio Upangaji Mzuri Wa Ratiba ya League??
Kwa hiyo baada ya kuona ubingwa umeota mbawa ndio mmeanza kutafuta kichaka cha kujificha Sio ? Yanga mna shida sana huwa mnapoteza muda sana kutafuta vijisababu vya kijingajinga kujustfy failures zenu na timu lenu bovu. Na kwa ujinga wenu wa viwango vya Phd usajili ujao nao mtapangishwa mafoleni ya kwenda kupokea magalasa tena airport
 
Na mimi nilitaka kusema hili asilonganishe na ulaya( nako viporo vipo) ila sio kwa kiwango cha huku kwasababu ya changamoto za lojistiki. Anayesafiri kwa ndege binafsi ana nafasi zaidi ya kujipangia ratiba vizur kuliko ndege ya jumuiya. Nilishangaa sana connections za DRC hapo pembeni ya kigoma mpk waende Addis au kwenda hapo Cairo eti wamepitia Dxb
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…