Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Hakuna ramani za 10,000 Acha kudanganya watu.

Afu mamlaka za kusimamia professionalism sijui zinafanya nini
 
Tofali 2800 zinaweza kutosha au kutotosha kujenga nyumba ya vyumba 3 inategemea
1. aina ya nyumba
2.Uwanja jinsi ulivyo (una slop au hauna)
3.Muonekano wa paa hapa kuna
*Pitched roof (paa la kuonekana kama zilivyo
nyingi)
*Hidden roof (paa lisilooneka)
*Lean to roof (paa la upande mmoja)

N:B wewe ndio utaamua zitoshe au zisitoshe kutokana na unachokihitaji kwenye nyumba yako
 
Doooo, UVIMO. Kweli ramani kama hiyo mnajinadi? Dirisha la choo linakuwa ndani. Si umeharibu biashara yako. Kwanini mtu asi download ramani yake kama ramani zenyewe ndiyo hizo.
Maana ukiwa na App ya Pinterest kuna ramani za kila aina. Ni kweli tofali 2800 zinatosha nyumba anayoitaka. Labda tu kiwanja kiwe na slope kali.
 
Uko sahihi kabisa, Safi sana.
 
Kkoo kuna mtu kamwaga chini anauza 20000 na makadilio yake kabisaa ya ujenzi
Yani kwa wewe unaesema mtu kamwaga kariakoo binafsi sipingi, kila mtu na namna anavyoona anaweza kupata wateja. Ila kuna jamaa humu anasema kuna watu unawapa wazo lako kisha wanakuchorea from zero sketching kwa Tsh elfu ishirini. Hiyo naikataa, kazi ya kuchora seriously haiishi ndani ya masaa mawaili au matatu, ni siku nzima au mpaka siku tatu depending na mchoraji na complications za mteja. Hakuna mtu atafanya kwa elfu ishirini, ila kwa hizo zilizochorwa kisha zinamwagwa na kuuzwa inawezekana kwasababu .............
 
Kuna wengine wanamaliza kujenga alafu wanakuja humu kuomba jinsi ya kuziba ufa.

Nakuunga mkono, swala la utuliwaji wa wataalamu Tz bado ni shida sana.
Ndio mkuu. Niliwahi kuwa kwenye magroup ya ujenzi facebook huko
Ilikua ni kero watu wanakuja na matatizo na maswali yaleyale yanayojibiwa kila siku, mpaka niliamua kujitoa. Maana ilifikia kuwa kero, watu hawajifunzi.
Hakunaga shida kwenye kupita shortcut kwa njia unayoijua vizuri, shida ni pale unapojaribu kubahatisha
 
Hao wa stationery wanakua na hizo program kwaajili ya kufungulia ‘project files’ za michoro tu na kusaidia kuSave. Hasa Ukienda chuo Ardhi pale yes wapo. Lakini sio kwamba wanachora na kama ikitokea labda mmoja,
But nitakachokupinga hapo ni kusema wanachora kwa hiyo elfu kumi, its a big no, hizo sanasana ni kazi za watu (ma architect) ziliachwa wakati wa kuprint labda wao ndio wanaziuza kwa bei hiyo kama ni kweli.
 
kuzingatia baadhi ya vitu kama north direction, access road, type of soil, water table na dampness ya eneo husika n.k.
Kwa hiyo unakuja site na vifaa vya kupima water table na area dampness ?

Na vifaa vyenu vinapima dampness hata kipindi cha kiangazi kikali ?
 

Kaka kuchora sio kazi kabisa ile ni application tu so mzoefu wa kuchora ni fasta sana mkuu
 
Swala la msingi ni kwamba ramani imepatikana bila kujali ni kwa namna gani
 
Tena tofari hizo ni nyingi sana, hata vyumba kadhaa vinaweza kua self contained. Hata tofari 2500 zinaweza kufanya mambo.
 
ROOM MOJA NI WASTANI WA TOFALI NZITO 400, os nusu ya hizo zitafaa kumaliza room3 na nusu ya zilizobakia zinamaliza sebule na jiko na zilizobakia choo moja na store.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…