Je TRC/SGR inahujumiwa ama inajihujumu!

Je TRC/SGR inahujumiwa ama inajihujumu!

20241106_160657.jpg
 
Kama usafiri wa treni ya umeme ungefanya Kazi kwa ufanisi hasa kwenye hii njia ya Dar Dodoma ingekuwa ni mkombozi na mapinduzi makubwa ya usafiri wa haraka Tanganyika.

Nimemsikia mkurugenzi mkuu wa TRC alilalamika kwamba wanahujumiwa na wanawajua kwa majina wahujumu wote.. Hapa inashangaza kidogo.

1. Wahujumu wanajulikana mpaka majina lakini hawajakamatwa mkurugenzi anakuja kulalama mitandaoni

2. Uhujumu unaofanywa ni wa kukata waya za umeme kwenye njia ya reli🥺🥺 hapa nadhani tumeongopewa.. Ule umeme ni HT huyo anaweza kukata nyaya zake akabaki salama anahitaji moyo wa jiwe, uthubutu na vifaa vya aina yake.

Kuna tatizo kubwa SGR na hawataki kuliweka wazi

Jumapili iliyopita tulipata safari ya dharura kwenda Dodoma tukitokea Dar . Tukaamua tuondoke na SGR lakini mara tukapata taarifa kuwa imezimika njiani zaidi ya masaa matano.. Ile ya kurudi Dar

Kwa kuhofia hizo shida tukaamua kuondoka na gari binafsi.. Tulikuwa jumla sita. Tukasafiri salama na Jumatatu tukafanya kilichotupeleka Dodoma na kumaliza nusu.

Watatu kati yetu wakaamua kurudi Dar mchana ile na sisi wengine tukabaki

Niliyoyaona SGR Dodoma


Tulifika pale saa sita kuwahi treni ya saa nane itakayofika Dar saa 11 lakini tukawa tumeichelewa. Lakini customer care tuliyokutana nayo kuanzia eneo la kupekuliwa mpaka kwenye ticket ni mbovu sana

Wafanyakazi was SGR ni washamba na wanajiona wao ndo kila kitu wana dharau na ni watemi..

Mtandao wao wa kukata ticket ulikuwa unasumbua lakini hawakujali hata kutoa taarifa..Utaratibu pia ni mbovu sana.

Askari waliopewa kandarasi ya usalama pale ni kampuni ya SUMA JKT aisee walikuwa na utemi na mabavu kwa abiria wengi bila sababu.. Yaani fuata wanachosema basi .. No argument!

RUSHWA

Nilishuhudia askari wa SUMA JKT wakiingia ndani kwa wakata ticket na vimemo kisha wakatoka na tickets.. Kuna watu hawapangi foleni pale..wanawatumia hao askari

Ubovu wa treni zenyewe

Kwakuwa tulikosa ile ya saa nane hivyo tulikata ile ya saa 11 kufika saa moja usiku.. Hivyo ikabidi tuzubaezbae mitaa hiyo hiyo kuliko kwenda na kurudi.

Soma Pia: Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Ni katikati kuzubaa huko ndio nikakuta vijana wa boda pale nje wanasema . .. Na hili la leo sijui kama litafika Dar bila kukata moto.

Ndugu zetu waliondoka saa kumi na moja lakini walifika Dar karibia saa sita usiku.. Goma lilikata moto njiani na hitilafu haikuwa umeme bali engine. Utabiri wa boda ukatimia

Treni zilizoletwa zina walakini mkubwa.. Sasa hapa anayehujumu ni nani?
Haya masuala ya cheap price kwa vichwa vya treni yanaweza kutukost double, TUAGIZE VICHWA KUTOKA GERMAN, tutaachana na masumbufu haya! / viwe chini ya mtengenezaji mkorea mwenyewe kwa miezi kadhaa.
 
Back
Top Bottom