Je, trillioni 10 zinatoka wapi kukamilisha trillioni 34 za Bajeti?

Je, trillioni 10 zinatoka wapi kukamilisha trillioni 34 za Bajeti?

Dullah07

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2017
Posts
220
Reaction score
475
Habari wanachama wa JF,

Swali langu mimi ni kuwa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 ni trillioni 34 na pointi kadhaa sasa najiuliza hadi utawala wa Hayati Magufuli R.I.P, makusanyo ya kodi kwa mwezi ni trillioni 2 ambako ndani ya mwaka mzima ni trillion 24 tena hapo bila kushuka kwa makusanyo katika miezi yote 12. Sasa je, katika trillioni 34 ya bajeti kuna upungufu wa trillioni 10 kutoka katika makusanyo.

Je, hizo 10 trillioni zinatoka wapi kuja kukamilisha 34 trillioni?
 
Sasa hapo tunapunguza deni la Taifa au tunaongeza maana naona tutazidi kukopa
 
Hili hata sio fikirishi, jibu ni rahisi tu mabeberu yatajazilishia, na uongo pia kutumika Kama kawaida ya nchi yetu chini ya CCM
inabidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama kuwalipa chadema ruzuku ambayo wanazurura tu nakujilipa maposho ruzuku ikiingia tu mbowe anaanza ziara mpaka ziishe
 
Sasa hapo tunapunguza deni la taifa au tunaongeza maana naona tutazidi kukopa
Deni linalipwa huku tukiendelea kukopa. Ndio maana kwenye budget hiyo hiyo, kutoka kwenye makusanyo ya TRA kuna fungu la kulipa madeni.
 
Kuna kama 4 tr zitakopwa na nyingine misaada
 
Serikal inabid kufungua vyanzo vpya vya mapato na kuongeza wigo wa ukusanyaj kodi ikiwa moja wapo km kodi za lain za simu
 
Jumong atatuua huyu sasa, kwanza anaendelea kuzungukwa na majambazi makuu katika serikali yake... Raisi yeyote lazima aje na team yake inayomtii... fikiria mtu kama Maderu kaja na slogan za kuibia raia kwenye shughuli zao kuu vocha,Luku n.k.

Unatgemea pesa za wanachi kukuza Taifa huku tukiaminishwa taifa ni Tajiri bila kugawa gawio kwa raia... Serikali yenyewe bajeti za matumizi ni kubwa kuliko ya Maendeleo pumbavu sana hawa mashetwain
 
Nchi za africa bajeti zao huwa ni tegemezi - bila wahisani nchi hizi hamna kitu, zinaweza kuwa zinasonga kwa mwendo wa kinyonga - na ndiyo maana tumeambiwa tuanze kushapisha data za Covid kama tunahitaji misaada kufidia bajeti yetu.

Kwa mfano kwenye hiyo bajeti ya 34 trillion, 60% ni Operational costs na 40% ni fedha za maendeleo. sasa hapo kwenye maendeleo ndiyo kimbembe kilipo - bila wahisani mzee inabakia bla bla nyingii.

Way forward: Hadi hapo tutakapojifunza kutumia ardhi yetu vizuri ndipo tutaacha utegemezi - nchi yenye mapori na ardhi yenye rutuba ya kumwaga tunashindwa kuilisha dunia?
 
inabidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama kuwalipa chadema ruzuku ambayo wanazurura tu nakujilipa maposho ruzuku ikiingia tu mbowe anaanza ziara mpaka ziishe
Sawa kabisa na kule kutembea na loba la hela na kugawa kwa wanyonge naona hakuna tena lazima lipungue tu.
 
Kweli nimeamini kuwa JF ndio kisima cha maarifa.
 
inabidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama kuwalipa chadema ruzuku ambayo wanazurura tu nakujilipa maposho ruzuku ikiingia tu mbowe anaanza ziara mpaka ziishe

Akili za kiwango cha kutawala mkeo na watoti tu ndio hizi!! Kwa hiyo Mbowe akiacha ziara basi matumizi ya serikali yasiyo ya lazima tayari yamedhibitiwa!!

Ondoa hilo ji.vi kwenye hilo fuvu na utafikiria mambo ya maana.
 
Kwanza hata hayo makusanyo hayawezi kufika hiyo trilioni 2 kwa mwezi hivyo hiyo nakisi katika bajeti ni zaidi ya hiyo trilioni 10 ambayo ili kuipata lazima wakope na pia kuomba kupewa misaada.
 
Nadhani wameongeza wigo wa mapato. Kwa mfano kwenye miamala ya fedha wameongeza kodi kutegemea na muamala, kodi ya majengo iko kwenye luku hivyo hata mpangaji anailipia na nadhani pia watategemea ufadhili kutoka kwa mabeberu. Sasa hivi si tumewakumbatia!!!! Nchi hii inachekesha sana!!!
 
Back
Top Bottom