SoC01 Je, tufumbe macho au tutafute suluhu la machinga?

SoC01 Je, tufumbe macho au tutafute suluhu la machinga?

Stories of Change - 2021 Competition

msani

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Posts
1,801
Reaction score
1,191
JE, TUFUMBE MACHO AU TUTAFUTE SULUHU LA MACHINGA?

Labda niseme kwamba mimi ni machinga kwa style yangu ya biashara, na niseme wazi kwamba nimefanya umachinga tangu nikiwa shule ya msingi au niseme kabla sijaanza shule ya msingi.

Maisha yangu, ambayo ni maisha ya machinga wengi, yalikuwa ni kukimbizana na mgambo wa jiji la Mwanza na aidha kukamatwa au kuharibiwa bidhaa zangu zikiwemo ndizi nilizokuwa nauza na machungwa yangu.

Baada ya msuguano huu serikali imekuwa ikijenga masoko au kutenga maeneo kwa ajili ya machinga sisi lakini yasiyo na uasili wetu. Machinga tunafanya biashara kuwafuata wateja na wengi wetu ni kwa ajili ya kula. Sasa maeneo mengi ambayo yamekuwa yanatwengwa na serikali sio rafiki kwa sababu wateja hawafiki maeneo hayo kwa sababu ya umbali. Chukulia upo Mwanza mjini halafu mnaambiwa mhamie Sabasaba na wakati sisi tunavizia wanaotoka makazini ili tuwauzie bidhaa zetu, hii inafanya turejee maeneo hayo hayo kila siku.

DSM walijenga soko la Machinga Complex na kule Mbeya Soko la Mwanjelwa, lakini ujenzi na muuondo wake wa kibiashara sio rafiki yaani sio asili ya machinga. Machinga wengi ni wale ambao kwao kwa siku wanatafuta 5,000 au 10,000 lakini kule juu nani anafika kwenda kununua bidhaa za machinga na gharama ziko juu.

Tumerudia kosa kwenye Soko la Kisutu na Soko la Dodoma. Kwenye biashara za Real Estate ambapo masoko haya yanaangukia kuna kitu kinaitwa PAYBACK PERIOD, yaani muda ambapo mwekezaji anataka kurejesha fedha yake ya uwekezaji na aanze kupata faida. Wakti wa uzinduzi wa Soko la Kisutu uliofanywa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli(R.I.P) ilielezwa kuwa Payback periodi ni kati ya miaka 8-10, hili lilinishtua kidogo kwa sababu ilimaanisha kodi za kupanga ndani ya soko zingekuwa kubwa na kuwazuia wengi kwenda kupanga maeneo hayo. Kwa kawaida na ukizingatia ile ni huduma kwa jamii na kwa ajili ya kuwapunguza machinga mitaani basi ilipaswa iwe kuanzia miaka 25 hadi 30. Hii tafisiri yake wafanyabishara wangelipishwa kodi ya wastani ambayo wangehimili kulingana na biashara zao na ingewavuta wengi kuweka biashara zao humo ndani. Kosa kama hili limefanywa kwenye Stendi ya Magufuli pale Mbezi na Dodoma. Pamoja na kwamba kodi za Stendi ya Magufuli ziliamuliwa kwa mnada lakini hakukuwa na uhalisia ndio maana hadi leo maeneo mengi yapo wazi.

TUFANYE NINI?

Baada ya kuona hizi changamoto nyingi za machinga, mimi niliwaza jambo kwamba hatupaswi kuwahamisha wamachinga kutoka sehemu walipo wateja.

Rais Magufuli aliwahi kusema kwamba “Msiwaondoe machinga kama bado hamna sehemu ya kuwapeleka na wasipelekwe sehemu ambako hakuna biashara”

Naunga mkono kauli hii ya aliyekuwa Rais wetu.
Serikali ina wajibu wa kutumia kodi zetu kutatua matatizo yetu.
Nashauri serikali iwezeshe wawekezaji, wakope kupitia benki, na baada ya hapo ifanye acquisition(nadhani ni kununua) ya ardhi maeneo ya makazi ya watu na kisha ijengwe miundo mbinu ambayo itawaweka machinga maeneo hayo.

Mfano: Eneo la Manzese liwekwe soko pale ambalo litakuwa la wazi ambapo zitajengwa meza za kisasa kwa muundo ule ule wa machinga halafu hilo eneo likachukuliwa leseni moja na TIN Number moja. Baa day hapo machinga watalipia gharama kidogo labda 500 au 1000 kwa siku, na hapo wasilipie Tena ile 20,000 kwa mwaka bali hiyo hela anayolipa kwa mwezi ikatwe asilimia ilipwe serikalini kama kodi. Mfano Machinga ikitengwa shilingi 100 kwenye kodi yake atakuwa amelipia 36,000 kwa mwaka badala ya 20,000 kwa mwaka na watakuwa wanafanya biashara kwenye mazingira ya kwao ya asili.

Tunataka kufanya biashara lakini najua huku kujazana barabarani sio kuzuri na najua ipo siku mtatumia nguvu kutuondoa kama msipopata njia nzuri ya suluhu ya hili tatizo.
Pesa zetu za kodi zitumike kutatua matatizo yetu kwa ubia na sekta binafsi. Baadhi ya maeneo yalasimishwe mfano karume pale dsm. Kuna mambo tutayazoea taratibu bila nguvu na moja wapo ni soko la Machinga Complex, litajaa lakini sio kwa kutumia nguvu.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom