Je tuibe pesa kwasababu ofisi au kampuni ni ya mzungu?

Brainy Chick

Member
Joined
Mar 9, 2013
Posts
64
Reaction score
21
Habari wana business forum!!

Kuna jambo linanitatiza na ningependa kupata maoni yenu! Mimi ni mfanyakazi wa kampuni fulani hapa nchini na baadhi ya wafanyakazi wenzangu wamekuwa na tendency ya kumuibia muajiri. Nikiwaconfront wanasema mimi ni mnoko na kwamba hawa "wazungu" hawana faida yoyote kwetu. Si kwamba mimi siwezi kuyafanya wanayoyafanya bali ni kwamba mimi si mtu wa aina hiyo. Je niendelee tu kutazama wakifanya ubadhirifu, ukizingatia ofisi yetu inatoa huduma ya kijamii kwa hiyo kwa njia moja au nyingine tuta-affect hao wanajamii ambao ndio walengwa wa hii kampuni/shirika!!
 
Kama wanaiba na wewe unajua bila kuchukua hatua yoyote basi na wewe ni mwizi pia,haiwezekani unashuhudia wizi na unakaa kimya.
 
Bado natafakari hatua ya kuchukua kwasababu hawa ni watu kama mimi na wanamsururu wa watu unaowategemea. Kwa sasa nimeshawaonyesha stand yangu juu ya suala hili.
 
Wakati unatafakari wao wanazidi kuhujumu misaada ambayo ilitakiwa kufaidisha jamii nzima mnayoihudumia,kama wana watu wanawategemea hilo halikuhusu maana hapo mpo kazini na mambo ya nyumbani kwao hayakuhusu,fuata sheria za kazi na utafanikiwa.
 
Usithubutu kufanya kitendo cha kuvunja sheria eti kwa sababu wengine wanavunja.
Acha waibe wakikamatwa watajua thamani ya wizi ni nini, but hakikisha mikono yako haihusiki na haingii hatianiani!
 
Na hili ndo moja ya sababu kuu kabisa ya kwa nini Wawekezaji wengi wanakuja na wafanya kazi wao, kwa Kifupi Watanzania hawaamini kabisa, Unakuta hata kwenye Mahoteli ya Kitalii watanzania wanaiba sana kuanzia Vijiko, Glass, Mashuka na kazalika, kuna siku nimeenda kwa jamaa mmoja anaye fanya kazi hoteli moja kubwa kabisa, ya kitalii kwenye mbuga za Wanayama jamaa kila anacho tumia ni cha hiyo hoteli kunazia Mataulo, glass, Vikombe, Mashuka na vyote vina chata/nembo ya Hoteli,

Utaona kwamba makampuni mengi sana ya kizungu na hata ya wahindi wanatumia watu wa nje kwa zile nafasi nyeti kama ya Uhasibu, Store na kazalika na zile za kawaida kama Kufagia, Udreva na walinzi hapo ndo uwanja wa Wabongo kujinafasi, na moja ya sababu kuu ni wizi,

So kuendelea kuibia Wawekezaji hakuwakomo wao bali ni watzania Kujikomoa wenyewe kwani jamaa wanapata sababu za kuhalalisha kuajili wageni

Utaona hata Mashirika/NGOs nyingi za kimataifa zinazo operate na Tanzania, wakurugenzi wengi ni wakutoka Kenya, Uganda na kwingineko na baadhi ya Mashirika polisi yao ni kwamba Shirika likiweka Ofisi mathalani Tanzania basi Mkuu wa shirika hilo kwa upande wa Tanzania lazima awe Mtanzania, Ila mashirika Mengi kwa Upande wa Tanzania imeshindikana kabisa, ingawa kwenye ofisi za hayo hayo mashirika Upande wa Uganda, Rwanda, Kenya, Zambia na kwingineko zinaongozwa na Raia wa hapo, Ila kwa Bongo imeshindikana kisa Wizi na ufisadi,
 
:nono::nono::nono::nono:

Labda kama ni kwenye migodi ya dhahabu....nchi kama nchi inaibiwa sana na hawa wawekezaji
 
Tabia ya kuiba maofisini/ kuiba kwa kalamu inaelekea kuwa ya kawaida kwa watanzania hasa vijana. In fact huu ni ujambazi kama ujambazi mwingine. Hii ni tabia ya hatari manake inaua ubunifu, inakatisha tamaa wafadhili na wadau wa maendeleo na kikubwa kabisa ni kwamba ni dhambi na inaleta laana kwa wanaoifanya. Kama Mungu amekupa neema ya kupata huo ufahamu kwamba kuchota pesa ni tabia mbaya endelea hivyo hivyo. Na usiogope kutoa taarifa unapoona mtu anaiba. Jamani tutende haki ili taifa letu lipone. Tutende haki hata kwa gharama ya kuitwa wanafiki, wanoko n.k.
 
Ibeni tu hadi kampuni/shirika/ngo ife mrudi kijiweni mkapige umbeya

Mkuu,

Nimependa sana comment yako.Watu hawana muda ya kufanya kazi kwa ufanisi ili waboreshe maslahi yao wanachowaza ni kuiba na mwishowe shirika/coy ife waanze tena kutembeza CV!
 
Habari wana business forum!!

Kuna jambo linanitatiza na ningependa kupata maoni yenu! Mimi ni mfanyakazi wa kampuni fulani hapa nchini na baadhi ya wafanyakazi wenzangu wamekuwa na tendency ya kumuibia muajiri. Nikiwaconfront wanasema mimi ni mnoko na kwamba hawa "wazungu" hawana faida yoyote kwetu. Si kwamba mimi siwezi kuyafanya wanayoyafanya bali ni kwamba mimi si mtu wa aina hiyo. Je niendelee tu kutazama wakifanya ubadhirifu, ukizingatia ofisi yetu inatoa huduma ya kijamii kwa hiyo kwa njia moja au nyingine tuta-affect hao wanajamii ambao ndio walengwa wa hii kampuni/shirika!!

Brainy Chick nakushauri pamoja na kujaribu kuwaelimisha wafanyakazi wenzio wadokozi athari za kile wanachokifanya, itasaidia sana kama ukizungumza na mwajiri namna anavyoibiwa bila kutaja majina yao, ili mwajiri aweke mifumo ambayo itadhibiti wizi huo! Kama mwajiri hatakuwa na ubunifu wa kuweka mifumo ya kudhibiti wizi huo kampuni itashindwa kutimiza malengo yake! Ukiona wizi unaendelea na mwajiri hachukui hatua jiandae kwa lolote hasa kama mwishowe wizi utafanya kampuni ifungwe. Jukumu la wewe kuwa-confront wafanyakazi wenzio ni kujitoa muhanga ambako hakuna tija. Hicho unachofanya ni risk kubwa sana na ni hatari sana kwa jamii ya Tanzania ya leo ambayo watu wameshaumizwa sana na ufisadi! Ni kama kutaka kuwafukuza fisi kwenye mzoga. They will kill you!! Kama nafasi yako hapo kazini inahusika na usimamizi wa hao wafanyakazi wezi timiza wajibu wako kuwaonya na ikibidi kuwatimua, hapo hata kama ukifanyiwa mbaya ni haki yako maana utakuwa umetimiza wajibu wako!
 
yawezekana wanaiba kwasababu kile wanachopewa hakikidhi mahitaji yao. si kwamba wafanyakzi wanapenda kuiba, lazima kuna sababu nyingi zinazopelekea wafanye vitendo hivyo.
 
Brainy Chick nakushauri pamoja na kujaribu kuwaelimisha wafanyakazi wenzio wadokozi athari za kile wanachokifanya, itasaidia sana kama ukizungumza na mwajiri namna anavyoibiwa bila kutaja majina yao, ili mwajiri aweke mifumo ambayo itadhibiti wizi huo! Kama mwajiri hatakuwa na ubunifu wa kuweka mifumo ya kudhibiti wizi huo kampuni itashindwa kutimiza malengo yake! Ukiona wizi unaendelea na mwajiri hachukui hatua jiandae kwa lolote hasa kama mwishowe wizi utafanya kampuni ifungwe. Jukumu la wewe kuwa-confront wafanyakazi wenzio ni kujitoa muhanga ambako hakuna tija. Hicho unachofanya ni risk kubwa sana na ni hatari sana kwa jamii ya Tanzania ya leo ambayo watu wameshaumizwa sana na ufisadi! Ni kama kutaka kuwafukuza fisi kwenye mzoga. They will kill you!! Kama nafasi yako hapo kazini inahusika na usimamizi wa hao wafanyakazi wezi timiza wajibu wako kuwaonya na ikibidi kuwatimua, hapo hata kama ukifanyiwa mbaya ni haki yako maana utakuwa umetimiza wajibu wako!

Mzee,
Kukaa kimya kuliwahi kutugharimu sana siku moja kazini kwetu AR, lililpofumuka lilikula wote, wasio na walio,lakini pia siku nyingune ilitugharimu sana tulipojaribu kufanya kwa usahihi kile tunachopaswa kufanya, kumbe ndani ya mchezo wa wenzetu wale kuna mkono wa bosi wetu, hatari yake ilikuwa kubwa. Visasi hadi home.

Njia nzuri ni kuwakanya na kuwaambia ukweli juu ya madhara ya vitendo vyao. Vinginevyo kama utawajibika kwa vitendo vyao, huna njia isipokuwa kuwatimua. Ila uwatimue kama na wewe ni msafi.
 
Back
Top Bottom