Je, tukemee udini, ukanda na ukabila au? Je, neno Sukuma Gang si neno la kibaguzi? Mnaonaje tukiungana kukemea ubaguzi wowote kwa jina lolote?

Je, tukemee udini, ukanda na ukabila au? Je, neno Sukuma Gang si neno la kibaguzi? Mnaonaje tukiungana kukemea ubaguzi wowote kwa jina lolote?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala hizi za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hizileta kwa mfumo wa swali fikirishi na mimi kutoa tuu maoni yangu lakini kukupa wewe msomaji fursa ya kufikiri, kushauri na kutoa majibu unayoona yanafaa.

Swali la leo ni kuhusu kuibuka na kuchepua kwa viji sentiments vya viashiria vya ubaguzi wa udini, ukanda na ukabila, sasa jee ni tuunganishe nguvu kukemea au tuache tuu ukiisha ota na kukomaa ndipo tuukate?. Ubaguzi huu wa kisasa unafanywa kwa viji neno neno vya kibaguzi, je neno Sukuma Gang, sio neno la kibaguzi?. ni neno tuu la kawaida tuliache au ni neno la kibaguzi linalostahili kukemewa?. Je mnaonaje kama Watanzania tukiungana kukemea vijineno neno vyenye viashiria vya Ubaguzi wa aina yowote kwa jina lolote?

Nimeileta hoja hii kufuatia as days goes by, hizi issues za hii kitu inayoitwa Sukuma Gang is escalating to the point of unbecoming!. Sukuma gang ni itikadi siyo kabila
Sukuma gang ni itikadi liyoasisiwa na Magufuli inayoamini katika ukatili unaohusisha matusi, utekaji, uporaji, mauaji na uonevu.
The Mkuu Sexless , kwanza nikupongeze kuileta hoja hii, pili japo ni kweli neno Sukuma Gang ni itikadi tuu, lakini si kweli kuwa iliasisiwa na Magufuli!. Tumwacheni Magufuli apumzike kwa amani!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Neno Sukuma Gang ni a fictitious Group that doesn't exist in reality lililobiniwa na yule Kigogo wa Twitter na watu wajinga wajinga wenye akili fupi wakaamini hili kundi ni kweli lipo!. Kiukweli kabisa Sukuma Gang sio kundi la kweli, halipo popote and don't exist anywhere in reality except ndani ya vichwa vya watu waliofilisika kisiasa!
Kwahiyo itikadi hii isihusishwe na kabila la Wasukuma. Mfano, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ndugu Sabaya yeye ni Sukuma gang lakini siyo Msukuma. Wengine ni Polepole, Ndugai, Bashiru, Mnyeti, Happi, Kabudi, n.k.
Pia sii kweli! bali baada ya Kigogo wa Twitter kuliasisi kundi hili fictitious, akatumia nguvu kubwa kulifanyia indoctrination kuwa hili kundi does real exist, hivyo wale watu wa Magufuli na watu wote wanaomsupport Magufuli wakawa pointed kuwa ni members wa Sukuma Gang, hata mimi ni Msukuma, na namsupport Magufuli na sio Sukuma Gang!
Lakini wapo Wasukuma ambao pia ni wafuasi watiifu wa itikadi hii ya sukuma gang. Sina haja ya kuwataja.
Hakuna kitu kama hiki, ila kwa vile indoctrination ya existence ya uwepo wa kundi hili imefanyika na watu wenye akili fupi waliofilisika kisiasa wakaamini', kama na wewe unaamini kuwa kundi la Sukuma Gang kweli lipo and does exist in reality, ujijue ni akili fupi and muflis kisiasa kama wale muflis wengine wote wanaoamini ujinga huu!
Nimeandika haya ili kuondoa dhana inayotaka kujengwa na baadhi ya watu ama kwa upotoshaji wa makusudi au kwa bahati mbaya kuwa kuwachukia wafuasi wa Sukuma gang ni kuchukia Wasukuma. Hili siyo jambo zuri na kufanya hivyo ni kupanda mbegu ya ukabila.
Hapa nakuunga mkono!
Mm Sexless mwandishi wa uzi huu nawachukia Sukuma gang na muasisi wao ingawa nami ni Msukuma.
Kumchukia mtu yoyote kwasababu yoyote sio jambo jema! Dini zinatufunza hata adui mpende!. Hivyo it's not right kumchukia mtu yoyote!

Japo hii shana ya the existence of the Sukuma Gang ni dhana tuu, na the Sukuma Gang ni just a fictitious Group that doesn't exist in reality, lakini kufuatia indoctrination iliyofanywa na yule Kigogo wa Twitter, watu wenye akili ndogo, akili fupi na waliofilisika ki fikra, wakaamini, hivyo chuki dhidi ya Wasukuma is real!. Hili sio jambo jema!.

Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa Tanzania kuliko makabila yote, zikitokea nafasi zozote za uongozi, na watu wote wako huru kugombea, obviously Wasukuma pia lazima watakuwepo.

Kulitokea nafasi fulani za uongozi ndani chama fulani, wakajitokeza wagombea 186 kugombea nafasi 8 aa uongozi. Miongoni mwa waliojitokeza walikuwepo Wasukuma wengi tuu ila mimi nawajua kulikuwa na Wasukuma wawili ambao kama wangepitishwa wangetupatia wawakilishi wazuri the best of the best.

Ikasemekana kuwa mmoja kati ya hao Wasukuma wawili ni member wa the Sukuma Gang!. Then kwenye mchujo ikaelezwa kuwa wamepewa maelekezo hatua ya kwanza kabisa ni kuwakata Wasukuma wote waliojitokeza!. Na kweli Wasukuma woote tukakatwa eti ni Sukuma Gang! This is not fair at all! Taifa linakosa uwakilishi wa watu wazuri kwa ubaguzi wa kijinga kabisa!

Na katika hili naomba na mimi nijiunge kwenye kukemea hii sumu ya ubaguzi mbaya kabisa ya kuwabagua Wasukuma kwa kisingizio cha Sukuma Gang, na naomba kutamka kama kuna Msukuma yoyote popote ameadhibiwa au kubaguliwa kwa kisingizio ni member wa the Sukuma Gang, then dhambi hiyo ya ubaguzi, itawatafuna wabaguzi hao kupitia kitu kinachoitwa karma! Karma haina mswalie Mtume wala haijali nani ni nani!

Paskali
 
Jiulize kwanza kwa nini ni sawa Mtu mweusi kumuita majina ya Kibaguzi Mzungu lkn Mzungu akifanya the same kwa mtu mweusi anaweza hata kufunguliwa mashitaka kwa Ubaguzi? Jibu ni power, mtu mweusi ni weak na Mzungu ni strong ndo maana pia inakubalika kuita Sukuma gang na kukejeli Sukuma jinsi utakavyo lkn Msukuma haruhusiwi kufanya the same kwa wengine bila ya consequences.

Hivyo kwangu Wasukuma ni powerful na wengine ni weak ndiyo maana weak wako sensitive.

Fikiria tu kwa mfano kilema cha macho alichoumbwa nacho Mbowe labda angeumbiwa nacho Magufuli hali ingekuwaje, unafikiri wangemsitiri kama Mbowe anavyositiriwa? Hata watu wanaomchukia Mbowe bado wanamsitiri sijawahi kusikia mtu akikejeli macho ya Mbowe lkn ule upande mwingine wasingejali hivyo ni swala kukosa power, maturity na pia lack of boundaries, Wasukuma wanajua wanajitambua na wanajua power yao na wanaowakejeli ni weak na cowards!
 
Na sijui unataka tukemee nini,hivi unakataaje kitu ambacho kipo.Magufuli alijaza Wasukuma Serikalini na wengine uwezo hamna kabisa.

Hao watu waliojazw na Magufuli Serikali ni kanzia kwenye Junior posts mpaka kwenye senior posts hadi kwenye siada ndio wanaounda hiyo Sukuma Gang.

Jambao LA msingi ni kuhakikisha hili jambo halitokei tena.
 
Haijalishi ubaguzi unafanyika kwenye eneo gani ila sio jambo la kuliacha limee na kukua.

Ubaguzi ni mbaya kwa anaye baguliwa, huzalisha chuki ndiyo maana Mwalimu Nyerere kwa kulitambua hili aliweza kumchukua Mmakonde wa Tandahimba na kumfanya DC Monduli.

Au Mkurya wa Tarime na kumfanya Mkurugenzi wa Halmashauri Masasi.

Kama Nchi, tusimame na kukemea Ubaguzi wowote dhidi yetu Watanzania.

Mambo yakiharibika, hatuna Nchi nyingine ya kukimbilia zaidi ya hii tuliyonayo.
 
Watu wote hao hawawezi kuwa wrong

Kila mmoja anayajua yaliyotokea na tutakaa nayo moyoni
Yale mazuri na mabaya pia kwani ndio Dunia ilivyo

Kuna watu hawaamini ukimwi mpaka leo wakisema ni myth
Wengine wanasema Holocaust ilitengenezwa na wanaamini hivyo

Kwa kweli kuna vijana wengine wanasema vita ya kwanza haikutokea

Sasa acha na mimi niamini ninachoamini
 
Pascal njaa kali Kwa mujibu wa mwenda zake..

" The Sukuma Gang ni a fictitious Group that doesn't exist in reality lililobiniwa na yule Kigogo wa Twitter na watu wajinga wajinga wenye akili fupi wakaamini hili kundi ni kweli lipo!. Kiukweli kabisa Sukuma Gang sio kundi la kweli, halipo popote and don't exist anywhere in reality except ndani ya vichwa vya watu waliofilisika kisiasa!."

Nguli wa habari na mwanasheria msomi nchini umeamua kuja kuleta mada ambayo unaamini ni fictitious tena ya watu waliofilisika kisiasa.Tukubali au tukatae Kanda ya nyonyo ndio chimbuko la ukabila Kwa hivi karibuni toka aingie mwendazeke.Kuna Kanda zilisahaulika kabisa Hadi kufikia mtukufu kusema hatapeleka maendeleo Kwa sababu hawakumchagua.
 
Sukuma gang na panya road ndiyo magenge ya kihalifu yakukemewa

Nadhani criminology and penology inataka jinai ikemewe na jamii ione hakuna manufaa kwa kuwa muhalifu au kushiriki uhalifu

Kuwa mualifu ni kufanya, kusaidia na kuchochea

Kushiriki nikuwa a part of transaction au ku-conspire

Now, Sukuma gang ni watu sadist, wanaopenda kuona wenzao wanaishi kama mashetani, kwa kutenda jinai, malicious prosecutions eventually kula hela za plea bargain.

Wamepoteza 1.5 Trillion, wamefanya upigaji kwenye manunuzi ya ndege na miradi mikubwa ya kipigaji

Hao ni watu hatari kuliko panya road, tuwakemee kwa nguvu zetu zote

Hakuna mtu mwenye matatizo na wasukuma, bali sukuma gang
 
Sio Sukuma gang tu kuna maneno mengi tu yanayotumiwa na mabeberu kudhalilisha jamii isiyo fanana na Wazungu. Lugha hiyo inatumika humu JF sana tu, na cha kusikitisha, unakuta na kusikia mpaka Viongozi wakuu wa Serikali na Vyama wanakurupuka na kutumia maneno hayo/misamiati hiyo! Waandishi wa habari ndio usiseme!

Tukirudi humu mitandaoni hawa wabaguzi wanatumia kauli za Viongozi hao kuendeleza ugaidi wa mitandaoni, ugaidi dhidi ya jamii fulani-its pathetic and abhorring. Kwa kurudia hizo kauli. Inaudhi kweli.
 
Back
Top Bottom