Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,480
- 7,443
Ebu fikiria kama tungeendelea na ule mchezo wa kuchekeana chekeana bila tumbua tumbua mambo yangekuwaje? Ukiangalia upande mmoja wa shilingi ni lazima uigeuze na upande wa pili ili ujihakikishie kuwa ni real.
Habari ya wizi wa kura imeingia vipi?Unamtumbua mtu humpeleki mahakamani tuone amefungwa, kama sio maigizo ni nini? Kinachowafanya wanaoigiza picha la kutumbua wasipeleke wezi wenzao mahakamani, unakuta hao wanaowatumbua ndio hao hao waliowatumia kufanikisha wizi wa kura ili wao wakae madarakani. Sasa hapo wanaishia kwenye maigizo ya kutumbua, na sio kupeleka mahakamani maana wote ni wachafu.
Habari ya wizi wa kura imeingia vipi?
Tumbua tumbua inaingia mwaka wa 6 sasa, hayo maigizo yenu ya wizi wa kura hayana hata miezi 2; sasa hivyo vitu viwili vinaendanaje? Hivi nyie makamanda mnakwama wapi linapokuja swala la reasoning?Unamtumbua mtu humpeleki mahakamani tuone amefungwa, kama sio maigizo ni nini? Kinachowafanya wanaoigiza picha la kutumbua wasipeleke wezi wenzao mahakamani, unakuta hao wanaowatumbua ndio hao hao waliowatumia kufanikisha wizi wa kura ili wao wakae madarakani. Sasa hapo wanaishia kwenye maigizo ya kutumbua, na sio kupeleka mahakamani maana wote ni wachafu.
Ukifuatilia sequence ya matukio ya tumbuatumbua kama una akili zako utakuta zoezi hili lilianza mara tu Awamu ilipoingia madarakani na waliotumbuliwa walikuwa wasomi, wataalam na weledi walioajiriwa na Awamu za nyuma na nafasi hizo wakipewa walioteuliwa na Awamu hii. Teuzi hizi zilifanywa kwa upendeleo wa "nani anatoka wapi" lakini zoezi halikuleta matokeo yaliyotegemewa na malalamiko ya wananchi yakazidi ndo teua/tengua ikaanza mpaka wakuteua wakaisha ikabidi waliotenguliwa wateuliwe tena na wakiteuliwa tena watenguliwe tena mpaka kieleweke. Muhula huu uteuzi haujakamilika lakini sasa hawateuliwi na kutenguliwa bali maagizo toka juu yanatolewa mtumishi asimamishwe kazi na kaimu achaguliwe kabla ya uteuzi kufanyika. Hata kukicha bado shuka inahitajika maana baridi ingaripo!Natoa onyo kwa Watanzania wote wenye mapenzi na nchi yao tusipende kushabikia mambo bila kuyachuja kama yana manufaa kwetu.
Hii dhana ya kutumbua majipu, imeipatia sifa serikali ya awamu ya tano. Hii ni kwa sababu tumbua tumbua imeonekana kama ni dawa ya wazembe na mafisadi.
Lakini kila tumbua tumbua ikifanyika mimi binafsi sioni mabadiliko ya kiutendaji kwa wateule wa Rais wa JMT.
Nasema hivi tumbua tumbua ni moja ya adhabu ya kuwafanya viongozi waogope kufanya makosa. Lakini mbona hawaachi? Mbona hawabadiliki?
Hii ni dhahiri kuwa tumbua tumbua haina tija kwa Watanzania. Maana ni kama maigizo yenye kuwafurahisha watazamaji wachache kati ya wengi ambao hawajafurahi maana baada ya igizo hakuna walicho nufaika nacho.
Katumbuliwa DED Igunga watu wamefurahi, lakini ukiuliza Watanzania ni kilio cha aina moja kimetawala. Viongozi wasiojali kero za Wananchi, wasio na huruma, waliovimba matumbo.